Wednesday, 7 September 2016

TSSA YATOA TAARIFA KWA SERIKALI JUU UKUZAJI UCHUMI NA UJEZI WA VIWANDA NCHINI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Viajana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama akizungumza wakati wa Mkutano wa kupokea taarifa ya Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA), juu ya hatua iliyofikiwa na Mifuko hiyo katika ukuzaji Uchumi na ujenzi wa Viwanda nchini, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa LAPF Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA), Meshach Bandawe akizungumza  wakati wa Mkutano wa kutoa taarifa kwa Serikali  juu ya hatua iliyofikiwa na Shirikisho hilo katika ukuzaji Uchumi na ujenzi wa Viwanda nchini, uliofanyika Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara ambaye pia ni Mjumbe wa Shirikisho hilo, akichangia mada katika Mkutano wa kupokea taarifa ya Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA), juu ya hatua iliyofikiwa na Mifuko hiyo katika ukuzaji Uchumi na ujenzi wa Viwanda nchini, uliofanyika Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka akizungumza wakati Mkutano huo uliotoa taarifa kwa Serikali  juu ya hatua iliyofikiwa na Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA) katika ukuzaji Uchumi na ujenzi wa Viwanda nchini, uliofanyika Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Mkutano huo uliotoa taarifa ya Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA), juu ya hatua iliyofikiwa na Mifuko hiyo katika ukuzaji Uchumi na ujenzi wa Viwanda nchini, uliofanyika Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mwenyekiti wa Shirikisho hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa LAPF, Eliud Sanga.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha wakifatilia kwa makini taarifa hiyo iliyokuwa ikitolewa na Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA), juu ya hatua iliyofikiwa na Mifuko hiyo katika ukuzaji Uchumi na ujenzi wa Viwanda nchini.
Katibu Mkuu ofisi ya Waziri wa Nchi, katika Ofisi ya Waziri Mkuu, 
Sera, Bunge, Kazi, Viajana, Ajira na Walemavu, Eric Shitindi (kulia) akiwa na  Mwenyekiti waShirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA) ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa LAPF, Eliud Sanga wakifatilia Mkutano huo.
Wajumbe wa Mkutano huo kati ya Serikali na Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi za Jamii nchini (TSSA).

WENYE MAJINA HAPO CHINI WATAKIWA KUONANA NA MWAJIRI WAO-MAHAKAMA.

Tunaomba kutoa taarifa kuwa, wenye majina na anuani hapo chini ambao ni watumishi/walikuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania wanahitajika kupata taarifa muhimu na maalum juu ya masuala yahusuyo Utumishi wao: Wafike na kuonana na Bibi. Agatha Ng’ingo – Mkurugenzi Msaidizi- Idara ya Utawala na Utumishi, namba ya simu (0673 – 001 773) ndani ya siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe ya tangazo hili.
S/N
JINA KAMILI
CHEO
KITUO CHA KAZI
C/N

1
BW. ROBERT WILLIAM CHAGAKA
DEREVA II
MAHAKAMA YA WILAYA IRAMBA
111824992

2
BW. GODLISTEN MOSES MWANRI
DEREVA II
MAHAKAMA YA WILAYA KISHAPU
111827839


3
BI. AGNES AUDAX RWEGOSHORA
HAKIMU MKAZI II
MAHAKAMA YA MWANZO UJIJI KIGOMA
111838464

4
BI. HAPPINESS ELIAS MISHWARO
HAKIMU WA MAHAKAMA YA MWANZO MWANDAMIZI
MAHAKAMA YA WILAYA MBARALI
10915901

5
BW. BARAKA JAFARI MUKAMA
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II
MAHAKAMA YA WILAYA ILALA
9927780

6
BW. RAMADHANI MOHAMED KILYOUSUNGU
MLINZI
MAHAKAMA YA WILAYA RUFIJI
9496501

7
BI. REHEMA SAMWEL PANDAPANDA
HAKIMU MKAZI II
MAHAKAMA YA WILAYA MPWAPWA
9927919

8
BI. HAWA GODREY MKUMBO
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II
MAHAKAMA YA WILAYA KASULU
8203232

9
BW.CHRISTINA JOHN MAYILA
MSAIDIZI WA OFISI MWANDAMIZI
MAHAKAMA YA WILAYA KAHAMA
7758540

10
BW. YASSINI WAZIRI MASELE
MLINZI
MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI SINGIDA
111400187

11
BW. JOSEPH FRANCIS BOMA
MLINZI
MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI SINGIDA
111397724

12
BW. BRUTON RABIEL KIMARO
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II
MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI MANYARA
7203497

13
ABIHUDI GILLIARD MASEU
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II
MAHAKAMA KUU ARUSHA
5187924

14
HUSSEIN HASSAN BACHOO
AFISA UGAVI I
DAR ES SALAAM
5529186

15
ASHA MAGOMBA ABDALLAH
MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II
MAHAKAMA YA WILAYA MONDULI
111827925

16
BW. AMRI MUSSA RASHIDI
MLINZI
MAHAKAMA YA WILA
YA TANDAHIMBA
9544435

Imetolewa na,
MTENDAJI MKUU.

WAZIRI MKUU, MAJALIWA AKAGUA UJENZI WA MAKAZI YAKE MAPYA DODOMA

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa na Mkewe Mary  (kushoto)  wakipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama kuhusu ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu, kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia  kwake ) wakikagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Badhi ya Mawaziri na viongozi wa mkoa wa Dodoma baada ya kukagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu kwenye kilima cha Mlimwa mjini Dodoma Septemba 7, 2016. Katikati ni mkewe Mary.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tuesday, 6 September 2016

BENKI YA MAENDELEO YADHAMINI SHINDANO LA GOSPEL STAR SEARCH



Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Benki ya Maendeleo, Peter Tarimo akisaini mkataba wa udhamini wa shindano la Gospel Star Search (katikati) huku meneja wa Mrado huo wa GSS, Samwel Sasali (kushoto) akishuhudia tukio hilo lililofanyika jana hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam.
 
Siku ya jana Kamati Ya Gospel Star Search na Kampuni mbili ambazo ni Maendeleo Bank na Grace Product Wametiliana Mkataba wa Udhamini wa Gospel Star Search 2016. Pichani tukio likifanyika Regency Hotel. Milango ipo wa Wadhamini wengine Pia Makampuni na watu Wa Mavazi Mnakaribishwa.
 
 Meza kuu. 
Ndugu waandishi wa habari tunashukuru sana kwa kuitikia wito wetu siu ya leo, katika project hii kubwa inayoendelea ya Gospel star search. Tulikwisha kuanza toka na tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa mpaka sasa lakini lengo kuu hasa la uwepo wetu hapa siku ya leo ni kuwajuza juu ya uwepo na kutiliana saini na wadhamini wetu ambao wameona ni vyema na tumekubaliana kufanya kazi pamoja katika project hii ya Gospel star search. Nitamkaribisha mwenzangu yeye atasema zaidi kuhusu GSS na hatua tuliofikia mpaka sasa na kuwatambulisha wadhamini wetu.
LENGO KUU Ahsanteni sana waandishi wa habari kwa kuitikia wito wetu, kama alivyosema mwenzangu lengo letu siku ya leo ni kuwatambulisha wadhamini wetu kwenu na kwa watanzania ,lakini kabla ya kwenda mbali ni vyematukatoa mrejesho mfupi juu ya GSS ilipoanza mpaka hatua tuliofikia kwa mwaka huu. 
GSS ina lengo kubwa ya kutafuta waimbaji wa muzii wa injili na kuwasaidia kujitambua kuwapa nafasi ili kukuza vipaji vyao na kuvifanya vionejkane kwa watu kwaajili ya kua faida kw watu lakini hata kwao wenyewe pia.Tunaamini sana kipaji kama kikitumika kwa namna ilio sawa kinaweza kubadili kabisa maisha ya mtu na akawa mtu mwingine mwenye maisha bora yalioletwa na kipaji au talanta alionayo hii ndio sababu tumeipa kauli mbiu ya KIPAJI CHAKO…
HATMA YAKO. Tumeanza na wilaya tatu za mkoa wa Dar es salam kwa sasa, Kinondoni, Temeke pamoja na Ilala na kila sehemu tumechua washiriki wa tano hivyo kua na jumla ya wshiriki 15 kwa wilaya zote 3 ambao hawa ndio wamefanikiwa kuingia hatua ya nuusu fainali. Mchakato wetu umekua na round mbili (2) za mchujo ambazo kwazo ndizo zimetupa washiriki hawa 15 waliopo mpaka hivi sasa. 
Ndugu waandishi wa habari tunashukuru sana wadhamini wetu ambao waliona ni vyeama kushiriki na sisi kwa kutufanyia udhamini kwenye project hii kubwa ya GSS, ambao leo tuko nao hapa kwaajili ya kuwatambulisha rasmi kwenu..ambao ni • Maendeleo Bank • Grace Product • Brand exponetial
• Kiango media • Clouds Media Group • Fm studios (Faith music lab) • 3D Kwa hiyo uwepo wetu hapa ni kuwatambulisha rasmi watu hawa amabao wameona ni vyema kusimama na sisi na pia kutiliana saini mbele yenu kama ishara ya kuingia ubia katika project GSS. Kwa kusema haya sasa nitatoa nafasi kwa wadhamini kusema kdogo ju yao lakini pia juu ya GSS karibuni sana!
HITIMISHO Pia tungependa kuchukua fulsa hii kutoa wito na hamasa kwa makampuni mengine ambao wanaweza kushirikiana na sisi kama wadhamini kweye project hii ya GSS bado milango ipo wazi na tutafurahi sana kushirikiana na ninyi katika project GSS 2016 ,Uwanja wetu ni mpana na jukwaa letu ni kubwa hivyo itakua ni nafasi ya manufaa kwetu na kwenu pia kama mtaamua kutuunga mkono nkwa udhamibni katika project hii ya GSS 2016 kwa hatua zilizosalia za nusu fainali na fainali. Baada ya kusema haya ninaomba niwashukuru tena kwa uwepo wenu na hayo ndio yalikua maelezo juu ya lile lililotuweka hapa siku ya leo. (P.T)

Monday, 5 September 2016

Wazazi Wajitokeza kwa Wingi kupima Watoto Wenye Matatizo ya Moyo

Baadhi ya wazazi na walezi wakisubiri kuingia kwenye chumba cha daktari kwa ajili ya watoto kuchunguzwa kama wana matatizo ya moyo. Watoto watakaobainika watafanyiwa upasuaji na wazazi watatakiwa kuchangia gharama. 
  John Stephen, MNH

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo imeanza kupima watoto bure ili kubaini kama wana matatizo ya moyo watachangia gharama za upasuaji. 

Wazazi na walezi wenye matatizo ya moyo wamejitokeza kwa wingi leo katika taasisi hiyo wakiwa na watoto na kupatiwa vipimo ili kubaini matibabu. 

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Profesa Mohamed Janabi amesema kwamba watoto watakaobainika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa upasuaji.

“Watoto watakaobainika kuwa tatizo tutawafanyia upasuji, wazazi wanatakiwa kuchangia kiasi cha fedha ili kukamilisha matibabu kwa watoto husika,”amesema Profesa Janabi.

Taasisi hiyo imeanza shughuli ya kuwapima watoto ili kubaini kama wana matatizo ya moyo na kuwafanyia upasuaji. Pia, watu wazazi wametakiwa kujtokeza kwa ajili ya watoto kufanyiwa upasuaji.
Baadhi ya wazazi wakiwa na watoto katika chumba cha Dk Stella Mongella wakisubiri watoto wao kufanyiwa vipimo Leo kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Leo Dk Sulenge Kubhoja wa taasisi hiyo, akimchunguza mtoto Lisa Mashauri (2), mkazi wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam.
Dk Sulenge Kubhoja akiendelea na uchunguzi kwa mtoto Hellen Emmanuel kutoka mkoani Iringa.
Baadhi ya wazazi na walezi wakiwa na watoto wao leo nje ya taasisi hiyo kabla ya kuingia katika chumba cha daktari leo.

KAMANDA WA KANDA MAALUM YA DAR ES SALAA SIMON SIRRO AZUNGUMZIA UJAMBAZI

index
Amesema kuwa majambazi walikiri kuwa na wenzao wako katika msitu wa Vikindu.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha kifaa cha kuangalia wakati wakifanya uhalifu majambazi kwa waandishishi wa habari ikiwa ni sehemu ya vifaa vilivyokuwa vikitumika na majambazi sugu leo katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha bunduki  kwa waandishi wa habari ikiwa ni sehemu yabunduki zilivyokuwa zikitumika na majambazi sugu leo katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na waandishi habari juu ya operesheni walioifanya na kukamata majambazi watatu katika viwanja vya ofisi ya kanda maalum leo jijini Dar es Salaam.
 
 
 

Chalila Kibuda wa Michuziblog.

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam  limefakiwa kukamata watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi hatari  ambao wamekuwa wakishiriki matukio mbalimbali ya uhalifu kwa kutumia silaha.
 
Watu hao wanaodaiwa kuwa majambazi walipatikana na bunduki 23 za aina tofauti tofauti, Risasi 835, kifaa cha kuzuia risasi kuingia mwilini tatu (Burret Proof), Sare za Polisi, Pingu 48 pamoja na Radio 12 za mawasiliano.
 
Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya kanda  maalum, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Sirro amesema kuwa majambazi hao walikuwa na mtandao mkubwa ikiwa ni kununua silaha nje ya nchi  kwa ajili ya kufanyia uhalifu katika maeneo mbalimbali.
 
Kamanda Sirro amesema baada ya tukio hilo timu ya polisi ya upelelezi  iliweka mtego na kufanikiwa kukamata majambazi watatu maeneo ya Mbagala, Keko na Kawe.
 
Kamanda Sirro amesema katika mahojiano walikiri kufanya tukio katika benki ya Habib African maeneo ya Kariakoo 2014 na Stanbic 2014.
 
index
 
 
 

KURASA ZA MBELE ZA MAGAZETI YA LEO