Thursday, 8 September 2016

KAMANDA SIRRO AWATOA HOFU WANAPANGAJI WA NYUMBA ZA WAGENI JIJINI DAR


Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam anatoa rai kwa wakazi wa Jiji la Dar Es salaam na wageni wanaoingia jijini wakitokea mikoani  kupuuza  taarifa za sauti  zinazozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Polisi wanawakamata ovyo watu wanaolala kwenye nyumba za kulala wageni. 

Taarifa hizo za uvumi  zinazoendelea kuzagaa  kwenye mitandao ya Kijamii kama WHATSAPP, TELEGRAM na pia zimechapishwa kwenye baadhi ya magazeti kwamba Askari Polisi wanawakamata watu  ovyo mchana wakiwa kwenye nyumba za kulala wageni  kwa madai ya kukamata kwa makosa ya uzembe na uzururaji na pia kutimiza kauli ya Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ‘HAPA NI KAZI TU’.

Kimsingi niwatoe hofu raia wema kuwa tunaendelea na oparesheni za kuwasaka watuhumiwa wa makosa mbalimbali yakiwemo wanaofanya biashara ya nyumba za kulala wageni kinyume cha sheria (guest bubu), mjambazi na wahalifu wengine wa makosa mbalimbali.

 Aidha taarifa za kuaminika zimebaini kuwa baadhi ya nyumba za kulala wageni zimekuwa zikitumika kuhifadhi magenge ya wahalifu, dada poa na kaka poa, hivyo Jeshi la Polisi tunawajibika kufuatilia na kuwakamata wahalifu.

Niwajibu wa Polisi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye nyumba za kulala wageni, Hoteli, migahawa, Vilabu vya vileo,  kumbi za starehe zinazokesha na zisizokesha na watakaobainika kuvunja sheria, hatua kali za kisheria dhidi yao zitachukuliwa. Sheria ya Mwenendo ya makosa ya jinai kifungu cha 60(1) (sura ya 77 iliyofanyiwa marekebisho 2002) kinampa nguvu askari kufanya ukaguzi wa maeneo yote yaliyotajwa hapo juu na kumkamata mtu yeyote anayetiliwa shaka akienda kinyume na utaratibu wa biashara hizo. 

Sambamba na hayo nawatahadharisha wafanyabiashara wote wa nyumba za kulala wageni wafuate taratibu za kupokea wageni kwa kuandika kwenye vitabu, kuandika namba za vitambulisho vyao na sehemu wanayotoka, na pale watakapomtilia mashaka mteja yeyete watoe taarifa kituo chochote cha polisi. 

Pia wenyeviti wa serikali za mitaa na wajumbe wa nyumba kumi wanawajibika kuwatambua wageni wote wanaoingia kwenye himaya zao na kuwachukulia hatua stahiki ili kuimarisha usalama katika jiji letu la  Dar Es salaam.

DAR ES SALAAM BILA UHALIFU INAWEZEKANA, TUSHIRIKIANE KUISAFISHA JIJI LETU

S.N.SIRRO - CP
 KAMISHNA WA POLISI
KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

MAKAMU WA RAIS AZINDUA JENGO LA SEKRETARIETTI YA MAADILI YA UMMA KANDA YA KUSINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Kamishna wa Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda mara baada ya kuwasili kwenye halfa fupi ya uzinduzi wa jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara 
 Jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa halfa fupi ya uzinduzi wa jengo la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Kusini mkoani Mtwara 
  Kamishna wa Tume ya Sekretarieti ya Maadili ya Umma Jaji Mstaafu Salome Kagandaakihutubia kwenye hafla hiyo
 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Ofisi ya Rais Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki akihutubia kwenye hafla hiyo.
                                        ................................................... 

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameiagiza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Nchi kuchunguza na kuwachukulia hatua kisheria na za kinidhamu viongozi na watumishi wa umma ambao wanakiuka taratibu za kazi kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
 
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 8-Sep-2016 mjini Mtwara wakati anafungua jengo la sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya Kusini ambalo ujenzi wake umegharimu takribani shilingi Bilioni mbili.

 
Makamu wa Rais amesema iwapo kama hatua hizo zitachukuliwa haraka zitakomesha na kupunguza kasi ya mmomonyoko wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma hali ambayo itaongeza uwajibikaji katika utendaji wa kazi miongoni watendaji hao.
 
Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuiimarisha sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma nchini kwa kuijengea uwezo wa rasilimali watu na fedha kwa kadri hali ya uchumi itakavyo ruhusu ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
 
Makamu wa Rais amewahimiza viongozi na watumishi wa umma kuthamini na wahakikishe walinda maslahi ya umma wakati wote wa utendaji wao wa kazi ili kuondoa malalamiko kwa wananchi.

 
Makamu wa Rais amesema ni jambo la muhimu kwa sekretarieti hiyo kufutilia mienendo ya viongozi wa umma na kuwabaini wale wanaokwenda kinyume na misingi ya uadilifu na wachukuliwe hatua ipasavyo kabla hawaleta madhara kwa serikali na jamii kwa ujumla.
 
Makamu wa Rais pia ametoa rai maalum kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara kuitumia ofisi hiyo mpya ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya Kusini kwa kutoa taarifa kuhusu mienendo ya viongozi wanaokiuka maadili ya umma katika utendaji wao wa kazi ili waweze kuchukuliwa hatua.
 

 
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki amesisitiza kuwa kazi ya kuhakiki mali na madeni ya viongozi wa umma itaendelea kwa kasi nchini na mwaka huu sekretarieti hiyo itahakiki mali za viongozi wapatao 500 kote nchini.
 
Naye Jaji Mstaafu na Kamishna wa Maadili Nchini Salome Kaganda akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa jengo hilo ameiomba serikali itenge fedha za kutosha kwa ajili ya kufanikisha zoezi la uhakiki wa mali na madeni ya viongozi kwa nchi nzima.

Wednesday, 7 September 2016

MATUKIO YA BUNGENI MJINI DODOMA.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (MB) akimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba Leo Bungeni Mjini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wakiingia katika ukumbi wa bunge kuhudhuria kikao cha 2 cha bunge la kumi na moja  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mbunge wa Jimbo la Urambo Mhe.Margaret Sitta akimueleza Jambo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa leo Mjini Dodoma.
Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akijibu swali wakati wa kikao cha 2 cha bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alitoa wito kwa waajiri nchini kuwasilisha nyaraka za wastaafu kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii miezi mitatu hadi sita kabla ya kustaafu kwa wateja wao ili kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza.

TSSA YATOA TAARIFA KWA SERIKALI JUU UKUZAJI UCHUMI NA UJEZI WA VIWANDA NCHINI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Viajana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama akizungumza wakati wa Mkutano wa kupokea taarifa ya Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA), juu ya hatua iliyofikiwa na Mifuko hiyo katika ukuzaji Uchumi na ujenzi wa Viwanda nchini, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa LAPF Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA), Meshach Bandawe akizungumza  wakati wa Mkutano wa kutoa taarifa kwa Serikali  juu ya hatua iliyofikiwa na Shirikisho hilo katika ukuzaji Uchumi na ujenzi wa Viwanda nchini, uliofanyika Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara ambaye pia ni Mjumbe wa Shirikisho hilo, akichangia mada katika Mkutano wa kupokea taarifa ya Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA), juu ya hatua iliyofikiwa na Mifuko hiyo katika ukuzaji Uchumi na ujenzi wa Viwanda nchini, uliofanyika Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka akizungumza wakati Mkutano huo uliotoa taarifa kwa Serikali  juu ya hatua iliyofikiwa na Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA) katika ukuzaji Uchumi na ujenzi wa Viwanda nchini, uliofanyika Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Mkutano huo uliotoa taarifa ya Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA), juu ya hatua iliyofikiwa na Mifuko hiyo katika ukuzaji Uchumi na ujenzi wa Viwanda nchini, uliofanyika Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mwenyekiti wa Shirikisho hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa LAPF, Eliud Sanga.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha wakifatilia kwa makini taarifa hiyo iliyokuwa ikitolewa na Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA), juu ya hatua iliyofikiwa na Mifuko hiyo katika ukuzaji Uchumi na ujenzi wa Viwanda nchini.
Katibu Mkuu ofisi ya Waziri wa Nchi, katika Ofisi ya Waziri Mkuu, 
Sera, Bunge, Kazi, Viajana, Ajira na Walemavu, Eric Shitindi (kulia) akiwa na  Mwenyekiti waShirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa LAPF, Eliud Sanga wakifatilia Mkutano huo.
Wajumbe wa Mkutano huo kati ya Serikali na Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA).

WENYE MAJINA HAPO CHINI WATAKIWA KUONANA NA MWAJIRI WAO-MAHAKAMA.

Tunaomba kutoa taarifa kuwa, wenye majina na anuani hapo chini ambao ni watumishi/walikuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania wanahitajika kupata taarifa muhimu na maalum juu ya masuala yahusuyo Utumishi wao: Wafike na kuonana na Bibi. Agatha Ng’ingo – Mkurugenzi Msaidizi- Idara ya Utawala na Utumishi, namba ya simu (0673 – 001 773) ndani ya siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili.
S/N
JINA KAMILI
CHEO
KITUO CHA KAZI
C/N

1
BW. ROBERT WILLIAM CHAGAKA
DEREVA II
MAHAKAMA YA WILAYA IRAMBA
111824992

2
BW. GODLISTEN MOSES MWANRI
DEREVA II
MAHAKAMA YA WILAYA KISHAPU
111827839


3
BI. AGNES AUDAX RWEGOSHORA
HAKIMU MKAZI II
MAHAKAMA YA MWANZO UJIJI KIGOMA
111838464

4
BI. HAPPINESS ELIAS MISHWARO
HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO MWANDAMIZI
MAHAKAMA YA WILAYA MBARALI
10915901

5
BW. BARAKA JAFARI MUKAMA
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II
MAHAKAMA YA WILAYA ILALA
9927780

6
BW. RAMADHANI MOHAMED KILYOUSUNGU
MLINZI
MAHAKAMA YA WILAYA RUFIJI
9496501

7
BI. REHEMA SAMWEL PANDAPANDA
HAKIMU MKAZI II
MAHAKAMA YA WILAYA MPWAPWA
9927919

8
BI. HAWA GODREY MKUMBO
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II
MAHAKAMA YA WILAYA KASULU
8203232

9
BW.CHRISTINA JOHN MAYILA
MSAIDIZI WA OFISI MWANDAMIZI
MAHAKAMA YA WILAYA KAHAMA
7758540

10
BW. YASSINI WAZIRI MASELE
MLINZI
MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI SINGIDA
111400187

11
BW. JOSEPH FRANCIS BOMA
MLINZI
MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI SINGIDA
111397724

12
BW. BRUTON RABIEL KIMARO
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II
MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI MANYARA
7203497

13
ABIHUDI GILLIARD MASEU
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II
MAHAKAMA KUU ARUSHA
5187924

14
HUSSEIN HASSAN BACHOO
AFISA UGAVI I
DAR ES SALAAM
5529186

15
ASHA MAGOMBA ABDALLAH
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II
MAHAKAMA YA WILAYA MONDULI
111827925

16
BW. AMRI MUSSA RASHIDI
MLINZI
MAHAKAMA YA WILA
YA TANDAHIMBA
9544435

Imetolewa na,
MTENDAJI MKUU.