Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali, CAG Profesa Mussa Assad akizungumza na waandishi wafanyakazi ofisi hiyo wakati mkutano baraza jpya la wafanyakazi la wafanyakazi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora , Susan Mlay akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa ofisi ya CAG leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora , Susan Mlay akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa ofisi ya CAG leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
OFISI ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za serikali imeitaka serikali kuangalia upya vyanzo vyake vya mapato na matumizi ya fedha kwa sasa sio nzuri.
Akizungumza katika mkutano wa kwanza wa Baraza jipya la wafanyakazi wa ofisi hiyo, Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali, CAG Profesa Mussa Assad hiyo ni changamoto ambayo inapaswa kuangaliwa na kutafutiwa ufumbuzi na changamoto zinazoikabili ofisi yake, amesema kuchelewa kupokea mgao wa fedha za miradi ya maendeleo kwa wakati inasababisha ofisi hiyo kushindwa kutekeleza mipango na kukamilisha miradi husika kwa wakati.
Profesa Assaad amesema idadi ya watumishi iliyokuwepo katika ofisi yake ilikuwa 81 ikaongezeka hadi kufika 150 lakini bado wanahitaji watumishi wengine 129 wenye fani ya ukaguzi.
Aidha amesema kuwa kulingana na weledi wa wakaguzi hao Tanzania imeteuliwa kukaimu nafasi ya uenyekiti wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na China iliyomaliza muda wake mwaka 2014.
Nae Naibu Katibu Mkuu Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora , Susan mlay amesema watumishi wanatakiwa kuwa na weledi katika kufanya kazi ili kuleta tija kwa taifa ikiwa pamoja na kuangalia masilahi yetu kutokana na kazi wanazozifanya.
No comments:
Post a Comment