Mtangazaji maarufu wa kipindi cha Mkasi na Ngazi kwa ngazi,Salama Jabir amemtaja Vee Money kama mmoja wa wasanii wa bongo fleva ambao anaamini watafika mbali zaidi kutokana na kuwa na kipaji cha hali ya juu na kujituma sana.
Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times Fm,Salama amedai kwa sasa Vee Money ni kama ana pasha tu kwenye muziki kutokana na mipango anayomwona nayo.
“Yani namuamini Vee Money mno kwa sababu nae anajiamini, sasa hivi mbona bado ni kama anafanya Warm up vile, kuna vitu akivianza hivyo utaniambia, unajua Vanessa anaimba sana na atafika mbali” Alisema.
No comments:
Post a Comment