Saturday, 19 November 2016

TRA YAONGEZA MUDA WA KUBORESHA TAARIFA ZA WALIPAKODI HADI JANUARI 2017


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuwashukuru wakazi wa Dar es Salaam kwa  kushiriki katika zoezi la kuhakiki Namba ya Utambulisho Mlipakodi (TIN).

Kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi kutaka kuhakiki taarifa zao, Mamlaka imeamua kuongeza muda wa uhakiki hadi tarehe 31 Januari, 2017. Pamoja na kuongeza muda wa uhakiki, Mamlaka pia imeongeza vituo vya kuhakiki

TRA pia inawakumbusha wananchi kuwa wale wenye TIN za biashara wanatakiwa kuhakiki katika ofisi za kodi Mkoa husika na wenye TIN zisizo za biashara (yaani TIN iliyotokana na maombi ya leseni ya udereva au ya kuingiza mzigo bandarini) wanaweza kuhakiki katika kituo chochote hapa Dar es Salaam.

Vituo vya uhakiki vilivyopo ni kama  ifuatavyo:
Pamoja na vituo hivyo, Mamlaka imeanzisha kituo kinachohama (Mobile Office) ambacho kinatoa huduma sehemu mbalimbali.  Ili kuongeza ufanisi, Mamlaka itaendelea kuboresha huduma zake kwa kuongeza vitendea kazi na vituo vingine vya kuhakiki.

Mwisho, Mamlaka inawasihi  wananchi kuepuka kutumia  Matapeli (Vishoka) kwani zoezi hili linamtaka mlengwa kufika mwenyewe kwenye kituo husika.


Kwa ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana na kituo cha huduma kwa walipakodi kwa kupiga simu za bure: 0800 780078 / 0800 750075 barua pepe: huduma@tra.go.tz

Pamoja Tunajenga Taifa Letu

Limetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA- Makao Makuu

JUMIA TRAVEL YATOA TUZO KWA HOTELI ZINAZOFANYA VIZURI NCHINI TANZANIA




 Meneja Mkaazi wa Kampuni ya Jumia Travel Tanzania, Fatema Dharsee (kushoto), akielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo.

 Hafla ikiendelea.

 Wadau wakiwa kwenye hafla hiyo.

 Meneja Mkaazi wa Kampuni ya Jumia Travel Tanzania, Fatema Dharsee (kulia), akimkabidhi tuzo Flora Rwehumbiza katika hafla hiyo.

Meneja Mkaazi wa Kampuni ya Jumia Travel Tanzania, Fatema Dharsee akimkabidhi tuzo ya  Ushirikiano Mkubwa mwaka 2016 kwa Meneja wa Huduma za Hoteli ya Amaan Bungalows, Daudi Fundi (kushoto). Hafla ya sherehe hizo zilifanyika jana katika ukumbi wa Mayfair jijini Dar es Salaam.

 Meneja Mkaazi wa Kampuni ya Jumia Travel Tanzania, Fatema Dharsee (kulia) akikabidhi tuzo ya Mshirika Bora Katika Biashara mwaka 2016 kwa Mtendaji wa Mauzo wa Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam,  Emma Sizya.

Meneja Mkaazi wa Kampuni ya Jumia Travel Tanzania, Fatema Dharsee (kushoto), akizungumza na wanahabari.
Na Dotto Mwaibale
MTANDAO unaoongoza kwa huduma za hoteli kwa njia ya mtandao barani Afrika wa Jumia Travel umetoa tuzo kwa hoteli na washirika wake wakati wa hafla fupi iliyofanyika siku ya Alhamisi katika ukumbi wa hoteli ya Mayfair jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa sherehe za utoaji wa tuzo hizo zilizofanyika Dar es Salaa jana, Meneja Mkaazi wa Jumia Travel Tanzania Fatema Dharsee alibainisha kuwa tuzo hizo zimelenga kuleta chachu katika matumizi ya huduma za hoteli mtandaoni nchini na kupanua wigo wa huduma kwa wateja.
“Leo hii tumejumuika hapa kuzitambua na kuzitunuku hoteli zinazotoa huduma nzuri pamoja na kupendwa na wateja wa ndani na nje ya nchi. Mbali na sababu hizo lakini kikubwa zaidi ni kwa hoteli hizi kuendana na mabadiliko ya teknolojia kupitia mtandao wa intaneti ambao unawezesha huduma zao kufikiwa na mtu yeyote duniani,” alisema Dharsee.
“Hoteli zote zilizojiunga au kujumuishwa kwenye mtandao wetu wa ‘Extranet’ zinazo fursa kubwa za kuongeza ufanisi na thamani ya biashara yao kwani hazitegemei tena wateja wanaokwenda moja kwa moja kutafuta huduma kwenye meza zao za maulizo. Kupitia mtandao wetu ambao unapatikana kwenye kompyuta, tabiti na simu, unamwezesha meneja wa hoteli au mapokezi mahali popote walipo mbali na vituo vyao vya kazi kupokea maombi ya wateja kisha kuthibitisha au kubatilisha upatikanaji wa huduma husika,” aliongezea Dharsee
Aliendelea mbele kwa kufafanua zaidi kuwa vipengele vya tuzo za Jumia Travel Tanzania vilivyokuwa vikiwaniwa ni pamoja na:
Chaguo la Wasafiri – hii ilitolewa kutokana na maoni ya wateja au wageni wengi walioitembelea; Hoteli Iliyoonesha Ushirikiano Mkubwa – hii ilitolewa kwa kigezo cha kuthamini mchango na ushirikiano wake; Hoteli Bora Inayochipukia – hii ilitolewa kutokana na juhudi na jitihada zilizooneshwa katika sekta nzima kwa ujumla; Hoteli Iliyopokea Maombi Zaidi Kutoka Kwa Wateja – hii ilitolewa kwa mujibu wa kuwa na maombi mengi kutoka kwa wateja; na Mshirika Bora Katika Biashara – hii ilitolewa kwa kutuunga mkono na mchango mkubwa katika biashara.
“Ningependa kutoa shukrani za dhati kwa hoteli zote zilizokubali wito na kuhudhuria hafla hii. Uwepo wenu hapa jioni ya leo unaonyesha kutuamini na kuunga mkono jitihada za kuinua sekta ya utalii na ukarimu nchini hususani kuhamasisha kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani,” alihitimisha Meneja Mkaazi huyo wa Jumia Travel nchini Tanzania.
Katika hafla hiyo hoteli zilizojinyakulia tuzo hizo ni pamoja na Serena ambayo ilitunukiwa tuzo ya Mshirika Bora Katika Biashara; Tanzanite Executive Suites ilitunukiwa tuzo ya Chaguo Bora la Wasafiri; Amaan Bungalows ilitunukiwa tuzo ya Hoteli Iliyoonesha Ushirikiano Mkubwa; Harbour View Suites ilitunukiwa tuzo ya Hoteli Iliyopokea Maombi Zaidi Kutoka Kwa Wateja; na Slipway ambayo yenyewe ilitunukiwa tuzo ya Hoteli Bora Inayochipukia.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo Mtendaji wa Mauzo kutoka Hoteli ya Serena ya jijini Dar es Salaam Emma Sizya amesema kuwa amefarijika kupokea tuzo hiyo na kuipongeza kampuni ya Jumia Travel Tanzania kwa kuja na kitu hiki cha kipekee.
“Kwanza ningependa kuipongeza Jumia Travel Tanzania kwa kuja ni hizi tuzo ambazo ninaamini kuwa zitaleta mchango mkubwa katika kuhamasisha sekta ya hoteli nchini. Tumekuwa tukiona sekta mbalimbali zikiwa na tuzo zao lakini yetu ikiwa imelala kidogo, huu ni mwanzo mzuri na ninaamini waandaaji hawataishia hapa,” alisema na kumalizia Sizya kwamba, “Serena siku zote tunajivunia kuwa mbele katika kuunga mkono jitihada za wadau mbalimbali wanaofanya kazi na sisi.
Lengo letu kubwa ni kuona kuwa kwa pamoja tunashirikiana katika kuwashawishi wateja kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia ambapo sasa hivi kupitia kampuni kama hii unaweza kupata huduma zetu mtandaoni.”
Hafla hiyo imeambatana na kuadhimisha miaka mitatu tangu Jumia Travel kuanzishwa pamoja na kampeni maarufu ya mauzo inayoendelea kwa jina la ‘Black Friday’ ambayo  imeanza Novemba 14 mpaka Novemba 25, 2016. Matarajio ya kampuni kwa wiki hizi mbili za mbili ni makubwa ambapo imelenga kuwapatia wateja fursa ya kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma za awali kwa ajili ya msimu wa sikukuu kwa gharama nafuu. 
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namb

Magazeti ya Leo Jumamosi



KAMILISHENI UJENZI WA MAGOMENI KOTA KWA WAKATI – MAJALIWA



kot7
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mshauri wa Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Edwin Nnuduma  kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipotembelea mradi huo Novemba 18, 2016. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally  Happy.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kot1
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wajenzi wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam kukagua mendeleo ya mradi huo Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kot2
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wajenzi wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam kukagua mendeleo ya mradi huo Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kot3
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipokagua Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam Novemba 18, 2016.  Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Happy. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kot4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mshauri wa Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Edwin Nnuduma  kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipotembelea mradi huo Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya WaziriMkuu)
kot03
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mshauri wa Wakala ya Majengo Tanzania (TBA), Edwin Nnuduma  kuhusu Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam wakati alipotembelea mradi huo Novemba 18, 2016. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally  Happy.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kot6 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watalaamu wa ujenzi wa mradi wa nyumba za makazi Magomeni watumie utaalamu wao vizuri na wakamilishe kwa wakati.
Ametoa agizo hilo leo mchana (Ijumaa, Novemba 18, 2016) wakati alipokagua ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na wataalamu kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) eneo la Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu amewataka wataalamu hao waendelee kufanya kazi hiyo kwa kufuata misingi ya weledi wa taalauma yao kwani Serikali inawaamini. “Muhimu mjue kwamba mmepewa dhamana hii kubwa ya kukamilisha ujenzi huu ili wananchi waliokuwa wanaishi hapa waweze kurudi katika makazi yao,” amesema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ushauri wa TBA, Mhandisi Edwin Nnunduma amesema awamu ya kwanza ya ujenzi huo itahusisha majengo matano ya makazi. “Kati ya majengo haya matano, manne yatakuwa na ghorofa nane na moja litakuwa na ghorofa tisa, ambapo wakazi zaidi ya 600 waliokuwa wanaishi eneo hili tangu zamani watakabidhiwa,” amesema.
Mhandisi Nnunduma amesema majengo hayo yanajengwa kwa teknolojia ambayo imezingatia uwezo wa wakazi wake ambapo ina majiko yanayoweza kutumia kuni na mkaa.
Amesema mradi huo ambao unajengwa kwa awamu tofauti utahusisha ujenzi wa nyumba za makazi, maduka makubwa na ya kisasa pamoja na ofisi.
Mhandisi huyo amesema awamu ya kwanza iliyoanza Oktoba Mosi, mwaka huu inahusisha ujenzi wa nyumba za makazi ya wananchi waliokuwa wanaishi katika eneo hilo ambayo inatarajiwa kukamilika Oktoba, mwakani.(P.T)

Tuesday, 15 November 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MSTAAFU WA AFRIKA KUSINI THABO MBEKI IKULU




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.


. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mwenyeji wake Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mwenyeji wake Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
tabo10

PPF MWANZA YAVUNA WASANII 202 WA MIKOA YA KANDA YA ZIWA.

Meneja wa PPF Kanda ya ziwa, Meshack Bandawe akizungumza na baadhi ya wasanii  wa mikoa ya kanda ya ziwa mara baada ya kuwakabidhi kadi za uanachama mara baada ya kujiunga na mfuko huo mwishoni mwa wiki.

WASANI  202 wa mikoa ya kanda ya ziwa wajiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF kupitia mfumo wa uchangiaji wa hiyari wa Wote Scheme jijini Mwanza wakati wa warsha fupi ya kuwajengea uwezo wa sanii  iliyofanyika katika ofisi ya mkuu wa Mkoa  jijini Mwanza.

Akizungumza wakati wa kuwakabidhi kadi za uanachama wasanii hao Meneja wa PPF Kanda ya ziwa, Meshack Bandawe amesema wasanii mbali mbali wamejiunga katika mfumo ‘Wote Scheme’moja kwa moja   katika  Mfuko huo ambapo watapata mafao yanayotolewa na PPF 
moja kwa moja katika mfumo wa Wote Scheme ambapo mtaweza kupata huduma ya matibabu baada ya kuchangia miezi 3, 
 faida ni kupata mikopo ya biashara,  pamoja na mafao ya uzeeni.

Amewaasa wananchi wote wa mikoa ya kanda ya ziwa ambao hawapo katika sekta rasmi kama madereva wa Tax, wajasiliamali, wakulima, wavuvi, wafanyabiashara na madereva wa bodaboda wajiunge na mfuko wa PPF ili waweze kunufaika na mafao mbali mbali.

Wasanii hao ni kutoka Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Tabora na  Geita, pamoja na kupata elimu kutoka PPF vilevile washiriki walipata fursa ya kujengewa  uwezo wa kuhariri kutengeneza Miswada ya filamu pamoja na umuhimu wa kujiunga na mifuko ya uchangiaji wa hiari kwa ajili ya manufaa yao wenyewe pamoja na familia zao.  

Kwa upande wa wasanii wamefurahia sana mfumo wa Wote scheme kwani umekuja wakati sahihi ambapo Mfumo huu wa PPF utawasadia kwa kuwezesha kupata mikopo ya maendeleo na Bima ya afya, hivyo kuwafanya kuendelea na maisha yao.
Meneja wa PPF Kanda ya ziwa, Meshack Bandawe akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa Mfuko wa PPF, Msanii wa Filamu jijini Mwanza, Mwanaharusi Hela ambapo zaidi ya wasanii 202 walipojiunga na  na mfuko wa PPF mwishoni mwa wiki katika warsha ya kuwajengea uwezo wasanii wa mikoa ya kanda ya ziwa jijini Mwanza leo.
 Meneja wa PPF Kanda ya ziwa, Meshack Bandawe pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa PPF akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasaniiwaliojiunga na  PPF kupitia mfumo wa Wote Scheme.
 Msanii wa filamu  Mwanaharusi Hela akizungumza jinsi alivyofurahishwa na  mfumo wa wote scheme kupitia PPF ambapo utamnufaisha kwa kupata huduma ya afya  na mkopo wa maendeleo.
 Msanii na mpiga picha wa filamu akichangia maada wakati wa warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wasanii wa Mikoa ya kanda ya ziwa iliyofanyika jijini Mwanza.
 Afisa uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF jijini Mwanza, Mohamed Nyengi mwenye tisheti nyeupe akitoa maelekezo jinsi ya kujaza fomu ya kujiunga na mfuko wa uchangiaji wa hiari wa PPF (Wote Scheme) ambapo PPF iliweza kutoa semina kwa washiriki umuhimu wa kuchangia na Mfuko wa Pensheni wa PPF.

 Afisa uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF jijini Mwanza, Mohamed Nyengi  kulia akitoa maelekezo kwa wasanii wa mikoa ya kanda ya ziwa jijini Mwanza. 
 Msanii akijaza fumu ya kujiunga na uanachama wa mfuko wa PPF jijini Mwanza mara baada ya kuhudhuria warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wasanii hao jijini Mwanza.

UGENI WA NORDIC WATUA WIZARA MAMBO YA KATIBA NA SHERIA KUANGALIA UTEKELEZAJI WA MIRADI MBALIMBALI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akitoa neno la ukaribisho kwa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulipotembelea wizara wake jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Serikali ya Tanzania imeshukuru msaada mkubwa unaotolewa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na mfumo imara wa utoaji haki kwa kuzingatia demokrasia na uwajibikaji.

Serikali imesema kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika mfumo ya utoaji haki nchini kutokana na misaada iliyotolewa na nchi hizo kupitia Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambao unasaidia mpango huo wa UNDAP.

Hayo yameelezwa wakati ujumbe mzito wa kutoka nchi za Nordic ulipotembelea Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria. Nchi hizo za Nordic pamoja kutoa mchango wake mkubwa katika bajeti za serikali ya Tanzania pia hutoa mchango mkubwa kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya shughuli zake nchini.

Mataifa hayo ni ya Sweden, Norway, Denmark, Finland na Iceland ambayo kwa pamoja yanaitwa mataifa ya Nordic ni wadau muhimu wa Umoja wa Mataifa na pia kwa serikali ya Tanzania.

Ujumbe kutoka nchi hizo upo nchini kwa ajili ya kuimarisha mahusiano kati yao na Mashrika ya Umoja wa Mataifa yanayofanyakazi kama taasisi moja na nchi hizo (Delivering as one) kwa lengo la kuimarisha na kusukuma mbele malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).

Katika ziara hiyo iliyoanzia Novemba 14 wajumbe hao waliweza kuangalia utekelezaji mbalimbali wa miradi ya Umoja wa Mataifa na hasa hatua za mwanzo za miradi ya UNDAP ll.

Ujumbe huo wenye watu 13 kutoka Wizara za Mambo ya Nje za mataifa hayo wanatarajia kuzuru pia Kigoma na Dodoma wakimaliza Dar es Salaam.

Wakiwa Dar es Salaam, jana na leo watakutana na wawakilishi wa taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali na AZAKI na pia wanatarajia kutembelea ofisi za Bunge.Taarifa iliyotolewa katika mkutano huo imesema ingawa msaada wa Umoja wa Mataifa umekuwa siku zote ukililenga eneo maalumu linaloshughulikiwa na mashirika tofauti ya Umoja wa Mataifa, imekuwa nguvu kupima athari zake katika maeneo mbalimbali yaliyokusudiwa.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Awa Dabo akielezea dhumuni la ziara ya ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka Umoja wa Mataifa ulipotembelea wizara hiyo jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam. 

Hata hivyo imeelezwa kuwa kupitia programu mbalimbali na miradi katika demokrasia na uwajibikaji kuwezesha utawala bora, kumefanya kuwepo na nafuu fulani.

Serikali ya Tanzania ilielezea matumaini yake kwamba UNDAP ll, Mashirika ya Umoja wa Mataifa yakifanya kazi kama taasisi moja yatasaidia wizara katika kufanikisha kwa namna sahihi mfumo wa haki kwa wananchi.

Programu hizo ni pamoja na UNDAP 1 iliyosaidia wizara kutengeneza na kutekeleza mpango wa haki za binadamu (MHRAP 2013-2017). Mpango huo ulibainisha maeneo mbalimbali yaliyotakiwa kufanyiwa kazi na wadau mbalimbali.

UNDAP I ilisaidia wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali kujenga uwezo kwa wafanyakazi wake katika masuala ya majadiliano katika mikataba na namna ya kuiandika hasa katika sekta ya uziduaji.
Mkurugenzi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina (aliyesimama) akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka Umoja wa Mataifa ulipotembelea wizara hiyo jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam. 

Wanasheria kadha wa serikali na majaji walinufaika na elimu hiyo.

Aidha chini ya UNDAP I, Umoja wa Mataifa ulitoa msaada wa kiufundi kwa wizara kwa lengo la kuwezesha kufanya utafiti kuhusu hali ya mfumo wa haki wa mtoto nchini Tanzania na kuweza mkakati endelevu wa haki za mtoto kuanzia wmaka 2013-2017.

Wizara pia inasaidiwa kufuatilia mkakati huo kupitia majukwaa ya haki za watoto yanayofanyika kila mwaka.

Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria kwa mujibu wa sera ndiyo iliyokabidhiwa majukumu ya kutengeneza kanuni na viwango, kuratibu na kufuatilia utii usio na shuruti katika mfumo wa sheria na hivyo kupata matokeo yaliyokusudiwa ya sheria husika.

Wizara hii inajishughulisha na masuala ya Katiba, utawala na utoaji wa haki; uandishi wa sheria; uendeshaji wa mashtaka; Mikataba na sheria za kimataifa: msaada wa kisheria na haki za binadamu;usajili uboreshaji wa sheria, kabidhi wasihi, udhamini na mufilisi na kadhalika
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Mdemu akizungumzia ufadhili wa Umoja wa Mataifa kwa ofisi yake wakati wa mkutano na ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka Umoja wa Mataifa uliofanyika katika Wizara ya Mambo ya Sheria na Katiba jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam. 

Mamlaka ya Wizara katika mambo mengi ni mtambuka na hivyo kuifanya kuwa na ugumu fulani katika utendaji wake.

Aidha akifafanua zaidi amesema kutokana na misaada ya mashirika ya Umoja wa Mataifa, Watanzania wameweza kuwa na mfumo bora zaidi wa haki kwa watoto wanaoingia matatani na sheria.

Aidha watoto zaidi ya 1,500 wamepatiwa msaada wa kisheria katika mji wa Mbeya na Dar es Salaam na yote hayo yamewezeshwa na UNDAP l.

Wizara pia iliangalia matatizo ya ukatili wa kijinsia na watoto katika Dar es Salaam, Dodoma na Kilimanjaro na matokeo yake kusambazwa kwa wadau mbalimbali kwa kuyafanyia kazi.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar Bw. Kubingwa Mashaka Simba akitoa taarifa ya utekelezwaji wa miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa ujumbe wa wataalam wa Umoja huo waliotembelea Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Tanzania Bara jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam. 

Aidha kwa kusaidiwa na Umoja wa Mataifa ambayo iliratibu mkutano wa kwanza wa wadau kuzungumzia sheria ya ndoa ya mwaka 1971 katika hali ya kuongeza haki zaidi ka wanawake na watoto.

Pia alisema katika UNDAPll mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yanasaidia pia kuangalia mfumo wa haki wa sasa hasa kwa makundi yenye uhitaji yaliyosahaulika na kukuza ulinzi na usalama kwa mama na mtoto.

Ujumbe huo pamoja na kuwa mzito pia utafanya safari ya kuangalia miradi ya Bunge iliyopewa chapuo na fedha za Umoja wa Mataifa pia watatembelea eneo la dawati la Jinsia Chang'ombe na kutembelea taasisi ya PASADA.

Maeneo mengine ni ghala la Chakula Kizota, miradi ya TASAF na pia kiwanda cha kusindika mafuta kilichopo Dodoma.
Kiongozi wa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Anders Ronquist kutoka Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweden (SIDA) akizungumza jambo kwa niaba ya ujumbe huo ulipotembelea wizara hiyo jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kushoto) wakati wa ziara ya ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka Mashirika ya Umoja wa Mataifa ulipotembelea wizara hiyo.
Sehemu ya ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka Mashirika ya Umoja wa Mataifa ulipotembelea Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam. 

Balozi wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt akizungumza jambo wakati akiagana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (kushoto). Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju mara baada ya kumalizika kwa mkutano na ujumbe wa Nordic uliotembelea wizara hiyo jana.
Deepika Nath wa UN Women akimwonyesha kitu Edgar Kiliba (kushoto) wa Ofisi ya Mkuu wa Umoja wa Mataifa kitengo cha mawasiliano mara ya kumalizika kwa mkutano wa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka Mashirika ya Umoja wa Mataifa ulipotembelea Wizara ya Mabo ya Katiba na Sheria jana 14/11/2016 jijini Dar es Salaam.