Wednesday, 27 July 2016

MAPAMBANO YA NGUMI SASA KURUSHWA LIVE NA STAR TV

indexMkuu wa vipindi wa Star TV, Yusuph Kamote kushoto  akibadilishana mkataba na Jay Msangi mara baada ya kusainiwa jijini leo. Akishuhudia tukio hilo ni Chief Kiumbe
…………………………………………………………………………………………………………
 Na Mwandishi wetu
Kituo cha Televisheni cha  Star Tv  kimeingia makubaliano na kampuni ya Hall of Fame kwa ajili ya kurusha moja kwa moja ‘live’ mapambano sita ya ngumi za kulipwa nchini kuanzia mwezi ujao.
 
Hatua hiyo ina lengo la kuendeleza mchezo huo ambao ni wa pili kwa kupendwa nchii kwa mujibu wa
Mkuu wa Program wa Star Tv Dar es Salaam, Yusuph Kamote.
 
Kamote alisema kuwa kwa kupigia kituo chao ambacho kina masafa marefu na kupatikana hadi maeneo ya vijijini,  mashabiki wa ngumi za kulipwa watapata fursa ya kujionea ‘live’ mapambano hayo tofauti na awali ambapo mashabiki wa ngumi za kulipwa wa mjini walikuwa wanapata fursa hiyo.
 
“Tumezoa kuona mambo haya katika soka lakini sasa Star Tv imepanua wigo na kuingia kwenye ngumi, tutaonyesha live mapambano yote ambayo Hall of Fame itayaandaa iwe ya hapa nchini au nje ya nchi,” alisema Kamote.
 
Ofisa Mtendaji mkuu wa Hall of Fame, Jay Msangi alisema makubaliano hayo yanatoa fursa kwa kampuni, taasisi na mashirika kujitokeza kudhamini ngumi na kujitangaza ndani na nje ya nchi.
 
“Mpango uliopo ni kuandaa mapambano sita ya kimataifa kila mwaka ambayo yatafanyika hapa nchini na mengine nje ya nchi, hivyo katika kila pambano moja, Kampuni ya  Star Tv italitangaza kwa siku 35 na siku ya pambano litarushwa live, kama litafanyika Dar es Salaam, watazamaji wa Star Tv wa mikoani watapata fursa ya kulishuhudia vivyo hivyo na wale wa Dar es Salaam ambao hawatakwenda ukumbini.
 
“Makubaliano haya sasa yanafungua milango kwa kampuni, taasisi na nashirika kutumia nafasi hiyo kudhamini masumbwi na kujitangaza kila siku katika siku 35 kila baada ya miezi miwili.
 
Naye Mkurugenzi wa Kampuni inayowasimamia mabondia hapa nchini ya Respect Eagle, Chief Kiumbe alisema makubaliano hayo yatasaidia kuinua mchezo wa ngumi na mabondia hapa nchini.
 
“Tumekuwa tukishuhudia mashabiki wakikesha kusubiri mapambano ya Ulaya, tunataka hamasa hiyo ifanyije pia katika mapambano ya hapa nyumbani na tunaamini kwa umoja huu tutafanikiwa.

“Tunahitaji kuleta hamasa mpya katika ndondi na kuendana na kasi ya Serikali ya kuleta maendeleo hivyo umoja huu utaleta taswira mpya ya masumbwi,” alisema Chief Kiumbe

No comments:

Post a Comment