Mkuu
wilaya ya Iringa Richard Kasesela alitembelea maduka ya vijana
wajasiliamali waliofungua maduka ili kuweza kunyanyua maisha yao. vijana
hawa wamepata mikopo na kuweka maduka yao katika hadhi ya kimataifa.
Akizungumza nao Kasesela alifurahishwa sana na unadhifu wa maduka hayo
yaliyopo mtaa wa msikiti wa miyomboni. Kasesela hutumia jumapili
kutembelea wafanya biashara ndogondogo na wale wa sokoni ili
kuwahamasisha kukuza biashara zao na kuitangaza.
Maduka
haya yana wiki moja tuu toka yaanzishwe hayana tofauti na yale ambayo
ukienda nje ya nchi utayakuta. Wajasilia mali walialamikia wingi wa kodi
ndogo ndogo pia mazingira ya baishara bado si rafiki sana. Mkuu wa
wilaya aliahaidi kulifanyia kazi. ALITEMBELEA maduka ya fettilicious,
M8, Young D na mengineyo.
No comments:
Post a Comment