na Fredy Mgunda,Iringa.
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi amesaini mkataba wa ushirikiano na NGO ya world share ya nchini korea ,NGO hiyo inajishughurisha na utoaji wa misaada ya ujimbaji wa visima,ujenzi wa tower pamoja na mfumo wa maji katika shule za msingi.
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo mbunge huyo amesema kuwa watashirikiana katika kuwasidia watoto yatima,watu wenye ulbino,taa ndogo za solar kwa ajiri ya kaya masikini katika vijiji ambayo havijafikwa na umeme.
Makubaliano yamefanyika jana ikiwa ni siku moja tu baada taasisi hiyo kuahidi kushughulikia tatizo la maji katika shule ya msingi ya Makalala Mchanganyiko ya mjini Mafinga.Akitoa ahadi hiyo mbele ya Balozi wa Korea nchini, Song Geum Young aliyetembelea jimbo hilo kwa mwaliko wa mbunge wake, Cosato Chumi, afisa wa taasisi hiyo Nara Kim alisema:
“Tutatoa msaada huo kama tutahakikishiwa kuondolewa vikwazo vya askari wa usalama barabarani wakati tukisafirisha mtambo wa kuchimba visima toka Dar es Salaam. Alisema taasisi hiyo inayofanya kazi zake nyingi jijini Dar es Salaam inahofia kupata kadhia kutoka kwa askari hao kama inavyotokea mara kwa mara katika jiji hilo.
Afisa wa NGO ya world share ya nchini korea Nara Kim na mbunge wa jimbo mafinga mjini Cosato Chumi wakisaini mkataba wa makubaliano ya kazi
Afisa wa NGO ya world share ya nchini korea Nara Kim na mbunge wa jimbo mafinga mjini Cosato Chumi wakionyesha sehemu ya mkataba huo.
Balozi wa Korea nchini, Song Geum Young akionyesha taa ndogo za solar kwa ajiri ya kaya masikini katika vijiji ambayo havijafikwa na umeme.
No comments:
Post a Comment