Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir akitoa Nasaha katika futari Maalum iliyoandaliwa na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ambapo mufti mkuu aliwataka waislam kutojihusisha na matendo ya Kigaidi kwani hayaendani na maelekezo na mafundisho ya Allah.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa neno la shukrani kwa wageni waliojumuika kwenye futari aliyoiandaa nyumbani Oysterbay jijini Dar es Salaam kwake ambapo aliwataka Watanzania kudumisha mani na kuishi kwa upendo
Waalikwa kwenye Futari ilyoandaliwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiswali muda mfupi kabla ya kufuturu.
Sehemu ya Wageni waliohudhuria
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya amani Sheikh Alhad Mussa akizungumza na waalikwa kwenye futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Padri John Solomon akitoa salaam za Kamati ya Amani wakati wa futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
No comments:
Post a Comment