Saturday, 27 August 2016

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI

MUFTI ASEMA BAKWATA HAITISHWI NA MANENO KUHUSU PAUL MAKONDA

MUFTI wa Tanzania, Shehe Mkuu Abubakar Zubery (pichani), amesema Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) halitishwi na maneno yanayoendelea mitandaoni kuhusu kujengewa jengo katika Makao Makuu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye ni Mkristo.

Mufti alisema kumekuwa na maneno mengi, yanayozungumzwa katika mitandao ya kijamii baada ya Makonda kusema atajenga jengo hilo katika makao makuu ya Bakwata, Kinondoni jijini humo, huko wengi wakisema kwa nini baraza hilo limekubali kujengewa na mtu ambaye sio Muislamu.

Alitoa kauli hiyo jana wakati Mkuu wa Mkoa huyo, akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo hilo ambalo litatumia Sh bilioni tano hadi kukamilika kwake.

Mufti Zubery alisema maneno hayo, hayawasumbui na wapo Wakristo wengi waliowahi kuchangia maendeleo kwa Waislamu, lakini hayakutokea maneno kama yanayotokea sasa.

“Kwa nini Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa alipotupa Chuo Kikuu hamkusema? Wapo wadau wengi tu Wakristo walitoa… leo Makonda katoa maneno yamekuwa mengi.

Acheni jamani, mbona hayo ni maneno ya husda na choyo, Waislamu wametoa na sasa Wakristo. Hata Mtume amewahi kupokea misaada kama hiyo,” alisema Mufti.

Kwa upande wake, Makonda alisema hashangazwi na maneno yanayoendelea, kwani Watanzania wamekuwa wakibeza kila jambo zuri linalofanywa na viongozi. Alisema jengo hilo linatarajiwa kujengwa kwa udhamini wa Kampuni ya GSM Foundation, ambao walikubali kujenga kwa gharama zao mpaka kukamilika.

“Wengi waliuliza fedha nitatoa wapi, lakini wanasahau mimi ni mtu wa watu, nimezungumza na wadau wangu, wamekubali kujenga jengo hilo ambalo nimewataka wajenge kwa muda wa miezi kumi na nne,” alifafanua Makonda na kuwataka viongozi wa serikali kutoa kipaumbele kwa viongozi wa dini wanaotaka kupata huduma katika ofisi zao kwani ni watu muhimu na wanapaswa kuwa mbele wanapohitaji huduma.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aongoza ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha 25 cha Wakuu wa Nchi wanaoshiriki kwenye mchakato wa APRM

Mheshimiwa Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha 25 cha Wakuu wa Nchi wanaoshiriki kwenye mchakato wa APRM. Pia walikuwepo Mheshimiwa Dkt Susan Kolimba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mheshimiwa Dkt. Khalid S. Mohamed, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Kikao hicho kilifanyika mjini Nairobi, Kenya; kuanzia tarehe 21-26 Agosti 2016 na kilihudhuriwa na jumla ya Wakuu wa Nchi 22. 

APRM ni Mpango wa Kujitathmini Ki-Utawala Bora uliobuniwa na Wakuu wa Nchi za Kiafrika mwanzoni mwa miaka ya 2000, ili kutatua changamoto za utawala bora zinazolikabili bara la Afrika. Tanzania ni miongoni mwa nchi 35 zinazoshiriki kwenye Mpango huu. 

Kauli mbiu ya kikao hiki ni “kuwa na APRM Imara itakayosaidia kuleta Mabadiliko katika Uongozi barani Afrika” na hivyo kuendelea kuwa chombo kitakachosaidia katika kufikiwa kwa malengo ya Umoja wa Afrika (Agenda 2063) na Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Umoja wa mataifa. 

Kwa mara ya kwanza katika historia ya kuanzishwa kwa Mpango huu, APRM ilipata muda wa siku takriban sita za kuangazia kwa kina masuala mbalimbali ambayo ni pamoja na Ripoti za Tathmini za nchi za Djibouti na Chad, Ripoti ya utekelezaji wa Mpango kazi wa Nchi ya Msumbiji, Mpango Mkakati wa APRM 2016-2020, Mpango Kazi na Bajeti kwa mwaka 2016/17, Masuala mbalimbali yanayohusu utendaji wa Jopo la Watu Mashuhuri, Hati ya Kuinganisha APRM kama Taasisi ndani ya Umoja wa nchi huru za Kiafrika, Taarifa ya Mkaguzi wa Mahesabu ya APRM, Vianzio vya Fedha na Maeneo ya changamoto yanayopendekezwa kuingizwa kwenye Hojaji Kuu ya APRM pamoja na kuzingatiwa kwenye mbinu za tathmini y utawala bora kwa vipindi vijavyo. 

Maeneo mtambuka katika Afrika yaliyoonekana kuhitaji mikakati endelevu ya pamoja katika kuyatafutia ufumbuzi ni pamoja na; Minyukano ya kimtazamo hasa juu ya itikadi, sekta binafsi kutowezeshwa vya kutosha, miundo mbinu duni ikiwa nia pamoja na nishati, barabara, reli, simu, mitandao ya mawasiliano n.k, dola zisizokuwa imara, changamoto zihusuzo masoko, ukosefu wa viwanda pamoja na usindikaji wa bidhaa usiyoridhisha, uhaba wa wataalam, maendeleo duni katika sekta ya kilimo, maendeleo duni katika sekta ya huduma ikiwa ni pamoja na benki, bima, utalii n.k, udhaifu kwenye mifumo ya kidemokrasia na udhaifu wa uwajibikaji katika sekta ya umma. Baada ya mjadala wa kina kuhusu maeneo yaliyotajwa hapo juu, ilikubalika kuwa, Hojaji Kuu ya APRM pamoja na mbinu za tathmini zifanyiwe marekebisho ili kulenga zaidi mambo hayo muhimu na hatimaye kuungezea mchakato wa APRM thamani zaidi. 

Tanzania inaendelea kutekeleza Mpango kazi wa APRM kwa kushirikiana na Wizara, Idara na Wakala za Serikali, pamoja na kuishirikisha Sekta Binafsi.

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AKUTANA NA BALOZI MDOGO WA CHINA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akisalimiana na Mgeni wake Balozi mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe,Xie XiaowuTek Chand Barupai alipofika Ikulu Mjini Unguja leo, 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akizungumza na Mgeni wake Balozi mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe,Xie XiaowuTek Chand Barupai alipofika Ikulu Mjini Unguja leo,[Picha na Ikulu.]26/08/2016. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akiagana na Mgeni wake Balozi mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyia kazi Zanzibar Mhe,Xie XiaowuTek Chand Barupai alipofika Ikulu Mjini Unguja leo baada ya mazungumzo yao,[Picha na Ikulu.]26/08/2016.

Mafundi wa TEMESA washauriwa kutumia mafunzo waliyoyapata kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri(katikati aliyesimama) akizungumza na mafundi wa TEMESA wakati akifunga mafunzo ya mafundi wa Wakala hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016. 
Kaimu Mtendaji TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan(kulia) akitoa neno kwa mafundi wa TEMESA wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016 kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri . 
Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri akionesha moja ya vifaa vilivyokabidhiwa na mafundi wa TEMESA kwa ajili ya karakana zao wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016. 

Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri akikabidhi cheti kwa mmoja wa mafundi Bw.Saidi Waziri kutoka Arusha wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016. 

Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri akikabidhi moja ya vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya karakana za TEMESA kwa Bw. Japhet Mwita mmoja wa washiriki wa mafunzo yaliyofanyika hivi karibuni katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016. 

Baadhi wa mafundi wa Temesa kutoka mikoa mbalimbali nchini wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016. 

Picha/Habari na Theresia Mwami TEMESA 

Mafundi wa TEMESA wameshauriwa kutumia mafunzo waliyoyapata kuendana na mabadiliko ya teknolojia katika utengenezaji magari na vifaa vya umeme. Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Bodi ya Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi Wakala hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT). 

Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri amesema kuwa Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA imedhamiria na kuhakikisha kuwa magari na mitambo yote ya Serikali inatengenezwa kitaalam ili kuleta tija na thamani halisi ya fedha iliyokusudiwa pamoja na kukidhi kiu na matarajio ya wateja. 

”Napenda kuwakumbusha kwamba mnayo dhamana kubwa ya kutengeneza magari ya Serikali hivyo kwa mafunzo mliyoyapata ninaamini mmejenga uwezo wa kutosha wa kuhudumia magari na vifaa vya umeme kwa kutumia mfumo wa kisasa” alisema Mhandisi Mashauri. 

Ameongeza kuwa ni fursa pekee kwa mafundi waliopata mafunzo hayo kwenda kuwafundisha wenzao ambao hawakuweza kupata mafunzo hayo ili kuongeza kasi ya kutengenza magari na vifaa vya umeme na kupunguza changamoto zilizopo katika utengenezaji magari kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA). 

Aidha Kaimu Mtendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan amewashukuru washirika wa TEMESA wakiwemo Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kampuni ya Superdoll kwa kuwezesha kufanyika kwa mafunzo hayo ambayo yataleta chachu ya utendaji kazi wa mafundi na karakana za TEMESA zilizopo nchini nzima. 

Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kampuni ya Superdoll waliandaa mafunzo ya siku 14 yaliyoanza Agosti 9 na kumalizika Agosti 26, 2016 yaliyoshirikisha jumla ya mafundi 25 kutoka mikoa mbalimbali ili kuwapa uwezo wa kutengeneza magari kwa kutumia mifumo ya kisasa.

MAJAMBAZI WASAFISHA NYUMBA YA Q CHIFU

Q Chief
Q Chief amethibitisha nyumba yake kuvamiwa na majambazi na wamefanikiwa kuiba baadhi ya vitu vilivyomo ndani ikiwemo laptop iliyokuwa na baadhi ya colabo zake.

Akiongea na Clouds FM, muimbaji huyo amedai kuwa thamani ya vitu vyake vilivyoibiwa ni kama milioni mbili au tatu.
“Watumishi wa shetani wameamua kufanya kitu cha kihistoria, siku zote wanarukaruka mmoja wawili tunapigiza nao kelele wanaondoka lakini this time wamekuja watu kama sita, saba au nane. Wamekuja na mapanga, wamekuja na mafokolisti yale ya kufungua, wamekuja na gari moja nje sasa sijui walikuwa wanataka kubeba kila kitu?,” ameuliza Q Chief.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aongoza ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha 25 cha Wakuu wa Nchi wanaoshiriki kwenye mchakato wa APRM

Mheshimiwa Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha 25 cha Wakuu wa Nchi wanaoshiriki kwenye mchakato wa APRM. Pia walikuwepo Mheshimiwa Dkt Susan Kolimba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mheshimiwa Dkt. Khalid S. Mohamed, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Kikao hicho kilifanyika mjini Nairobi, Kenya; kuanzia tarehe 21-26 Agosti 2016 na kilihudhuriwa na jumla ya Wakuu wa Nchi 22. 

APRM ni Mpango wa Kujitathmini Ki-Utawala Bora uliobuniwa na Wakuu wa Nchi za Kiafrika mwanzoni mwa miaka ya 2000, ili kutatua changamoto za utawala bora zinazolikabili bara la Afrika. Tanzania ni miongoni mwa nchi 35 zinazoshiriki kwenye Mpango huu. 

Kauli mbiu ya kikao hiki ni “kuwa na APRM Imara itakayosaidia kuleta Mabadiliko katika Uongozi barani Afrika” na hivyo kuendelea kuwa chombo kitakachosaidia katika kufikiwa kwa malengo ya Umoja wa Afrika (Agenda 2063) na Malengo Endelevu ya Maendeleo ya Umoja wa mataifa. 

Kwa mara ya kwanza katika historia ya kuanzishwa kwa Mpango huu, APRM ilipata muda wa siku takriban sita za kuangazia kwa kina masuala mbalimbali ambayo ni pamoja na Ripoti za Tathmini za nchi za Djibouti na Chad, Ripoti ya utekelezaji wa Mpango kazi wa Nchi ya Msumbiji, Mpango Mkakati wa APRM 2016-2020, Mpango Kazi na Bajeti kwa mwaka 2016/17, Masuala mbalimbali yanayohusu utendaji wa Jopo la Watu Mashuhuri, Hati ya Kuinganisha APRM kama Taasisi ndani ya Umoja wa nchi huru za Kiafrika, Taarifa ya Mkaguzi wa Mahesabu ya APRM, Vianzio vya Fedha na Maeneo ya changamoto yanayopendekezwa kuingizwa kwenye Hojaji Kuu ya APRM pamoja na kuzingatiwa kwenye mbinu za tathmini y utawala bora kwa vipindi vijavyo. 

Maeneo mtambuka katika Afrika yaliyoonekana kuhitaji mikakati endelevu ya pamoja katika kuyatafutia ufumbuzi ni pamoja na; Minyukano ya kimtazamo hasa juu ya itikadi, sekta binafsi kutowezeshwa vya kutosha, miundo mbinu duni ikiwa nia pamoja na nishati, barabara, reli, simu, mitandao ya mawasiliano n.k, dola zisizokuwa imara, changamoto zihusuzo masoko, ukosefu wa viwanda pamoja na usindikaji wa bidhaa usiyoridhisha, uhaba wa wataalam, maendeleo duni katika sekta ya kilimo, maendeleo duni katika sekta ya huduma ikiwa ni pamoja na benki, bima, utalii n.k, udhaifu kwenye mifumo ya kidemokrasia na udhaifu wa uwajibikaji katika sekta ya umma. Baada ya mjadala wa kina kuhusu maeneo yaliyotajwa hapo juu, ilikubalika kuwa, Hojaji Kuu ya APRM pamoja na mbinu za tathmini zifanyiwe marekebisho ili kulenga zaidi mambo hayo muhimu na hatimaye kuungezea mchakato wa APRM thamani zaidi. 

Tanzania inaendelea kutekeleza Mpango kazi wa APRM kwa kushirikiana na Wizara, Idara na Wakala za Serikali, pamoja na kuishirikisha Sekta Binafsi

MWANDISHI WA HABARI MARY LYIMO KUZIKWA LEO

Mwandishi wa Habari Mary Jovian Lyimo amefariki dunia Agosti 23 baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa Kansa ya Ini, kwa mujibu wa Dada wa marehemu, Liliani Jovian Lyimo amesema kuwa marehemu enzi za uhai wake aliwahi kufanya kazi katika Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASCO), kama Ofisa habari wa shirika hilo, pia alifanya kazi katika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Marehemu atazikwa leo Agosti 27 saa nane katika makaburi ya Kondo Kunduchi jijini Dar es Salaam. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amani.

Wednesday, 24 August 2016

DRC yaonesha nia na Bomba la Mafuta, Afrika Mashariki

Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Mhe. Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese amesema Serikali ya Kongo iko tayari kushirikiana na serikali ya Tanzania kwenye Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki.

Mhe Lusa- Diese aliyasema hayo katika kikao kilichokutanisha ujumbe wake na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na taasisi zake kilichofanyika jijini Dar es Salaam. 

Alisema kuwa lengo la ziara yake lilikuwa ni Serikali ya Kongo kuomba kushiriki na kuwa sehemu ya mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki linalojengwa kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania kutokana na kwamba sehemu ya Kongo ina mafuta. 

Alisema kuwa nchi ya Kongo kupitia wataalam wake ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Madini ili kufanikisha mradi mkubwa wa bomba la mafuta ambalo litanufaisha nchi zote za Afrika Mashariki. 

Naye Mkurugenzi kutoka Kampuni ya Oil of DR Kongo kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Giuseppe Ciccarelli alisema kampuni yake ina uzoefu kwenye utafiti na uchimbaji wa mafuta na kusisitiza kuwa mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki, kampuni yake itakuwa na uwezo wa kusafirisha kuanzia mapipa 30,000 hadi 100,000 kwa siku kulingana na mahitaji. 

Aliishukuru serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Madini kwa kuwa tayari kushirikiana na Kongo kwenye mradi wa bomba la mafuta na kuongeza kuwa kupitia mradi huu nchi zote kwa pamoja zitapata mapato na kukua kwa uchumi wake. 

Awali akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo alisema kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana na Kongo katika mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki na kuelekeza wataalam kutoka nchi zote mbili kuanza kukutana kuanzia sasa kwa ajili ya kujadili mpango wa ujenzi wa bomba hilo na kumwalika Waziri wa Mafuta wa Kongo, Mhe Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese kwenye kikao cha Mawaziri wa Nishati na Madini kutoka nchi za Tanzania na Uganda kinachotarajiwa kufanyika Tanga mapema mwezi Oktoba. 

Katika hatua nyingine Profesa Muhongo alisema kuwa nchi ya Kongo imeonesha nia kwenye utafiti wa mafuta katika Ziwa Tanganyika na kuongeza kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana na nchi ya Kongo kupitia kampuni za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi ili kuongeza kasi ya ugunduzi wa mafuta katika ziwa hilo lenye viashiria vya mafuta. 

Aidha alisisitiza kuwa mara baada ya ugunduzi wa mafuta katika Ziwa Tanganyika, nchi za Tanzania, Kongo na Burundi zitanufaika kupitia mapato pamoja na kuongezeka kwa ajira.

Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiongoza kikao kilichoshirikisha Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese na ujumbe wake, pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akielezea fursa za uwekezaji kwenye sekta ya mafuta na gesi mbele ya waandishi wa habari. Kushoto ni Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese.
Mkurugenzi kutoka Kampuni ya Oil of DR Kongo kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Giuseppe Ciccarelli akisisitiza jambo katika kikao hicho.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akipeana mikono na Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Aime Ngoi-Mukena Lusa- Diese (kushoto)

PICHA KALI KUTOKA KWA MWANADADA MWAMVITA MAKAMBA

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI