Wednesday, 18 May 2016

KATIBU MKUU WIZARA YA MALIASILI NA UTALII MAJ. GEN. GAUDENCE MILANZI AONGOZA MKUTANO WA 23 WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA HIYO



Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza wakati akifungua Mkutano wa 23 wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika jana katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii, Jijini Dar es Salaam. 

Katika salamu zake amewataka watumishi wa Wizara hiyo kuhakikisha kuwa wanatimiza wajibu wao katika kutekeleza lengo kuu la Wizara ambalo ni kuendeleza uhifadhi wa Maliasili, Malikale na Kukuza Utalii nchini. 

Amewataka watumishi wote wa Wizara kuwa waadilifu, wabunifu, kufanya kazi kwa ushirikiano, kuepuka vitendo vya rushwa na makundi yasiyokuwa na tija kwa Wizara na Serikali kwa ujumla. 

Alionya kuwa, Mtumishi yeyote atakeenda kinyume cha sheria na taratibu hatosita kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kuachishwa kazi ili kwenda sambamba na kauli mbiu ya Serikali ya awamu ya tano ya "HAPA KAZI TU"

Maj. Gen. Milanzi alimuwakilisha Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ambaye yupo Mkoani Dodoma kwa ajili ya majukumu mengine ya Kiserikali (Bunge la bajeti).
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Maliasili na Utalii wakiimba wimbo wa kuashiria umoja wa wafanyakazi (Solidarity Forever). 
Sehemu ya wajumbe wa Mkutano huo.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi (katikati),  Naibu Katibu Mkuu Angelina Madete (kulia) na Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Maliasili na Utalii Wilfred Msemo (kushoto) wakiimba wimbo wa wafanyakazi wa "Solidarity Forever" wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 23 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika jana tarehe 17 Mei, 2016 katika ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii, tawi la Bustani, Jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano huo wakiimba wimbo wa umoja wa wafanyakazi "Solidarity Forever"(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Maliasili na Utalii)

No comments:

Post a Comment