Moja ya headline kwenye mitandao ya kijamii iliyochukua nafasi usiku wa August 22 2016 ni pamoja na tukio la kumbukumbu ya kuzaliwa kwa staa wa bongo flava kutokea katika label ya WCB Raymond ambapo uongozi wake uliamua kumfanyia suprise ya zawadi ya gari aina ya Toyota Rav 4 yenye thamani ya milioni 20 za kitanzania.
Leo August 23 Raymond kupitia ukurasa wake wa instagram aliamua kuyatoa yake ya moyoni kwa kuandika…
’Kweli Nimeamini Mungu Hana upendeleo.nilikua mtu nilie jikatia tamaa ndani ya miaka takribani mi nne nilikua nikiangaika na muziki wangu nakushukuru sana sana‘
‘Kaka Lao Diamond Platnumz Umenifundisha vitu vingi saaaaaanaaa hadi leo naiona njia boss wangu Babu Tale ni mwaka wa tano sasa toka Umenijua umenivumilia kwa mengi hadi leo hii haujanichoka na unanisaidia kwa moyo mmoja’
‘Boss Sallam Sk Asante sana kwakupigania kila siku thamani ya muziki wangu nakuakikisha nafika sehemu nzuri Mkubwa Fella wewe ni zaidi ya mzazi maana umenilea nakunifundisha meeengi kwenye muziki‘
‘Madee Sitoacha kukushukuru kaka lao wewe nikioo naamini unafurahi kuniona mdogo wako hapa nilipo maana unanijua saaaaanaaaa‘
No comments:
Post a Comment