Tuesday, 2 August 2016

MSANII PATORANKING AANZA ZIARA YA UZINDUZI WA ALBAMU YAKE NCHINI TANZANIA

 Mwanamuziki maaarufu anaetambulika zaidi kwa miondoko ya dancehall na reggae kutoka nchini Nigeria Patrick Nnaemeka Okorie aka Patoranking akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ziara yake ya siku moja jijini Dar es salaam ya kuitambulisha album yake mpya inayokwenda kwa jina la “God over everything”. Pamoja nae ni Meneja Mkuu Masoko wa kampuni ya Spice Africa Joan Nkuzi ambapo kupitia programu yao ya Mziiki wanajishughulisha na uendelezaji wa kazi za wasanii mbalimbali nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.
 Mwanamuziki maaarufu anaetambulika zaidi kwa miondoko ya dancehall na reggae kutoka nchini Nigeria Patrick Nnaemeka Okorie aka Patoranking alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) siku ya jana jioni kwa ziara yake ya siku moja tu jijini Dar es salaam ya kuitambulisha albamu yake mpya aliyoipa jina la “God over everything” kwa mashabiki wake nchini Tanzania.
Toka kushoto ni Meneja Mkuu Masoko wa kampuni ya Spice Africa Joan Nkuzi, Mwanamuziki maaarufu anaetambulika zaidi kwa miondoko ya dancehall na reggae kutoka nchini Nigeria Patrick Nnaemeka Okorie a.k.a Patoranking, Meneja bidhaa wa Spice Africa Mariam Nnauye pamoja na Meneja wa Msanii huyo nchini Tanzania Tom Raymond kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza shughuli ya utambulisho wa album ya msanii huyo kwa waandsihi wa habari katika hafla iliyofanyika jana usiku ndani ya ukumbi wa Paparazzi jijini Dar es salaam. Msanii huyo alikuwa nchini kwa ziara ya siku moja kuitambulisha albamu yake ya “God over everything” kwa mashabiki wake nchini Tanzania.

Albamu iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu inayoitwa“God over Everthing” (GOE) kutoka kwa nyota wa mtindo wa reggae/dancehall wa kinigeria Patrick Nnaemeka Okorie a.k.a Patoranking hatimaye imekemilika.

Mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu nyerere (JNIA) jana jioni, msanii huyo wa miondoko ya reggae pamoja na timu yake iliyopokelewa na Spice Africa, kampuni ambayo inayofanya kazi na Patoranking katika kutangaza mziki wake na usambazaji wa albamu mpya ya msanii huyo kwa nchini Tanzania.

Akizungumza kwenye mkutano wa vyombo vya habari uliofanyika katika ukumbi wa Paparazi-Slipway jioni hiyo hiyo, msanii huyo alitambulisha baadhi ya vibao/nyimbo zake ambazo ziko katika albamu hiyo, baadhi ambazo tayri zinafanya vizuri katia anga za kimataifa kama “Girlie O”, “My woman”, “Make Am”, “Another Level”, “Alubarika” na wimbo wake mpya wa hivi karibuni “No Kissing Baby”aliomshirikisha msanii Sarkodie kutoka Ghana. Albamu hiyo imebeba nyimbo zilizotengenezwa katika label yake ya VP records yenye idadi ya zaidi ya nyimbo 16.

“Albamu hii ni ya kipekee; ina nyimbo kwaajili ya kila mtu, kwa watu wenye umri wowote na kila kona ya Afrika. Nilitaka kulipa fadhila/Heshima kwa asili yangu na pia kukumbatia mfumo mpya wa muziki wa kiafrika ambao unashika kasi Ulimwenguni kwa sasa. Nina furaha sana kuitambulisha albamu yangu kwa mara ya kwanza duniani kwa mashabiki wangu waTanzania”….alisema Patoranking.

Msanii huyo pia alitumia muda huo kufafanua kwanini alichagua Dar es salaam kama Jiji la kwanza kuitambulisha albamu yake mpya, “watanzania ni watu wazuri sana, nimeona wasanii wengi kutoka Nigeria na mataifa mengine wakija kufanya shoo hapa jinsi wanavyopokelewa vizuri na upendo mkubwa”. Aliwataja baadhi ya wasanii  wa Kitanzania ambao nyota huyu anapanga kufanya nao kazi akiwemo: Navy Kenzo na Vanessa Mdee a.k.a  V-Money ambao kwa maelezo yake ni kama wanafamilia.

Aliwashukuru mashabiki wake na vyombo vya habari vya Tanzania kwa kuunga mkono mziki wake  kabla  hajabainisha kuwa atatembelea Nairobi, Kampala na Accra-Ghana kuitambulisha albamu hiyo kabla ya kurudi nyumbani.

Patoranking pia aliendelea kutaja siri ya kuwa ameanzisha lebo ya kurekodi /studio aliyoiita “his baby”, ambayo msanii wa kwanza ametokea kutoka hapa hapa Tanzania, “Jina lake ni Walid, mnaweza msimfahamu kwa sasa, lakini mtamfahamu, huyu amekusudiwa kufanya mambo makubwa” alisema Patoranking

Kwa upande wake Meneja wa Masoko wa Spice Africa Joan Nkuzi amesema, ni heshima kubwa sana kwa Msani  nyota wa Nigeria kutambulisha albamu yake kwa mara ya kwanza hapa Tanzania na ndio maana hawakusitasita kuunga mkono juhudi zake. Jukumu kubwa lab Spice Africa kupitia application yake ya Mziiki ni kupeleka muziki wa Kiafrika duniani kote kama wakusanyaji na wasambazaji walioko katika masoko zaidi ya 12 ndani ya Afrika, walitoa uhakika sio tu kufanya kazi na wasanii wenye vipaji, bali pia wasanii ambao ni wanyenyekevu na ambao wanajua malengo yao – ambapo mmoja wao ni Patoranking.

No comments:

Post a Comment