…………………………………………………………………………………………………………………
Kampuni ya TBL Group imeibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya Rais ya mzalishaji bora kwa kipindi cha mwaka 2015,vilevile imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la uzalishaji wa vinywaji ambapo imetunukiwa tuzo kwa ushindi huo.
Tuzo ya mzalishaji bora hutolewa na Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI na hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali imefanyika leo jijini Dar es salaam katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo mgeni wa heshima aliyekabidhi tuzo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa John Magufuli.
Akiongea baada ya hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin,alisema ushindi huu ni zawadi kwa wafanyakazi wote wa kampuni kwa kuwa jitihada za kila mmoja ndizo zimepelekea mafanikio haya kupatikana.
“Kwetu TBL Grop tunayo furaha kwa kushinda tuzo hizi tulizofanikiwa kuzinyakua siku ya leo,haya kwetu ni mafanikio makubwa na tumefurahi kuona mchango wa uwekezaji wetu unatambuliwa na tunaendelea kuwa washindi wa tuzo mbalimbali zinazotolewa na taasisi mbalimbali”.Alisema Jarrin.
Alisema TBL Group itaendelea kufanya uwekezaji zaidi nchini na kuchangia kukua kwa uchumi wa taifa ikiwemo kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza tatizo la ajira nchini ambapo mbali na kutoa ajira kwenye viwanda vyake na mtandao wa wafanyabiashara inaoshirikiana nao tayari imeanzisha miradi ya kuwasaidia wakulima ambayo tayari imeanza kuonyesha mafanikio kwa kubadilisha maisha ya wakulima kuwa bora.
“Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kufanya kazi kwa karibu na wawekezaji na nina imani tutaendelea kushirikiana ili kuweza kupata mafanikio zaidi katika siku za usoni”.Alisema.

No comments:
Post a Comment