Tuesday, 31 May 2016

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI MUHIMBILI



Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) LEO. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamedi Janabi, Katibu wa baraza hilo, Dk Kissa Mwambene. Kushoto ni Mwenyekiti wa baraza hilo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia Makani.PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI (MNH)
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakipiga makofi wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya wakizungumza na wajumbe wa baraza hilo Leo kwenye hospitali hiyo.Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi LEO kabla ya kupiga kura za kuwachagua viongozi wapya wa baraza hilo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia Makani wa hospitali hiyo.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la MNH wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru katika kikao hicho.
Wajumbe wakipiga kura LEO za kuwachagua viongozi wapya wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali hiyo.
Dk Kissa Mwambene akiwashukuru wajumbe baada ya kumchagua Leo kuwa Katibu wa baraza hilo.
Wakili Eneza Msuya akiwashukuru LEO wajumbe baada ya kumchagua kuwa Katibu Msaidizi wa baraza hilo.
Kutoka kushoto ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa hospitali hiyo, Dk Kissa Mwambene, Mwenyekiti wa baraza hilo, Profesa Lawrence Museru, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamedi Janabi, Katibu Msaidizi wa baraza hilo, Wakili Eneza Msuya na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia Makani.

ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA KUPINGA MATUMIZI YA TUMBAKU DUNIANI



Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Zanzibar Dkt. Ghirmany akitoa taarifa ya Shirika hilo kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Wizara ya Afya Zanzibar.Picha Na Miza Othman – Maelezo Zanzibar.

Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar

Inakadiriwa zaidi ya watu milioni sita duniani kote hupoteza maisha kila mwaka kutokana na athari za matumizi ya tumbaku na wanaoathirika zaidi ni vijana wenye umri wa miaka 30 hadi 39.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Wizara ya Afya kwenye maadhimisho ya siku ya kupinga matumizi ya tumbaku Duniani, Meneja wa Kitengo cha maradhi yasiyoambukiza Zanzibar ndugu Omar Mwalimu Omar amesema mbali na kusababisha vifo, matumizi ya tumbaku yamekuwa chanzo kikubwa cha maradhi.

Amesema tafiti zilizofanyika zimeonyesha kuwa matumizi ya tumbaku yanachangia kwa asilimia 71 kupata saratani ya mapafu, asilimia 42 magonjwa ya njia za hewa na asilimia kumi magonjwa ya moyo.

Ndugu Omar amesema pamoja na kuwa Zanzibar haizalishi tumbaku na haina viwanda vya sigara, bado matumizi ya bidhaa hizo ni ya kiwango cha juu.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Wizara ya Afya mwaka 2011ulionyesha asilimia 7.3 ya wazanzibari kati ya miaka 25 hadi 64 ni watumiaji wa sigara na asilimia 4.1 wanatumia tumbaku kwa njia za kunusa na kuvuwata.

Meneja wa Kitengo cha maradhi yasiyoambukiza amezitaja athari nyengine zinazotokana na matumizi ya tumbaku ni kuanguka kwa uchumi wa nchi.

“Kama nilivyotangulia kusema, rika linaloathirika zaidi ni vijana wa miaka 30 hadi 39 ni wazi kuwa nchi zinapoteza nguvu kazi ambayo ipo katika umri wa kuongeza kipato cha nchi,” alisisitiza Ndugu Omar.

Amekiri kuwa katika vita vya kupambana na matumizi ya tumbaku kumejitokeza changamoto ya viwanda vinavyotengeneza bidhaa za tumbaku kuwa na nguvu kubwa ya kifedha na matumizi ya tumbaku imekuwa moja kati ya starehe hususan katika jamii ya vijana.

Amewataka waandishi wa habari kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Wizara ya Afya ya kudhibiti matumizi ya tumbaku kwa kuitanabahisha jamii juu ya athari zinazotokana na tumbaku.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) aliepo Zanzibar Dkt. Ghirmany amesema Umoja wa Mataifa umepanga kila ifikapo tarehe 31 Mei ya kila mwaka iwe ni siku ya kupinga matumizi ya bidhaa zinazotokana na tumbaku ili kuitanabahisha jamii juu ya athari inayotokana na tumbaku.

Ameishauri Serikali kuandaa kanuni ya matumizi ya tumbaku ili sheria iliyotungwa ya kudhibiti uvutaji wa sigara katika maeneo ya wazi iweze kufanya kazi.

Ujumbe wa mwaka huu katika kuadhimisha siku ya kupinga matumizi ya tumbaku Duniani ni ‘kuwa tayari kuondosha vivutio katika paketi za kuhifadhia sigara’.

WAZIRI WA AFYA MHE.UMMY MWALIMU ATOA TAMKO KUHUSU SIKU YA KUPINGA MATUMIZI YA TUMBAKU DUNIANI, TAREHE 31 MEI 2016




Siku ya kupinga matumizi ya Tumbaku Duniani, huadhimishwa duniani kote kila mwaka tarehe 31 Mei.Kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya kupinga matumizi ya tumbaku mwaka 2016 ni “jiandae kwa pakiti zisizo na matangazo wala vivutio”Kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha jamii juu ya kujiepusha au kujikinga na vivutio mbalimbali vya matangazo yanayo hamasisha matumizi ya sigara ambayo ina madhara mengi kiafya.


Tanzania kama zilivyo nchi nyingine duniani inaadhimisha siku hii, kwa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kutoa elimu ya umuhimu wa kuzuia na kujikinga na matumizi ya sigara na bidhaa za tumbaku.Tafiti nyingi zinathibitisha madhara yatokanayo na matumizi ya tumbaku ni pamoja na magonjwa yasiyoambukiza kama vile saratani, magonjwa ya mishipa ya damu na moyo, kiharusi, magonjwa ya njia ya hewa.Tafiti pia zinaonyesha takriban watu 6,000,000 hupoteza maisha duniani kwa mwaka kwa utumiaji wa tumbaku na bidhaa zake.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani kwa mwaka 2016, inalenga kuelimisha na kuhamasisha jamii kuachana na matumizi ya tumbaku na kusisitiza kwa wazalishaji kutokuweka maandishi au nembo zinazovutia ili kuishawishi jamii kutumia bidhaa hizo. Aidha tumbaku imekuwa ikisababisha madhara kiafya kama vile magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza. 

Magonjwa hayo ni magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, saratani, ugonjwa wa kisukari na magonjwa ya njia ya hewa.Mambo mengine yanayoongeza uwezekano wa kupata magonjwa yasiyoambukiza ni pamoja na ulaji usiofaa hasa matumizi ya chumvi kupita kiasi, kutofanya mazoezi, unywaji pombe kupita kiasi na msongo wa mawazo.

Ili kuzuia maradhi yasiyoambukiza yatokanayo na matumizi ya tumbaku na bidhaa zake ni muhimu kufuata kanuni za afya ambazo ni kutovuta sigara na kama wewe ni mvutaji, kutovuta sigara hadharani maana madhara yake ni sawa hata kwa mtu asiyevuta ambaye anapata moshi kutoka kwa mvutaji, kuendelea kuielimisha jamii juu ya madhara mbalimbali yatokanayo na utumiaji wa tumbaku hususani kwa vijana.

Serikali inaendelea na mkakati wa tiba kwa watu wenye uraibu wa matumizi ya tumbaku, ikiwa na lengo kupunguza matumizi hayo miongoni mwa jamii. Kuhakikisha pakiti za tumbaku na bidhaa zake ziwe na tahadhari ya madhara ya utumiaji wa tumbaku na bidhaa zake. Aidha, serikali, inaendelea kurekebisha sheria, kanuni na taratibu za udhibiti wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatumia maadhimisho haya kuwa sehemu ya uhamasishaji kwa jamii kama ilivyo kwenye nchi zote duniani.

SERIKALI KUANZISHA BAENKI YA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI.

MS2Na Lilian Lundo-MAELEZO
Serikali ya awamu ta Tano imedhamiria kuifanya sekta ya Viwanda nchini kuchangia pato la taifa kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka asilimia 7.3 ya sasa
Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema kuwa jambo hilo linawezekana hasa kwa kuzingatia nchi yetu ina rasilimali zinazohitajika katika kujenga uchumi wa viwanda.
“Nafahamu kwamba tunakila aina ya rasilimali inayowezesha uwepo wa viwanda hapa nchini ikiwemo umeme wa kutosha pamoja na malighafi zake na kwa maana hiyo serikali ya awamu ya tano imepanga kuifanya sekta ya viwanda kuchangia pato la taifa kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka 7.3 ya sasa”. Alisema Rais Magufuli.
Aidha Dkt. Magufuli aliwatoa wasiwasi wadau hao kuhusu uwepo wa soko la uhakika kwa bidhaa zitakazozalishwa kwani Tanzania imezungukwa na nchi zenye uhitaji wa bidhaa mbalimbali na pia ni Mwanachama wa jumuiya mbalimbali ndani na nje ya Afrika.
Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage aliwataka wamiliki wa Viwanda Nchini kuunganisha nguvu katika uanzishaji na uendelezaji wa viwanda nchini ili kuongeza upatikanaji wa bidhaa nchini hali itakayopelekea kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa watanzania.

YALIYOJIRI KWENYE KIKAO CHA 33 CHA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  Baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wakielekea ndani ya Ukumbi wa Bunge
leo kusikiliza Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Elimu,
Sayansi na Mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na Mbunge wa
Afrika Mashariki Mhe. Shy-Rose Bhanji nje ya Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.
Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi akichangia kuhusu Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga leo mjini Dodoma.
Baadhi ya Mawaziri wakifuatilia michango mbalimbali ya wabunge wakati wa mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliyowasilishwa leo mjini Dodoma.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvu akizungumza na Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mh. Peter Msigwa mara baada ya kikao cha bunge kuahirishwa mchana leo, Kushoto anayecheka  ni Mh. Balozi Augustino Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa.

NHIF YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WAKAZI WA JIJI LA TANGA KWENYE MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA.

MENEJA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOAN TANGA(NHIF) ALLY MWAKABABU AKIMSIKILIZA KWA UMAKINI MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA MWANANCHI ,BURHUANI YAKUB MWENYE TISHETI YA BLUU ALIYEKATA UFFANUZI KUHUSU HUDUMA ZAO.

KUSHOTO NI AFISA MATEKELEZO WA NHIF MKOA WA TANGA,MIRAJI KISILE AKIMUHUDUMIA MKAZI WA JIJI LA TANGA ALIPOTEMBELEA BANDA LAO LILILOPO KWENYE MAONYESHO YA PILI YA KIMATAIFA YA BIASHARA YANAYOFANYIKA ENEO LA MWAHAKO JIJINI TANGA.

AFISA UHAMASISHAJI WANACHAMA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA(NHIF) VISTUS TILUSASILA KUSHOTO AKITOA ELIMU KUHUSU MFUKO HUO KWA MKAZI WA JIJI LA TANGA.
MWENYEKITI WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOANI TANGA,HASSANI HASHIM AKIMULIZA JAMBO MENEJA WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA(NHIF) ALLY MWAKABABU WAKATI ALIPOTEMBELEA BANDA LAO KUPIMA SUKARI NA PRESHA.
MENEJA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA(NHIF) ALLY MWAKABABU WA PILI KILIA AKIPIMWA NA NESI WAKATI WA MAONYESHO YA PILI YA KIMATAIFA YA BIASHARA YANAOFANYIKA KWENYE VIWANJA VYA MWAKIDILA JIJINI TANGA.

UPIMAJI WA WANANCHI UKIENDELEA KWENYE BANDA LA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA MKOANI TANGA


Picha kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

TBL GROUP YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA WA TUZO YA MZALISHAJI BORA WA MWAKA 2015

TBL1Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli akikabidhi tuzo  kwa mshindi  wa kwanza wa Tuzo ya Rais ya mzalishaji bora wa mwaka 2015, kwa  Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin  wakati wa hafla ya kutoa  tuzo kwa washindi iliyofanyika jijini katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam . Wengine ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Dk. Samwel Nyantahe ( wa pili kulia)  na kushoto ni Waziri wa Biashara ,Viwanda na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage.
TBL2Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na maofisa waandamizi wa kampuni wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
TBL3Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na maofisa waandamizi wa kampuni wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
TBL4Rais John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na watendaji wa makampuni ambayo yameshinda tuzo mbalimbali katika kipindi cha mwaka huu
TBL5Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin (wa nne mstari wa mbele kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa kampuni hiyo waliohudhuria hafla ya kukabidhiwa tuzo.
…………………………………………………………………………………………………………………
Kampuni ya  TBL Group imeibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya Rais ya mzalishaji bora kwa kipindi cha mwaka 2015,vilevile imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la uzalishaji wa vinywaji ambapo  imetunukiwa tuzo kwa ushindi huo.
Tuzo ya mzalishaji bora hutolewa na Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI na hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali imefanyika leo jijini Dar es salaam katika  hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo mgeni wa heshima aliyekabidhi tuzo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa John Magufuli.
Akiongea baada ya hafla  hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin,alisema ushindi huu ni zawadi kwa wafanyakazi wote wa kampuni  kwa kuwa jitihada za kila mmoja ndizo zimepelekea mafanikio haya kupatikana.
“Kwetu TBL Grop tunayo furaha kwa kushinda tuzo hizi tulizofanikiwa kuzinyakua siku ya leo,haya kwetu ni mafanikio makubwa na tumefurahi kuona mchango wa uwekezaji wetu unatambuliwa na tunaendelea kuwa washindi wa tuzo mbalimbali zinazotolewa na taasisi mbalimbali”.Alisema Jarrin.
Alisema TBL Group itaendelea kufanya uwekezaji zaidi nchini na kuchangia kukua kwa uchumi wa taifa ikiwemo kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza tatizo la ajira nchini ambapo mbali na kutoa ajira kwenye viwanda vyake na mtandao wa wafanyabiashara inaoshirikiana nao tayari imeanzisha miradi ya kuwasaidia wakulima ambayo tayari imeanza kuonyesha mafanikio kwa kubadilisha maisha ya wakulima kuwa bora.
“Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kufanya kazi kwa karibu na wawekezaji na nina imani tutaendelea kushirikiana ili kuweza kupata mafanikio zaidi katika siku za usoni”.Alisema.
Kampuni ya  TBL Group imeibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya Rais ya mzalishaji bora kwa kipindi cha mwaka 2015,vilevile imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la uzalishaji wa vinywaji ambapo  imetunukiwa tuzo kwa ushindi huo.
Tuzo ya mzalishaji bora hutolewa na Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI na hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali imefanyika leo jijini Dar es salaam katika  hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo mgeni wa heshima aliyekabidhi tuzo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa John Magufuli.
Akiongea baada ya hafla  hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin,alisema ushindi huu ni zawadi kwa wafanyakazi wote wa kampuni  kwa kuwa jitihada za kila mmoja ndizo zimepelekea mafanikio haya kupatikana.
“Kwetu TBL Grop tunayo furaha kwa kushinda tuzo hizi tulizofanikiwa kuzinyakua siku ya leo,haya kwetu ni mafanikio makubwa na tumefurahi kuona mchango wa uwekezaji wetu unatambuliwa na tunaendelea kuwa washindi wa tuzo mbalimbali zinazotolewa na taasisi mbalimbali”.Alisema Jarrin.
Alisema TBL Group itaendelea kufanya uwekezaji zaidi nchini na kuchangia kukua kwa uchumi wa taifa ikiwemo kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza tatizo la ajira nchini ambapo mbali na kutoa ajira kwenye viwanda vyake na mtandao wa wafanyabiashara inaoshirikiana nao tayari imeanzisha miradi ya kuwasaidia wakulima ambayo tayari imeanza kuonyesha mafanikio kwa kubadilisha maisha ya wakulima kuwa bora.
“Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kufanya kazi kwa karibu na wawekezaji na nina imani tutaendelea kushirikiana ili kuweza kupata mafanikio zaidi katika siku za usoni”.Alisema.