Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati mkutano wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) juu ya utekelezaji wa agizo la kusitisha usajili bodi za wadhamini, Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa RITA, Emmy Hudson (Kulia) akitoa taarifa ya utekelezaji wa agizo la Waziri wa Katiba na Sheria Dk.Harrison Mwakyembe la kusitisha usajili wa bodi za wadhamini leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome.
Sehemu ya wajumbe wa bodi wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Harrison Mwakyembe hayupo pichani leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii).
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwa wakati wa uchguzi mkuu kumekuwa na utitiri wa vikundi ambavyo havionekani kazi zake na mwisho wa siku vinaomba msamaha wa kodi.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwakyembe amesema kutokana na utitiri wa vikundi hivyo aliagiza Wakala wa Usajili ,Ufilisi na Udhamini (RITA), kusitisha usajili wa vikundi hivyo na kufanya uchambuzi ni vikundi ambavyo viko hai na vina vigezo kwa mujibu wa sheria.
Amesema kufanya usajili wa vikundi ambavyo kimsingi hafifanyi kazi iliyokusudiwa mwisho wa siku kuna uwezekano wa kusajili vikundi ambavyo ni hatarishi kwa taifa.
Aidha amesema kuwa kutokana na uchambuzi ambao umefanywa na kubainika kuwepo kwa vikundi 180 ambavyo vinatakiwa kufutwa kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya bodi za udhamini.
Mwakyembe baada uchambuzi huo ameitaka RITA kuendelea na kazi usajili bodi za wadhamini kwa kufuata taratibu zote na kuwa na taarifa zao.
Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (RITA), Emmy Hudson amesekuwa katika uchambuzi huo kuna changamoto ambazo zilijitokeza ikiwa baadhi bodi za wadhamini kubadili ofisi pamoja na kubadili majina bila kufuata sharia.
Amesema kuwa bodi za wadhamini wengine wanamiliki mali bila kufuata sheria kwa mujibu sheria za RITA.
No comments:
Post a Comment