Saturday, 24 December 2016

MWENYEKITI MPYA WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JAJI SEMISTOCLES KAIJAGE AANZA KAZI RASMI.



Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan (kushoto) akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kulia) kwenye Ofisi za Tume zilizoko Posta jijini Dar es salaam. Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam kuiongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka 5.

Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakimpokea Mwenyekiti mpya wa Tume hiyo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Posta, jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kulia) akiwa Ofisini kwake kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa leo. Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameteuliwa kuongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016.


Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ofisini kwake.
Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage akitoa ufafanuzi kwa vyombo vya Habari kuhusu majina 11 yaliyoteuliwa kugombea Ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani Zanzibar na majina 72 ya wagombea Udiwani kwenye Kata 20 za Tanzania Bara. Picha/Aron Msigwa -NEC



MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHIMIZA ELIMU KWA WATOTO WA KIKE KASKAZINI UNGUJA



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi katika ufunguzi wa Madrasa ya Al-Madrasatul Munawwaratul Islamiyyah ya KilimaninTazari Zanzibar ikiwa sehemu ya ziara yake ya mkoa wa Kaskazini Unguja. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa Sheihiya ya Kilimani waliojitokeza kwa wingi kwenye ufunguzi wa Madrasa ya Al-Madrasatul Munawwaratul Islamiyyah ya KilimaninTazari Zanzibar ikiwa sehemu ya ziara yake ya mkoa wa Kaskazini Unguja. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki dua maalum mara baada ya zoezi la ufunguzi wa Madrasa ya Al-Madrasatul Munawwaratul Islamiyyah ya KilimaninTazari Zanzibar kukamilika ikiwa sehemu ya ziara yake ya mkoa wa Kaskazini Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ramani ya msikiti mkubwa unaojengwa kwa nguvu za wananchi alipotembelea Uwanja wa Jitimai uliopo Kidoti mkoa wa Kaskazini Unguja. 

............................................................................... 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi na walezi wa Tanzania Zanzibar waache tabia ya kuwaoza wasichana wa kike wakiwa na umri mdogo bali wawasomeshe kwa ajili ya manufaa yao ya jamii kwa ujumla.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akizindua madrasa ya kisasa iliyojengwa kwenye eneo la Kilimani na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa msikiti mkubwa kuliko yote nchini Tanzania unaojengwa katika eneo la Jitimai kidoti katika Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa michango ya wananchi katika siku yake ya kwanza ya ziara ya Kikazi Kisiwani Unguja.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kama wazazi na walezi watasomesha watoto wa kike elimu watakayopata itasaidia kwa kiasi kikubwa wasichana hao kufanya maamuzi sahihi na yenye tija katika jamii.

Amesisitiza kuwa pamoja na elimu kuwa ni haki ya msingi kwa mtoto wa kike hivyo ni muhimu kwa jamii nzima ya Zanzibar ihakikishe watoto wa kike wote wanapata elimu kwani watakuwa na uwezo wa kuchagua na kuandaa mustakbali wa maisha yao ya baadaye ikilinganishwa na hali ilivyo sasa kwenye baadhi ya maeneo.

Kuhusu elimu ya dini, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza wazazi na walezi kuwalea watoto katika maadili mema kwa kuzingatia maandiko matakatifu ya Mtume Mohammad (S.A.W).

Amesema vijana wengi wanaolelewa kwa kufuata misingi ya bora ya dini ni vigumu kurubuniwa na kujiingiza katika matendo yasiyofaa katika jamii.

SUALA LA KUACHIANA VITI VYA KUGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI KWA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA)BADO KIZUNGUMKUTI ARUSHA Mwenyekiti mwenza wa Ukawa James Mbatia akiwa na Viongozi wa CUF mkoa wa Arusha Mwenye shati la blue ni Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF)mkoa wa Arusha Zuberi Mwinyi baada ya mazungumzo ya ushirikiano wa ukawa Hotel ya Safari jijini Arusha picha na Maktaba





                                       
                                   
                                        Na Mahmoud Ahmad Arusha.

Suala la kuachiana viti vya kugombea udiwani,ubunge  kwa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)bado kizungumkuti katika Kata ya Mateves wilayani Arumeru  ambapo CUF na CHADEMA wasimamisha wagombea hali inayopelekea kugawa kura za wagombea hao wa Ukawa.

Akizungumza na wanahabari Ofisini kwake Mkurugenzi wa Uchaguzi mkoa wa CUF Arusha Zuberi Mwinyi alisema kuwa wao wamesimamisha mgombea kwenye kata hiyo kutokana na mgombea wao kukubalika kwenye kata hiyo hivyo kuwataka wenzao kuwaachia kata hiyo kwani wanazo kata nyingi kwenye maeneo hayo.

Mwinyi alisema kuwa Tulikuwa na makubaliano ya kuachiana kata na nafasi za Ubunge lakini wenzetu vyama wenza bado wamekuwa na Tamaa ya kusimamisha wagombea kila inapotokea nafasi wemekuwa mbele kusimamisha wagombea bila kujali makubaliano hali inayopelekea sisi kama chama kuamua kusimamisha mgombea wetu eneo hilo.

Alisema kuwa sisi kama CUF tumewaachia wenzetu wa chadema kata zote za jiji la Arusha ambapo walishinda kata 24 na moja kuangukia mikononi mwa chama cha Mapinduzi (CCM), ili hali wao wameshindwa kutuachia kata hiyo moja kama wenza na kutusaidia kuweza kuwa na mwakilishi kwenye vikao vya kutnga sera je huku ni kujenga umoja au kubomoa.

“Tulikuwa na makubaliano ya kuachiana kata na nafasi za ubunge jambo hili limeonekana kushindikana kwa wenzetu kuwa na tamaa huku tukiwadanganya wananchi kwa wimbo wa ukawa ukawa kumbe si hivyo wenzetu wapo kimaslahi zaidi na uroho wa madaraka”alisema Mwinyi.

Akatanabaisha kuwa CUF lazima itachukuwa kata hiyo na kazi ndio imeanza ya kuhakikisha kata inaingia mikononi mwetu tukiwa na lengo la kukijenga chama kuhakikisha mwaka 2020 tunakuwa na viti zaidi vya udiwani na ubunge katika jiji la Arusha na mkoa kwa ujumla.

Suala la mgawanyo wa maeneo ya kugombea limekuwa likivichanganya vyama hivi licha ya kuwepo makubaliano yaliofanywa na vingozi wa vyama vine hali inayoonekana kutokuwa na muafaka katika jambo hili, mfano majimbo ya segerea chadema na cuf walisimamisha wagombea na kujikuta wakiangukia pua katika jimbo hilo,hali inayoonyesha hakuna makubaliano katika hilo.

“tumekuwa tukiongea kweye vikao bila hatua kuchukuliwa na wenzetu wamekuwa waongeaji wazuri kwenye vikao bila utekelezaji hali inayotuwiwa vigumu kukijenga chama na kuwa na viti vya wabunge na madiwani katika mkoa huu kutoka na hila za wenzetu”alisisitiza Mwinyi
Juhudi za wanahabari kuwatafuta viongozi wa CHADEMA mkoani hapa akiwemo Mwenyekiti wa chama na Katibu wa Kanda ya kaskazini wa chama hicho Amani Golugwa ziligonga mwamba baada ya simu zao kutokupokelewa kila walipopigiwa bado juhudi zinaendelea kuwatafuta ili waweze kujibu madai hayo.

Thursday, 8 December 2016

MWENYEKITI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC) RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MKE WA MWANZILISHI WA TAIFA LA SUDAN KUSINI REBECCA NYANDENG DE MABIOR ILIYEAMBATANA NA UJUMBE WAKE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Rebecca Nyandeng De Mabior aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Rebecca Nyandeng Mabior Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Rebecca Nyandeng De Mabior mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mabior Garang Mtoto wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Hayati John Garang De Mabior Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

ZINGATIENI MAADILI NA UWAJIBIKAJI KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YENU: NAPE

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na watumishi wa Wizara yake wakati wa ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi la Wizara  katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza katika kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
 Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Magreth Mtaka akitoa hoja za wafanyakazi katika kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Wizara hiyo lililofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akipokea hotuba ya wafanyakazi kutoka kwa Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara hiyo Bibi Magreth Mtaka katika kikao cha Baraza la wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
 Baadhi ya wawakilishi wa watumishi wa  Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Taasisi zake wakifuatilia kikao cha Baraza la wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi wa Wizara yake mara baada ya kikao cha Baraza la wafanyakazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Desemba 08, 2016. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM


Na Raymond Mushumbusi -WHUSM
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewataka watendaji na watumishi wa Wizara yake kuzingatia maadili na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao.

Ameyasema hayo wakati akifungua Baraza la wafanyakazi la Wizara yake na kusisitiza kwa watendaji kuwasimamia watumishi walio chini yao kuzingatia maadili na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao katika kutoa huduma kwa wananchi.

Ameongeza kuwa kuwepo kwa ushirikiano kati ya uongozi na watumishi utasaidia kufanikisha masuala mbalimbali ya maendeleo ya Wizara, Taasisi zake na watumishi katika kuleta maendeleo ya Wizara katika kutimiza wajibu wao.

“Nawataka watumishi wazingatie maadili katika kutekeleza wajibu wao na naamini kwa juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano  tutarudisha maadili ya Utumishi wa Umma na bado taratibu zinaendelea kusimamiwa ipasavyo”asisitiza Mhe Nnauye.

Mhe. Nnauye amesisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli ana mpango wa dhati wa kurujesha maadili katika Utumishi wa Umma na kuhakikisha heshima yake inarudi.

Alieleza kuwa endapo kuna mtumishi yoyote atakayeshindwa kusimamia suala zima la maadili anapoteza utumishi wake.

“ Wananchi ndiyo tunaowatumikia na ndiyo wanaotufanya tuwepo hapa tulipo wanahitaji huduma bora. Kama hatutazingatia suala la maadili ni hakika hatutaweza kuwatumikia vema” alieleza.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara hiyo , Prof Elisante Ole Gabriel ameahidi kutekeleza agizo hilo kwa  kuhakikisha watumishi wanazingatia maadili na suala hili linafanyika kwa vitendo zaidi na sio maneno ili kuendelea kuunga mkono jitihada za  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli za kurudisha maadili katika Utumishi wa Umma.

“Mhe. Waziri nakuahidi mimi pamoja na watendaji wenzangu tutalisimamia suala hili na kulitekeleza kwa vitendo ili turudishe heshima ya utumishi wa Umma kwa kutoa huduma bora kwa wananchi na kurudisha uaminifu kwa wananchi”alisema Prof Gabriel.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Magreth Mtaka amesema kuwa ni jambo muhimu kwa watumishi kuzingatia maadili katika utekelezaji wa majukumu yao katiKa eneo la kazi.

“Niwashauri watumishi wenzangu tuzingatie maadili ya Utumishi wa Umma ili turudishe heshima ya utumishi wa umma na tutoe huduma iliyo bora kwa wananchi” alisema Bibi Magreth.

UWEPO ZA SHERIA ZA HABARI NA SHERIA ZA HAKI YA KUPATA TAARIFA HUSAIDIA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA- BI. ALINA MUNGIU

 Mtafiti katika masuala ya habari Bi. Alina Mungiu (wakwanza kulia)akijibu maswali wakati wa kikao cha Asasi za Kiraia katika mkutano wa Nne wa Mpango wa uendeshaji wa serikali kwa uwazi Jijini Paris Nchini Ufaransa ambapo alieleza jinsi uwepo za sheria za habari na sheria za haki ya kupata taarifa zinavyoweza kusaidia katika mapambano dhidi ya rushwa.
 Mkurugenzi wa Ushirikishwaji wa Asasi za Kiraia Bw. Paul Maasen akiongea na washiriki wa mkutano wa Nne wa Mpango wa uendeshaji wa serikali kwa uwazi Jijini Paris Nchini Ufaransa ambapo alisema serikali kutoa huduma kwa uwazi kutasaidia kuondoa vitendo vya rushwa na uwazi.
 Washiriki wa mkutano wa Nne wa Mpango wa uendeshaji wa serikali kwa uwazi Jijini Paris Nchini Ufaransa wakimsikiliza Mkurugenzi wa Ushirikishwaji wa Asasi za Kiraia Bw. Paul Maasen.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Nne wa Mpango wa uendeshaji wa serikali kwa uwazi Jijini Paris Nchini Ufaransa wakishiriki katika majadiliano ya masuala mbalimbali yanayohusiana na mpango wa uendeshaji wa serikali kwa uwazi
Mtafiti katika masuala ya habari Bi. Alina Mungiu akitoa mada kuhusu namna asasi za kiraia na ukuaji wa teknolojia unaweza kusaidia katika mapambano dhidi ya rushwa.

PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO-PARIS (UFARANSA)

WAZIRI WA BIASHARA, VIWANDA NA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NCHINI RWANDA, FRANCOIS KANIMBA ATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM.

Waziri wa Biashara, Viwanda na Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Rwanda, Francois Kanimba akizungumza na waandishi habari mara baada ya kutembelea bandari ya Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charle’s Mwijage
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charle’s Mwijage akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumtembeza Waziri wa Biashara , Viwanda na Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Rwanda, Francois Kanimba katika bandari ya Dar es Salaam leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Rwanda, Francois Kanimba akipata maelezo ya Bandari ya Dar es Salaam kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Biashara , Viwanda na Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Rwanda, Francois Kanimba akitembelea bandari ya Dar es Salaam ikiwa sehemu ya mkutano wa siku mbili wa kujadili masuala ya biashara kati ya Tanzania na Rwanda leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

DK MEDARD KALEMANI AFANYA ZIARA MIKOA YA RUVUMA, NJOMBE, IRINGA NA MOROGORO KUKAGUA MIRADI YA UMEME

 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (katikati) akizungumza na wananchi wa Kata ya Ulaya wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro, kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini (REA II na REA III), wakati wa ziara yake wilayani humo hivi karibuni.
 Diwani wa Kata ya Ulaya wilayani Kilosa, Matokeo Kenedi (kushoto), akimweleza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (kulia) mahitaji ya umeme kwa wananchi wa Kata yake, wakati wa ziara ya Naibu Waziri kukagua miradi ya umeme wilayani humo hivi karibuni. Kulia kwa Naibu Waziri ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Hassan Saidy.
 Nehemia Magendege kutoka Kijiji cha Ng’uruhe, Kata ya Pomerini wilayani Kilolo, akitoa maoni yake kuhusu utekelezwaji wa Miradi ya Umeme Vijijini (REA II na REA III) kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa ziara yake wilayani humo hivi karibuni.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kushoto), akiwasilisha taarifa ya Mkoa wake kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (kulia-mwenye miwani). Naibu Waziri na Ujumbe wake walifika Ofisini kwa Mkuu huyo wa Mkoa hivi karibuni, kabla ya kuanza ziara mkoani humo kukagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme.
 Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mugoyi Adam (wa pili kutoka kulia), akizungumza na wananchi wa Kata ya Ulaya (hawapo pichani), wakati wa ziara ya Naibu Waziri, Dk Medard Kalemani (kulia) wilayani humo hivi karibuni, kukagua miradi ya umeme.
Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Kata ya Ulaya wilayani Kilosa, Dk Edmund Mjengwa (kushoto), akimueleza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (kulia) mahitaji ya umeme katika Kituo hicho. Naibu Waziri ameelekeza Kituo hicho kiwe cha kwanza wilayani humo, kuunganishiwa umeme katika Mradi wa REA III.