Tuesday, 2 August 2016

MADIWANI MJI WA KIBAHA WAWAASA WATENDAJI/WATAALAMU WA HALMASHAURI KUSIMAMIA ILANI

index1Mbunge wa jimbo la  Chalinze Ridhiwani  Kikwete, akizungumza na vijana wa Chalinze Saccos iliyoanzishwa jimboni hapo ambapo Ridhiwani  ni mlezi wa saccos hiyo(Picha na Mwamvua Mwinyi)
indexMadiwani mbalimbali wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, wakiwa katika kikao cha baraza la  madiwani ambacho kilijadili na kupitisha agenda ikiwemo taarifa ya maendeleo ya kata,kupokea taarifa ya mapato na matumizi ambapo waligomea kupitisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka jana  baada ya kubaini mapungufu makubwa.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
……………………………………………………………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
MADIWANI wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,wamewataka wataalamu na watendaji wa halmashauri hiyo kuwa makini katika kuandaa taarifa mbalimbali ikiwemo ya utekelezaji wa ilani ili kuondokana na usumbufu wa kufanya maboresho yasiyo ya lazima.
Wamesema taarifa ya utekelezaji wa ilani ya mwaka jana ambayo ilikuwa ikijadiliwa katika kikao cha madiwani kilichofanyika ,kujadili mambo ya maendeleo,ilani na mapato na matumizi ,ina mapungufu makubwa.
Aidha madiwani hao wamewaagiza wataalamu na watendaji hao kufanya maboresho na kuirekebisha taarifa hiyo ili mwezi ujao iweze kujadiliwa na kupitishwa rasmi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti madiwani hao walisema,agenda ya kupitia taarifa hiyo muhimu ya uchaguzi ya mwaka 2015 wameiahirisha kwa ajili ya maboresho kabla ya kwenda chama.
Walielezea kuwa ni ngumu kuikwepa ilani ya chama tawala kwa kukubali kufanyakazi za serikali pasipo kuifanyia kazi ilani hiyo ambayo utekelezaji wake unakwenda sambamba na serikali iliyo madarakani.
 Diwani wa kata ya Visiga ,Mbegu Legeza,alisema watendaji ,wataalamu wa serikali sambamba na halmashauri wanapaswa kusimamia kikamilifu  utekelezaji wa ilani .
“Tuliyoyaona kwenye taarifa ya ilani hii mengi yamechotwachotwa na kubambikwa huku miradi mingine ikiwa haijawekwa kwenye taarifa hiyo”
“Mambo mengi hayapo sawa ukisema mmekopesha vikundi lazima iainishwe kata ngapi wamepewa hizo fedha,makundi gani yamepokea fedha,kuna viwanda vimejengwa na kuwekezwa vingine vimeandikwa vingine havijaandikwa”
“Kuna vikundi vimefundishwa lakini diwani wa kata husika hajui na kwenye kabrasha imeandikwa kuna elimu imetolewa kwenye kata hiyo hapo ni lazima diwani husika akatae”alisema legeza.
Diwani wa kata ya Mailmoja ,Ramadhani Lutambi alieleza kuwa ,hali hiyo inaonyesha udhaifu mkubwa kwa wataalamu hao kwa kushindwa kufanya kazi zao kwa uhakika.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Leonard Mloe,alikiri kuwepo kwa mapungufu kwenye taarifa hiyo ambapo alisema agenda nyingine zilijadiliwa na kupitishwa bila tatizo.
Agenda zilizojadiliwa ilikuwa ni pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo robo ya nne april-juni  2016 ,taarifa ya maendeleo ya kata na kupokea taarifa ya mapato na matumizi.
Nae mwenyekiti wa CCM mji wa Kibaha ,Maulid Bundala, alitoa wito kwa baraza hilo kubadili utaratibu wa kupitia taarifa ya ilani kwenye baraza hilo kwa kutenganisha na kuichambua ilani hiyo kwenye vikao vingine ambavyo haviudhuliwi na viongozi wa vyama.
Alisema raha ya chakula usikione kikipikwa wala kuandaliwa hivyo ni vyema ukafanyika utaratibu mwingine wa kujadiliwa taarifa hiyo kwenye kikao cha madiwani pekee kabla ya baraza.
Hata hivyo Bundala alisema baada ya kujadiliwa taarifa hiyo ni lazima itafika katika chama hivyo hakuna sababu ya kujadiliwa wakati wao wakiwepo.
Alisema watendaji,watalaamu wa serikali na halmashauri hawawezi kukwepa ilani ya chama cha mapinduzi ,na kusema anaeona kichefuchefu kutekeleza ilani hiyo atoke nje wakati wa kuijadili.
“Itakuaje maziwa ya ng’ombe yawe mazuri halafu ng’ombe wake awe mbaya,serikali hii inaongozwa na CCM,sasa utakwepaje kuisimamia ilani ya chama tawala,jamani huu ni wakati wetu na ukifika wa chama kingine itasimamiwa ilani yao”alisema Bundala.
Bundala alieleza kuwa hata kama ni mkurugenzi ameajiliwa na serikali ambayo imenatekeleza ilani ya CCM hivyo kuna kila sababu ya watendaji wote kufanyakazi kwa moyo na kusimamia majukumu yao.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Lucy Kimoi alisema wamepokea ushauri na maagizo yote na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi.
Katika hatua nyingine halmashauri hiyo imekisia kukusanya kwa mwaka 2015/2016 bil 3.744 katika mapato yake ya ndani .
Robo ya nne inayoishia juni mwaka huu,imekusanya mil.732.102 na kufanya jumla ya mapato yaliyokusanywa julai /juni 2016 kuwa zaidi ya bil.2.910.866 sawa na asilimia 78 ya makisio.

Pia imekisia kutumia zaidi ya bil.31.836.942 kwa lengo la kutoa huduma kwa wananchi wa mji huo .
Katika utekelezaji wa shughuli zake kwa robo ya nne iliyoishia juni 2016 imetumia bil.5.950.420 na kufanya jumla ya matumizi kwa julai/juni  mwaka huu kufikia bil.21.614.164 sawa na asilimia 67 ya makisio.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII PROFESA MAGHEMBE AWAASA BODI YA UTALII KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII.

 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akizungumza na wajumbe wa bodi ya utalii Tanzania(TTB) jijini Dar es Salaam leo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa bodi ya utalii. Amesema kuwa  bodi ya utalii wanawajibu wa kutangaza vivutio vilivyopo hapa nchini ili kila mtu na aweze kutembelea vivutio hivyo kwaajili ya kuongeza pato la Nchi.

Pia amesema kuwa Bodi ya Utalii inapaswa kulipa deni la bodi hiyo kwani linaleta doa katika bodi ya utalii hiyo.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Angeline Madete (Kulia ) na Mkurugenzi wa Wizara ya Maliasili na utalii, Zahoro Kimwaga wakiwa kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Bodi ya Utalii Tanzania jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Utalii wakimsikiliza  Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe jijini Dar es Saalaam.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe(Katikati) Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii(TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo kushoto na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Angeline Madete wakiwa katika picha ya Pamoja na wajumbe wa bodi ya Utalii (TTB)jijini Dar es Salaam leo.

TTCL KUIUNGANISHA TANROADS NCHI NZIMA.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dkt Kamugisha Kazaura akitoa neno la shukhurani baada ya TTCL kupata zabuni ya kuuganisha ofisi za TANROADS nchi nzima kwenye mkongo wa TTCL.
 Menejimenti ya TTCL na TANROADS wakiwa katika hafla ya kusaini mkataba wa TTCL kutoa huduma ya intaneti na  kuuganisha ofisi za TANROADS nchi nzima kupitia Mkongo wa TTCL.  
 Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dkt. Kamugisha Kazaura (Kulia),  Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfungale (Katikati) na  Mwanasheria wa TANROADS Dora Komba (Kushoto) wakisaini mkataba wa makubaliano ya TTCL kutoa huduma ya kuunganisha ofisi za TANROADS nchi nzima.

WAKALA wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Kampuni ya Simu Tanzania TTCL zimetiliana saini Mkataba wa huduma za Intaneti ambapo TTCL itaunganisha ofisi za Wakala hiyo nchi nzima kwa kutumia Mkongo wake wa Mawasiliano. 

Hafla ya kutiliana saini makubaliano hayo imefanyika leo katika ofisi za Makao Makuu ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na  kuhudhuriwa na Mtendaji Mkuu (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale, Afisa Mtendaji Mkuu (TTCL), Dkt Kamugisha Kazaura pamoja na maafisa Waandamizi kutoka TTCL na TANROADS. 

Mradi huo utakaotekelezwa katika Mikoa 25 na Vituo (3) vya mizani utatumia miundombinu ya mawasiliano ya Kampuni ya TTCL iliyounganishwa katika Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB). Mikoa hiyo ni pamoja Makao Makuu ya TANROADS, Mikoa ya Singida, Tabora, Kigoma, Tanga, Mtwara, Kibaha, Iringa, Musoma na Bukoba. 

Mikoa mingine ni Dar es salaam(Keko na Mabibo), Lindi, Makambako, Mwanza, Songea, Manyara, Shinyanga, Dodoma, Mbeya, Sumbawanga, Simiyu(Bariadi), Arusha, Mpanda, Moshi, Geita na Morogoro

Kampuni ya Simu Tanzania TTCL inatekeleza Mpango Mkubwa wa Mageuzi ya Kibiashara ambao umelenga kuboresha miundombinu ya Mtandao na biashara ili kukidhi mahitaji ya wateja na Nchi katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasilaino. Hadi sasa, Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imeunganisha makampuni binafsi, Mashirika ya Umma na ofisi za serikali zaidi ya 80 kwenye miundombinu ya mawasiliano ya TTCL yenye ufanisi mkubwa wa kimawasiliano ndani na nje ya nchi.

DC ILALA,SOPHIA MJEMA AZINDUA UWANJA WA NETIBOLI NA KIKAPU SHULE YA JANGWANI JIJINI DAR LEO



Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akifunga goli wakati wa uzinduzi wa uwanja wa Netiboli na Mpira wa Kikapu wa Shule ya Sekondari ya Jangwani uliojengwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake ya "Be Kidotified".  Mjema alizindua uwanja huo leo katika hafla fupi iliyofanyika katika shule hiy.Kushoto ni Jokate akishuhudia tukio hilo.PICHA NA MICHUZI JR
  Mkuu wa  Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kushoto) akitoa hotuba yake katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo (kushoto). Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wa Mwisho ni Mkuu wa Shule Msaidizi wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo (Kushoto) akizungumza katika halfa ya uzinduzi wa uwanja alioujenga kupitia kampeni yake ya "Be Kidotified" uliomgharimu kiasi cha Sh Milioni 50. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji Foundation, Barbara Gonzalez akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL, Fatema Dewji na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na wa Mwisho ni Mkuu wa Shule Msaidizi wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa. 
Mrembo wa zamani wa Tanzania, Faraja Kota akizungumza mbele ya Wanafunzi katika hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa kikapu na netiboli uliojengwa na mrembo, Jokate Mwegelo. 
 Mandhari ya uwanja wa Mpira wa Kikapu na Netiboli wa shule ya Sekondari ya Jangwani uliojengwa na Mrembo, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake ya "Be Kidotified".
Mkuu wa Wilaya ya Ilala pichani kati Mh.Sophia Mjema akiwasili kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa uwanja wa mpira wa Netiboli na Kikapu wa shule ya Jangwani leo jijini Dar,Pichani kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Ilala.Ndugu Edward Mpogolo na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti, Jokate Mwegelo.

 Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema alisema kuwa amefurahishwa na mpango huo wa Jokate kwa kusaidiana na Mo Dewji Foundation na kuwaomba kuuendeleza kwa shule nyingineza jijini.

Mjema alisema kuwa Dar es Salaam kuna shule nyingi na angependa kuona hata shule za Chanika zinafaidika na kampeni ya "Be Kidotified". Alisema kuwa amefarijika sana kuona shule aliyosoma yeye kufaidika kwa mradi huo na kuwaomba wanafunzi na walimu kuutumia uwanja huo kama fursa ya kuendeleza michezo na taaluma.

Wakati huo huo Mrembo mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake ya kuchangia jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified” amejenga uwanja utakaotumika kwa ajili ya michezo ya mpira wa kikapu na Pete (netiboli) kwa Shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani.

Uwanja huo ulizinduliwa jijini leo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye shule hiyo na kuhudhuriwa na wanafunzi, walimu na viongozi mbalimbali wa serikali. Ujenzi wa uwanja huo umemgharimu Jokate kiasi cha Shilingi milioni 50.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Jokate alisema kuwa ameamua kuonyesha mfano kupitia ‘Kidoti Brand’ kuchangia maendeleo ya michezo nchini hasa kwa katika shule ambazo ni kiini cha maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini. Mbali ya michezo, pia Kidoti Brand inajihusisha zaidi na maendeleo ya elimu hapa nchini.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ya Tanzania imeadhimia kuondoa changamoto nyingi katika elimu na yeye kuamua kuanzia katika masuala ya michezo ambayo uchangia ufaulu darasani na kuibua vipaji ambavyo vitamwezesha mshiriki kupata ajira.

Alisema kuwa moja ya changamoto kubwa zinazorudisha nyuma maendeleo ya michezo nchini ni ukosefu wa viwanja bora ambavyo ukwamisha wachezaji chipukizi kuonyesha vipaji vyao ipasavyo.

Kwa mujibu waJokate, alipokuwa anasoma, alikutana na changamoto hizo, lakini alipiga moyo konde na kujihusisha na shughuli mbalimbali za nje ya darasa ikiwa pamoja na michezo na kujifunza mengi.

“Mimi ni mjasiriamali mchanga sana hapa nchini, nimehamasisha kwa kile kidogo nilichonacho na kwa msaada wa wadhamini niliyotafuta kuhitimisha ujenzi wa uwanja huu ambao utatumika si kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Jangwani pekee, bali hata kwa mechi za shule nyingine, ”

“Nawapongeza wadhamini walioniunga mkono katika mpango huu kama Mo Dewji Foundation, na wadau ambao walikuwa nyuma yangu katika kuhakikisha kampeni ya ‘Be Kidotified’ inaanza kwa mafanikio makubwa na kuendelea kwa shule nyingine za hapa jijini,” alisema Jokate.

Alisema kuwa chapa ya Kidoti ni miongoni mwa chama zinazoongoza hapa nchini katika mitindo, urembo na burudani kabla ya kuamua kupanua wigo kwa upande wa michezo tofauti na mpira wa miguu.

Alifafanua kuwa alianza kwa kuanzisha kampuni ya Kidoti (Kidoti Company) na kuchangia katika soko la ajira nchini na baadaye kuanzisha “kidoti brand’ akiwa na lengo la kuhamasisha vijana kujihusisha katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali ili kuweza kukabiliana na maisha ya kila siku.
 

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA KATIKA KIWANDA CHA MTIBWA SUGAR.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha sukari cha Mtibwa   kukagua uzalishaji  wa sukari katika kiwanda hicho, Agosti 2, 2016.   Kulia ni  mkewe Mary, wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe na Wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha sukari cha Kagera na Mtibwa, Seif Ali Seif .  Kushoto ni Kaimu Katibu wa CCM mkoa Wa Morogoro, Kulwa Solobi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Meneja wa Kiwanda cha sukari cha Kagera,  Ashuwin  Rana baada ya kuwasili kwenye  kiwanda  cha sukari cha Mtibwa  baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha sukari cha Mtibwa Agosti 2, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Stephene Kebwe na wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Kagera Sugar na Mtibwa Sugar, Seif  Ali Seif .
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo la mtambo wa maji ya kumwagilia katika shamba la miwa la kiwanda cha sukari cha Mtibwa  wakati alipokitembelea kiwanda hicho, Agosti 2, 2016.  Kushoto ni  mkewe Mary na wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera na Mtibwa, Seif  Ali Seif .
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo la mtambo wa maji ya kumwagilia katika shamba la miwa la kiwanda cha sukari cha Mtibwa  wakati alipokitembelea kiwanda hicho, Agosti 2, 2016.  Kushoto ni  mkewe Mary na wapili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera na Mtibwa, Seif  Ali Seif.
 Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa na Mkewe Mary wakisalimiana  na wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa  wakati alipotembelea kiwanda hicho Agosti 2, 2016.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Stephene Kebwe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa wakati alipokitembelea kiwanda hicho Agosti 2, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).

Monday, 1 August 2016

ESRF YAWAKUTANISHA WADAU MBALIMBALI KUICHAMBUA BAJETI YA SERIKALI KATIKA SEKTA YA AFYA NA VIWANDA

TAASISI ya Utafiti ya Uchumi na Jamii (ESRF) imewakutanisha wasomi na wawakilishi wa taasisi za umma na kibinafsi kuchambua bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 katika Sekta ya Afya na Viwanda ili kuona inavyoweza kutatua changamoto zinazokabili Sekta hizo kwenye mdahalo uliokutanisha wasomi, wawakilishi wa Taasisi za Umma na Binafsi na kufanyika makao makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Akifungua mdahalo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt.Tausi Kida alisema, Taasisi yake imeona ni vema kuwakutanisha wadau kujadili bajeti hiyo katika sekta ya Afya na Viwanda, kwa vile zinagusa uchumi wa wananchi.
Akiwasilisha mada juu ya bajeti ya Serikali 2016/2017na changamoto zinazoikabili sekta ya Afya, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi Shirikishi, Cha Muhimbili, (MUHAS), Profesa Phares Mujinja alisema, ingawa bajeti iliyotengwa kwenye sekta ya Afya ni kubwa, lakini bado kuna changamoto kadhaa kwa vile Wizara hiyo imepanuka kutokana na kuhudumia maeneo mengi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mdahalo uliolenga kujadili changamoto zinazoikabili bajeti ya mwaka 2016/2017 kwenye sekta ya Afya na Viwanda, kwenye makao makuu ya ESRF jijini Dar es Salaam. Mdahalo huo umewakutanisha wasomi, wawakilishi wa Taasisi za Umma na Binafsi. (Picha zote na K-VIS MEDIA/Khalfan Said).
 
Profesa Mujinja alitolea mfano wa ununuzi wa madawa ambapo, zaidi ya asilimia 90 ya madawa yanayotumika huagizwa kutoka nje na hivyo fedha nyingi za kigeni hutumika.
Katika majumuisho yake, Profesa Mujinja alisema, ni vema Serikali ielekeze nguvu zake kwenye uanzishwaji wa viwanda vya kuzalisha madawa na vifaa tiba hapa nchini ili kwenda sambamba na malengo ya taifa ya maendeleo endelevu.
Akizungumzia kuhusu changamoto za bajeti kwenye eneo la Viwanda, muwasilisha mada Profesa Prosper H. Ngowi kutoka Chuo Kikuu Cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam, alisema, fedha zilizotengwa kwenye Sekta ya Viwanda ni Shilingi Bilioni 81, 871,992,000, ambapo asilimia 51 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na asilimia 49 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Kwa mtazamo wake, Profesa Ngowi alisema, mgawanyo huo ni mzuri na sio kwa kiwango kikubwa kwani hakuna tofauti na bajeti ya mwaka 2015/2016, na kuonyesha wasiwasi wake muda ambao Serikali inatoa fedha hizo kuhudumia maeneo yaliyokusudiwa.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Cha Muhimbili, Profesa Phares Mujinja, akitoa mada juu ya changamoto zinazoikabili bajeti ya Serikali ya 2016/2017 kwenye Sekta ya Afya wakati wa mdahalo huo.
 
“Bajeti ya 2016/2017 ni Asilimia 70.3% ya ile ya 2015/2016 na kwamba wizara hivi sasa ni kubwa kutokana na kuongezeka kwa sekta ya Uwekezaji.” Alifafanua.
Wakichangia mada hizo, wengi wa washiriki wameonyesha wasiwasi wao kuhusu kufanikiwa kwa malengo ya serikali kwenye Sekta hizo kutokana na muonekano wa bajeti yenyewe na mahitaji halisi ya sasa ya utoaji huduma kwenye Sekta hizo ili kufikia malengo ya kukuza uchumi wa nchi kumekuwepo kwa mtazamo kuwa biashara nchini zinaanguka kutokana na mkazo wa kukusanya mapato.
Akifunga mdahalo huo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Utawala na Ujenzi wa Maendeleo wa ESRF, Doris Likwelile, aliwashukuru washiriki kwa michango yao mbalimbali na kwamba mawazo yao yatawezesha utayarishaji wa mtazamo wa wadau kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 kwenye Sekta hizo mbili za Afya na Viwanda.

MBUNGE WA JIMBO LA MAFINGA MJINI COSATO CHUMI ASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO NA NGO YA WORLD SHARE YA NCHINI KOREA


na Fredy Mgunda,Iringa.

Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi amesaini mkataba wa ushirikiano na NGO ya world share ya nchini korea ,NGO hiyo inajishughurisha na utoaji wa misaada ya ujimbaji wa visima,ujenzi wa tower pamoja na mfumo wa maji katika shule za msingi.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo mbunge huyo amesema kuwa watashirikiana katika kuwasidia watoto yatima,watu wenye ulbino,taa ndogo za solar kwa ajiri ya kaya masikini katika vijiji ambayo havijafikwa na umeme.

Makubaliano yamefanyika jana ikiwa ni siku moja tu baada taasisi hiyo kuahidi kushughulikia tatizo la maji katika shule ya msingi ya Makalala Mchanganyiko ya mjini Mafinga.Akitoa ahadi hiyo mbele ya Balozi wa Korea nchini, Song Geum Young aliyetembelea jimbo hilo kwa mwaliko wa mbunge wake, Cosato Chumi, afisa wa taasisi hiyo Nara Kim alisema:

“Tutatoa msaada huo kama tutahakikishiwa kuondolewa vikwazo vya askari wa usalama barabarani wakati tukisafirisha mtambo wa kuchimba visima toka Dar es Salaam. Alisema taasisi hiyo inayofanya kazi zake nyingi jijini Dar es Salaam inahofia kupata kadhia kutoka kwa askari hao kama inavyotokea mara kwa mara katika jiji hilo.


Afisa wa NGO ya world share ya nchini korea Nara Kim na mbunge wa jimbo mafinga mjini Cosato Chumi wakisaini mkataba wa makubaliano ya kazi
Afisa wa NGO ya world share ya nchini korea Nara Kim na mbunge wa jimbo mafinga mjini Cosato Chumi wakionyesha sehemu ya mkataba huo.
Balozi wa Korea nchini, Song Geum Young akionyesha  taa ndogo za solar kwa ajiri ya kaya masikini katika vijiji ambayo havijafikwa na umeme.