Baadhi
ya wazazi na walezi wakisubiri kuingia kwenye chumba cha daktari kwa
ajili ya watoto kuchunguzwa kama wana matatizo ya moyo. Watoto
watakaobainika watafanyiwa upasuaji na wazazi watatakiwa kuchangia
gharama.
John Stephen, MNH
Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo imeanza kupima watoto bure ili
kubaini kama wana matatizo ya moyo watachangia gharama za upasuaji.
Wazazi
na walezi wenye matatizo ya moyo wamejitokeza kwa wingi leo katika
taasisi hiyo wakiwa na watoto na kupatiwa vipimo ili kubaini matibabu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi amesema kwamba watoto
watakaobainika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa upasuaji.
“Watoto
watakaobainika kuwa tatizo tutawafanyia upasuji, wazazi wanatakiwa
kuchangia kiasi cha fedha ili kukamilisha matibabu kwa watoto
husika,”amesema Profesa Janabi.
Taasisi
hiyo imeanza shughuli ya kuwapima watoto ili kubaini kama wana matatizo
ya moyo na kuwafanyia upasuaji. Pia, watu wazazi wametakiwa kujtokeza
kwa ajili ya watoto kufanyiwa upasuaji.
Baadhi
ya wazazi wakiwa na watoto katika chumba cha Dk Stella Mongella
wakisubiri watoto wao kufanyiwa vipimo Leo kwenye Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete (JKCI).
Leo Dk Sulenge Kubhoja wa taasisi hiyo, akimchunguza mtoto Lisa Mashauri (2), mkazi wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam.
Dk Sulenge Kubhoja akiendelea na uchunguzi kwa mtoto Hellen Emmanuel kutoka mkoani Iringa.
Baadhi ya wazazi na walezi wakiwa na watoto wao leo nje ya taasisi hiyo kabla ya kuingia katika chumba cha daktari leo.
No comments:
Post a Comment