Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji, Mh Charles Mwijage amezindua rasmi Kamati ya Kuboresha Mazingira ya Biashara Tanzania,Kamati yenye lengo la kufanya uchambuzi wa kina wa kufanya biashara nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kamati hiyo jijini Dar es Salaam,Waziri Mwijage amesema utashi wa Serikali ya Awamu ya Tano ni kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi unaoongozwa na viwanda kama inavyoelekezwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.
Amesema kuwa “Uwekezaji wa mazingira bora ni zoezi endelevu hivyo kazi yetu Sekta ya Umma na Sekta binafsi ni kujipima katika maboresho”.
Katibu Mkuu-Sera,Ofisi ya Waziri Mkuu(PMO),Dkt.Hamisi Mwinyimvua amezungumzia Jitihada za Serikali kuhusu Maboresho ya Mazingira ya Biashara zilizokwisha fanyika na kuahidi kuendelea kufanyika.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage akizungumza na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Biashara wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Kuboresha Mazingira ya Biashara jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu-Sera,Ofisi ya Waziri Mkuu(PMO), Dkt.Hamisi Mwinyimvua akizungumzia Jitihada za Serikali kuhusu Maboresho ya Mazingira ya Biashara zilizokwisha fanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Charles Mwijage akiwa katika picha ya pamoja na ziongozi mbalimbali jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
No comments:
Post a Comment