Amesema kuwa majambazi walikiri kuwa na wenzao wako katika msitu wa Vikindu.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha kifaa cha kuangalia wakati wakifanya uhalifu majambazi kwa waandishishi wa habari ikiwa ni sehemu ya vifaa vilivyokuwa vikitumika na majambazi sugu leo katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha bunduki kwa waandishi wa habari ikiwa ni sehemu yabunduki zilivyokuwa zikitumika na majambazi sugu leo katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na waandishi habari juu ya operesheni walioifanya na kukamata majambazi watatu katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo jijini Dar es Salaam.
Chalila Kibuda wa Michuziblog.
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam limefakiwa kukamata watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi
hatari ambao wamekuwa wakishiriki matukio mbalimbali ya uhalifu kwa
kutumia silaha.
Watu hao wanaodaiwa kuwa majambazi
walipatikana na bunduki 23 za aina tofauti tofauti, Risasi 835, kifaa
cha kuzuia risasi kuingia mwilini tatu (Burret Proof), Sare za Polisi,
Pingu 48 pamoja na Radio 12 za mawasiliano.
Akizungumza na waandishi wa habari katika
viwanja vya kanda maalum, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es
Salaam Kamishna, Simon Sirro amesema kuwa majambazi hao walikuwa na
mtandao mkubwa ikiwa ni kununua silaha nje ya nchi kwa ajili ya
kufanyia uhalifu katika maeneo mbalimbali.
Kamanda Sirro amesema baada ya tukio hilo
timu ya polisi ya upelelezi iliweka mtego na kufanikiwa kukamata
majambazi watatu maeneo ya Mbagala, Keko na Kawe.
Kamanda Sirro amesema katika mahojiano
walikiri kufanya tukio katika benki ya Habib African maeneo ya Kariakoo
2014 na Stanbic 2014.
No comments:
Post a Comment