Wednesday, 29 June 2016

UBUNGE WA OLE NANGOLE LONGIDO WATENGULIWA NA MAHAKAMA KUU ARUSHA

imagesKesi iliyokuwa ikiunguruma kuanzia  Februari 29 ,2016 katika Mahakam Kuu jijini Arusha imetolewa hukumu leo hii
Katika
shauri hilo aliyekuwa mgombea ubunge wa CCM jimbo la Longido Dkt
Kiruswa  alifikisha mahakamni shauri hilo la kupinga matokeo ya ushindi
dhidi ya mbunge wa Longido Mh.Onesmo Nangole.
Akisoma hukumu
hiyo,Jaji Mwagesi  alisema kuwa mlalamikaji ndugu Kiruswa aliwakilishwa
na Wakili msomi Dr.Masumbuko Lamwai na Wakili Haraka.Katika shauri
hilo,dai la msingi la mlalamikaji bwana Kiruswa lilikua ni:
1.Kutumika kwa lugha ya matusi na kashfa wakati wa kampeni kutoka kwa mh Onesmo Nangole.
2.Kuwepo kwa wapiga kura kutoka nchi jirani ya Kenya walioletwa na Mh Nangole
3.kutumika kwa magari ya Chadema kwenye kusindikiza na kubebea masanduku ya kupigia kura
4.Mkurugenzi wa Uchaguzi kutangaza matokeo baada ya mgombea wa CCM kutolewa nje.
5.Kutokea kwa vurugu ndani ya chumba cha kuhesabu matokeo
Kutokana
na madai hayo na kwa kuzingatia kanuni,sheria na ushahidi uliotolewa
pamoja na vielelezo na mashahidi wa pande zote mbili,Jaji kutoka
mahakama kuu Bukoba Mh.Jaji Mwagesi alisema;”Kutokana na kuzingatia
viini vyote vya shauri hili kama vilivyosikilizwa na kwa mujibu wa
sheria,Natamka kwamba;

Mahakama hii imetengua shauri hili na kwa
kujiridhisha kwamba mchakato mzima haukuwa wa haki na huru hivyo
mahakama inaamuru uchaguzi urudiwe upya.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA WAKUU WA MIKOA WATATU IKULU JIJINI DAR ES SALAAM NA KUKUTANA NA MWENYEKITI WA GATES FOUNDATION MELINDA GATES


MAF5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Ikulu jijini Dar es Salaam.
MAF6Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Charles Mlingwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mara Ikulu jijini Dar es Salaam.
MAF7Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Zainab Telack kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ikulu jijini Dar es Salaam.
MAF8Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya  Wakuu wapya wa Wilaya mara baada ya kuwaapisha wakuu wapya watatu wa Mkoa Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan watatu kutoka kushoto, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa watatu kutoka kulia na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakwanza kushoto.
MAF9Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa mikoa pamoja na Wakuu wa Wilaya wateule mara baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wa mikoa ya Shinyanga, Mara na Ruvuma Ikulu jijini Dar es Salaam.
MAF10Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa mikoa pamoja na Wakuu wa Wilaya wateule mara baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wa mikoa ya Shinyanga, Mara na Ruvuma Ikulu jijini Dar es Salaam.
MAF11Baadhi ya Wakuu wa Wilaya wateule  wakila kiapo cha uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam. 
MAF1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Mwenyekiti waGates Foundation Bi. Melinda Gates Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya mazungumzo.
MAF2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Gates Foundation Bi. Melinda Gates watatu kutoka kushoto mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
MAF4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti waGates Foundation Bi. Melinda Gates mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU

UFAFANUZI KUTOKA NBS


IND

MKUFUNZI WA MASWALA YA BIASHARA NA MASOKO REHEMA KASULE AWAPA ELIMU MANJANO DREAM MAKERS




Mkufunzi wa maswala ya biashara Mama Rehema Kasule kutoka nchini Uganda akiwapa elimu wanafunzi wa Manjano Foundation jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili kwenye majukumu yao ya kila siku ikiwemo kutengeneza uhusiano na watu waliofanikiwa kwa kuwa itasaidia kujifunza mengi.Pia namna ya kujiamini kuwaza mafanikio zaidi kuwa lazima wafanikiwe na kuachana kabisa na mawazo ya kushindwa akiwa sambamba na Afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions, Mama Shekha Nasser. 
Akieleza zaidi Mama Kasule amewataka Washiriki wa Manjano Dream Makers kama wanataka kufanikiwa kazi zao za upambaji na biashara zao ni lazima wafanye kwa moyo mmoja kutoka ndani ya nafsi pia kuachana na fikra za kukata tamaa na maneno ya watu ya kuwakatisha tamaa. Kwa upande afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions na Mkurugenzi wa Manjano Foundation mama Shekha Nasser amewataka washiriki hao kuongeza juhudi pia kuyatekeleza kwa vitendo yale yote waliofundishwa katika mafunzo hayo.

Mama Rehmah Kasule alikuwa jijini Dar akihudhuria kwenye semina ya siku 4 ya #PSIPSE "Partnership to Strengthen Innovation and Practices in Secondary Education.
Baada ya semina yake, mama Kasule akajitolea siku moja kuja kutoa mafunzo kwa washiriki wa Manjano Dream Makers ikiwa ni mojawapo ya mkakati wa washiriki walio wengi wa Vital Voices (na yeye akiwa mmojawapo) kwamba kila mwanamke ajitolee kuwasaidia au kuwafundisha wanawake vijana kitu anachokijua, yaani "Pay it Forward."

TANAPA YASAIDIA UJENZI WA MIUNDOMBINU KATIKA MAENEO YANAYOPAKANA NA HIFADHI YA TAIFA MILIMA YA MAHALE ILIYOPO MKOANI KIGOMA.





Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima ya Mahale,Mhifadhi Romanus Mkonda akizungumza juu ya ujenzi wa madaraja ulioanza katika barabara ya kuelekea katika hifadhi hiyo.
Wanahabari wakimsilikiliza Mhandisi kutoka kampuni ya ujenzi ya Lilangela inayojenga daraja la Lagosa katika barabara ya Buhingu wilayani Uvinza ,Marango Ngose alipokuwa akizungumzia juu ya ujenzi huo unaofadhiliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)



Kukamilika kwa ujenzi wa daraja hili kuta tatua changamoto ya wananchi katka vijiji hivyo kuvuka kwenda upande mwingine ambako kwa sasa wamekuwa wakilazimika kuvuka katikati ya mto huku wakiwa wamebeba vyombo vyao vya usafiri na hata mifugo imekua ikipita katika mto huo.
.
Kibao kinachoonesha taarifa mbalimbali juu ya ujenzi wa daraja hilo.




Baadhi ya mafundi wakijaribu kuchimba udongo katika eneo la mto Lagosa ambako daraja hilo linajengwa.
Baadhi ya malighafi zinazotumika kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo zikiwa eneo la ujenzi.


Ari kadharika kina mama na watoto kwa sasa wamekua wakilazimika kwenda kupata huduma ya maji upande wa pili wa mto huo na kwamba wanalazimika pia kupita ndani ya mto huo ili kuvuka kwenda katika makazi yao.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akiwa ameongozana na wanahabari wakitoka katika eneo kunako jengwa daraja hilo.



Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog aliyeko Kigoma.

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetoa Sh. Milioni 584 kwa ajili ya ujenzi wa madaraja mawili ikiwa ni njia.moja ya kutatua changamoto ya miundombinu ya barabara katika vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa Milima ya Mahale vilivyopo wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

Baadhi ya wananchi wanaoishi katika vijiji vya Lukoma na Igalula wanakabiliwa na changamoto ya barabara jambo linalowafanya washindwe kufanya shughuli zao za kimaendeleo.Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea vijiji hivyo vilivyoko mwambao mwa zimwa Tanganyika ,Mkuu wa idara ya ujirani mwema ,Mhifadhi Romanus Mkonda aliyataja madaraja hayo kuwa Lagosa na Lukoma.“Daraja la Lagosa linatumia Sh. Milioni 296 wakati lile la Lukoma litatumia Sh. Milioni 288,” alisema.

Alisema lengo la TANAPA ni kusaidia jitihada za serikali za kuimarisha mawasiliano ya barabara katika ukanda huo kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.“Iwapo barabara hiyo itapitika itarahisisha usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa ukanda huu na pia Hifadhi yetu itaweza kupata watalii wengi kwa sababu usafiri uliopo sasa hivi ni wa maji na Ndege pekee,” alisema.

Hata hivyo, alisema iwapo miundombinu hiyo ya barabara itakamilika itaepusha gharama kubwa ambazo Hifadhi inaingia kwa ajili ya kwenda mjini kununua vitu mbalimbali vya hifadhini.Aliongeza kuwa barabara hiyo itawasaidia wananchi hao kupata huduma mbalimbali zinazopatikana nje ya eneo lao ikiwa ni pamoja na kusafirisha mazao na kuyapeleka masoko ya nje.

“Kwa mfano tunapotaka kwenda mjini tunatumia Boti ambalo linatumia Lita 1000 za petroli kwenda na kurudi na oil lita 40...hivyo iwapo barabara zitakamilika gharama hizi zitapungua,” alisema.Pia, alisema barabara hizo zikikamilika utalii utaongezeka na kuliongezea taifa pato.Aliongeza kuwa kwa mwaka wa fedha 2016/17, TANAPA imetenga Sh. Milioni 500 kwa ajili ya kujenga madaraja ya Nkonkwa na Igalula yaliyopo vijijini hapo.

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Igalula, Mussa Matililo alisema iwapo madaraja hao yatakamilika itawarahisishia wananchi wa maeneo hayo katika shughuli zao za kilimo.“Pia, itarahisisha mawasiliano ya kijiji kimoja kwenda kijiji kingine kwa sababu kwa sasa mawasiliano yamekuwa magumu kutokana nah ii mito miwili,” alisema.

PBZ YAADHIMISHA SHEREHE ZA MIAKA 50 KWA KUSAIDIA JAMII NA KUTEMBELEA HOSPITALI YA KIDONGOCHEKUNDU.




Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ akizungumza na Maofisa wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar wakati wa kikabidhi msaada wa magodoro kwa ajili ya Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Mafunzo Kilimani Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akimkabidhi msaada wa magodoro 100 Kamishna Msaidizi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Omar Salum Mgaza. hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Mafunzo Kilimani Zanzibar.
Kamishna Msaidizi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Omar Salum Mgaza akitowa shukrani kwa PBZ  kwa msaada wao huo wa magodoro umeletwa wakati muafaka na kuwata taasisin nyengine kujitokeza kutoa misaada.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg.Juma Ameir akisalimiana na Muuguzi Dhamana wa Hospitali ya Kidongochekundu Zanzibar Ndg. Haji Vuai Hilal, wakati walipofika katika hospitali hiyo ya Mental kutowa misaada ya mashuka 200 kwa ajili ya hospitali hiyo. katikatika Afisa Masoko wa PBZ Ndg. Mohammed Nuhu. 
Afisa Masoko wa PBZ Ndg Mohammed Nuhu akisalimiana na Muuguzi Dhamana wa Hospitali ya Mental Kidongochekundu Zanzibar Haji Vuai Hilal. 
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Juma Ameir akizungumza na Uongozi wa Hospital ya Mental Kidongochekundu Zanzibar wakati wa kutembelea hospitali hiyo na kutoa msaada wa mashuka 200 ikiwa ni kusherehekea miaka 50 ya PBZ Zanzibar hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya hospitali hiyo.

MUONEKANO MPYA WA ZARI THE BOSS LADY