Thursday, 28 July 2016

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,MHANDISI MAKANI AFANYA KIKAO NA VIONGOZI WA HIFADHI YA TAIFA YA KISIWA CHA RUBONDO.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mhandisi Ramo Makani akizungumza na viongozi wa serikali ikiwemo kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Geita pamoja na viongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo alipokutana nao katika Hoteli ya Asilia Lodge.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akizungumza na mmoja wa wageni katika Hoteli ya Asilia Lodge iliyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Ugeni wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani ukipunga mikono kuaga wenyeji wao katika Hoteli ya Asilia Lodge ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Naibu Waziri wa Maliasilili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani ,akiviishwa vazi maalum (Boya) ambalo hutumika kujiokoa wakati uafiri wa maji unatumika.

WAGONJWA 45,000 WA SARATANI HUGUNDULIKA TANZANIA KILA MWAKA

Mhe Ummy Mwalimu akiwa na waziri wa afya (Uganda) Mhe .Sara Opendi na Mhe Omar Sey Waziri wa Afya wa Gambia. 
Waziri wa afya Ummy Mwalimu akifuatilia mkutano huo 
.Picha ya pamoja ya wake wa marais na mawaziri wa afya wa afrika,waliohudhuria mkutano wa 10 wa kupambana na saratani ya shingo ya Kizazi,matiti na tezi dume (picha/habari na wizara ya afya)

Na.Mwandishi wetu,Addis Ababa

Ugonjwa wa saratani nchini Tanzania ni chanzo cha magonjwa na vifo,hivyo inakadiriwa Takribani wagonjwa wapya wa saratani 45,000 hugundulika kila mwaka.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika Mkutano wa 10 wa kupambana na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume barani Afrika unaofanyika nchini hapa.

Waziri Ummy amesema kati ya wagonjwa hao asilimia 38 ni wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake, asilimia 14 saratani ya ngozi, asilimia 10 saratani ya matiti na saratani ya tezi ni asilimia 4 . Hatahivyo,takribani watu 35,000 hufariki kila mwaka kutokana na magonjwa ya Saratani.

Licha ya changamoto mbalimbali zinazokwamisha jitihada za kukabiliana na magonjwa hayo ikiwemo uhaba wa Miundombinu ya kutolea huduma za afya, vifaa tiba, Uhaba wa Watumishi wa Afya, rasilimali fedha na gharama kubwa za dawa za matibabu ya saratani,Waziri Ummy amesema Serikali ya Tanzania imepitisha Sera za Kitaifa na Miongozo mbalimbali ya Kupambana na Saratani, kutoe Elimu kwa jamii na watoa huduma za afya nchini kuhusu Saratani.

Aidha, kuanzishwa kwa huduma za upimaji wa saratani katika Hospitali na vituo vya afya zaidi ya 300 nchini na huduma za Tiba kupitia Hospitali ya Saratani ya Ocean Road.

“Serikali itapanua wigo wa matibabu ya saratani katika Hospitali ya Bugando Mwanza na KCMC, Kilimanjaro. Mipango ya baadae ni huduma hizo pia kutolewa ktk Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.”hii itapunguza wagonjwa kufuata huduma kwenye hospitali ya saratani ya Ocean Road

Mkutano wa 10 wa Saratani ya shingo ya kizazi, matiti na tezi dume barani Afrika unafanyika kwa kuasisiwa kwa juhudi za wake za Marais wa bara la Afrika. Mkutano huu unahudhuriwa na Wake wa Marais wa Afrika, Mawaziri wa Afya wa Afrika, Wanataaluma na Wadau wa Maendeleo. Lengo kuu ni kufanya mapitio ya hatua zilizochukuliwa na nchi za Afrika, changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya pamoja na ya nchi katika kukabiliana na saratani.

Wakati wa kukabidhiwa uenyekiti wa Umoja wa Wake wa Marais wa Afrika wa Kupambana na saratani ya Shingo ya Kizazi, Matiti na Tezi Dume kutoka kwa Mwenyekiti anaemaliza muda wake, mke wa Rais wa Kenya mama Magreth Kenyatta, Mke wa Waziri Mkuu wa Ethiopia mama Roman Tesfaye Abneh ameleeza masikitiko yake kwa jinsi ambavyo ugonjwa wa saratani unavyoua kuliko hata ugonjwa wa UKIMWI na kifua kikuu. 
 
Hivyo ameziomba nchi za Afrika kuongeza uwekezaji katika eneo hili hasa kwa kuhakikisha dawa zinakuwepo za kutosha, kuboresha utoaji wa huduma za afya ikiwemo upimàji na tiba, kuhakikisha nchi zinatoa mafunzo ya Kutosha kwa watumishi wa afya katika fani hii

MWENYEKITI WA CCM NA RAIS WA TANZANIA JOHN MAGUFULI AKUTANA NA SEKRETARI YA CCM

Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwasili ukumbini, kuzungumza na Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma, leo. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula na Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Waziri Mkuu Majaliwa KassimMajaliwa, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwasili ukumbini, kuzungumza na Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, Makao Makuu ya CCM, leo. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula na na kshoto baadhi yao ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Waziri Mkuu Majaliwa KassimMajaliwa, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rajab Luhwavi na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye. Picha zote na Bashir Nkoromo)
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (aliyesimama) akitoa maneno ya utangulizi kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli kuzungumza na Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM, Makamo Makuu ya CCM mjini Dodoma leo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula alipowasili Makamo Makuu ya CCMleo, kuzungumza na Wajumbe wa Sekretarieti
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akisalimiana na Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Zakia Hamdan Meghji alipowasili Makamo Makuu ya CCMleo, kuzungumza na Wajumbe wa Sekretarieti
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akisalimiana na Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka, alipowasili Makamo Makuu ya CCMleo, kuzungumza na Wajumbe wa Sekretarieti
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akisalimiana naKatibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi, Seif Shaban Nasoro alipowasili Makamo Makuu ya CCMleo, kuzungumza na Wajumbe wa Sekretarieti
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi alipowasili Makamo Makuu ya CCMleo, kuzungumza na Wajumbe wa Sekretarieti
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu UVCCM, Shaka Hamdu Shaka alipowasili Makamo Makuu ya CCMleo, kuzungumza na Wajumbe wa Sekretarieti
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akisalimiana na Katibu wa CCM wa Shirikisho, Siraji Madebe alipowasili Makamo Makuu ya CCMleo, kuzungumza na Wajumbe wa Sekretarieti
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akisalimiana na Katibu wa Sekretarieti, Anamringi Macha alipowasili Makamo Makuu ya CCMleo, kuzungumza na Wajumbe wa Sekretarieti
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli baada ya Mwenyekiti kuwasili Makao Makuu ya CCM, leo. Kushoto ni Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa na Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI