Waziri wa Habari, sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnaye akizungumza katika uzinduzi wa mashindano ya magari jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Habari, sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnaye akiwa amenyanyua bendera ya Taifa juu kuashiria uzinduzi wa Mashindano ya Mbio za Magari ya 2016 jijini Dar es Salaam leo .Kulia kwa Nape ni Katibu wa Balaza la Michezo Tanzania(BMT), Mohamed Kiganja.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amezindua mashindano ya magari ya hapa nchini ya 2016 na kuwataka watazania kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye mchezo huo ambapo amewataka kuacha kujiweka nyuma na kuitwa kichwa cha mwendawazimu kila siku. Hayo ameyasema wakati akizindua mashindano hayo ya magari yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho wilaya ya Bagamoyo ikihusisha magari 25.
Nape amesema kuwa wanachotaka kuona ni kuwa Tanzania inafanya vizuri kwenye mashindano hayo na zaidi wanataka kuona wanazidi kuwavutia wageni kwenye mashindano hayo ili kuongeza utalii wandani na kuongeza pato kwa serikali pale watakapoamua kutembelea mbuga za wanyama.
“Nawataka watanzania kuzidi kufanya vizuri kwenye mashindano na zaidi wawavutie wageni kwani watakapokuja kwa wingi wataongeza pato la taifa pale watakapotembelea hifadhi za taifa,”amesema.
Naye Rais wa chama cha Magari Tanzania (AAT), Bwana Nizar Jivani amesema kuwa mwaka jana waliweza kuondoa kauli ya kichwa cha mwendawazimu na walilitekeleza kama walivyomuahidi Raisi mstaafu wa awamu ya Pili Ally Hassan Mwinyi na mwaka huu watazidi kufanya vizuri na watabakisha ushindi nyumbani. Mashindano hayo yamezingatia viwango vyote ambapo jumla ya magari 25 yatashiriki ambapo kati ya magari hayo, Magari 4 yatatoka Uganda, 2- Zambia, Kenya (1), Falme za Kiarabu (1). Na kwa magari ya kutoka Tanzannia ni 17.
Magari hayo 17 ya Tanzania ambapo Dar es Salaam magari 10, Arusha (3), Moshi (3), na Tanga (1). Aidha, magari hayo yanatarajiwa kushindana katika umbali wa kilometa 246 kwa siku ya kwanza na yatakuwa kwa muda wa siku mbili.
No comments:
Post a Comment