Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri(katikati aliyesimama) akizungumza na mafundi wa TEMESA wakati akifunga mafunzo ya mafundi wa Wakala hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.
Kaimu Mtendaji TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan(kulia) akitoa neno kwa mafundi wa TEMESA wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016 kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri .
Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri akionesha moja ya vifaa vilivyokabidhiwa na mafundi wa TEMESA kwa ajili ya karakana zao wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.
Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri akikabidhi cheti kwa mmoja wa mafundi Bw.Saidi Waziri kutoka Arusha wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.
Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri akikabidhi moja ya vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya karakana za TEMESA kwa Bw. Japhet Mwita mmoja wa washiriki wa mafunzo yaliyofanyika hivi karibuni katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.
Baadhi wa mafundi wa Temesa kutoka mikoa mbalimbali nchini wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.
Picha/Habari na Theresia Mwami TEMESA
Mafundi wa TEMESA wameshauriwa kutumia mafunzo waliyoyapata kuendana na mabadiliko ya teknolojia katika utengenezaji magari na vifaa vya umeme. Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Bodi ya Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi Wakala hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri amesema kuwa Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA imedhamiria na kuhakikisha kuwa magari na mitambo yote ya Serikali inatengenezwa kitaalam ili kuleta tija na thamani halisi ya fedha iliyokusudiwa pamoja na kukidhi kiu na matarajio ya wateja.
”Napenda kuwakumbusha kwamba mnayo dhamana kubwa ya kutengeneza magari ya Serikali hivyo kwa mafunzo mliyoyapata ninaamini mmejenga uwezo wa kutosha wa kuhudumia magari na vifaa vya umeme kwa kutumia mfumo wa kisasa” alisema Mhandisi Mashauri.
Ameongeza kuwa ni fursa pekee kwa mafundi waliopata mafunzo hayo kwenda kuwafundisha wenzao ambao hawakuweza kupata mafunzo hayo ili kuongeza kasi ya kutengenza magari na vifaa vya umeme na kupunguza changamoto zilizopo katika utengenezaji magari kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Aidha Kaimu Mtendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi Manase Ole Kujan amewashukuru washirika wa TEMESA wakiwemo Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kampuni ya Superdoll kwa kuwezesha kufanyika kwa mafunzo hayo ambayo yataleta chachu ya utendaji kazi wa mafundi na karakana za TEMESA zilizopo nchini nzima.
Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kampuni ya Superdoll waliandaa mafunzo ya siku 14 yaliyoanza Agosti 9 na kumalizika Agosti 26, 2016 yaliyoshirikisha jumla ya mafundi 25 kutoka mikoa mbalimbali ili kuwapa uwezo wa kutengeneza magari kwa kutumia mifumo ya kisasa.
No comments:
Post a Comment