Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani ambayo ni kampuni mama ya Murhandziwa Profesa Bongani Aug Khumalo,akitoa maelekezo ya mchezo huo kwa waandfishi wa habari na wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kuuza tiketi, (kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini Abbas Tarimba na katikati ni Meneja mradi wa Kampuni hiyo,Brett Smith.Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya Michezo ya Michezo ya kubahatisha nchini Abbas Tarimba akijaribu mashine za michezo zinavyofanya kazi
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Gidani wakisikiza kwa makini maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya Michezo ya kubahatisha,Abbas Tarimba (hayuko pichani) muda mfupi baada ya hafla ya uzinduzi wa kuuza tiketi.
-Mshindi wa kitita cha milioni 100 kujulikana Jumamosi
Kampuni ya Murhandziwa Limited ya Afrika ya Kusini ambayo imepewa leseni ya kuendesha Bahati Nasibu ya Taifa leo imeanza kuuza tiketi nchini kote na droo ya kwanza ya mchezo huo itafanyika jumamosi ya wiki ijayo ambayo mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 100.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa kuuza tiketi jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania,Abbas Tarimba amesema kuwa wakati umefika kwa watanzania kushiriki bahati nasibu inayoendeshwa kitaalamu na inayowezesha washindi kujishindia donge nono na kubadilisha maisha yao.
“Zawadi ya milioni 100 sio ndogo itasaidia kubadilisha maisha ya mshindi pia zitatolewa zawadi mbalimbali na serikali inategemea kupata mapato kwa njia ya kodi Zaidi ya dola milioni 40 kwa mwaka kutokana na uwekezaji huu katika sekta hii na aliwataka watanzania wachangamkie kununua tiketi na kushiriki katika mchezo huu.
Mwenyekiti wa kampuni ya Gidani ambayo ni kampuni mama ya Murhandizwa Limited,Profesa Bongani Aug Khumalo alisema kuwa watanzania wategemee kuona michezo ya kubahatisha ikiendeshwa kitaalamu na kubadilisha maisha ya washindi kutokana na zawadi nono watakazopata washindi.
“Tiketi za Bahati nasibu hii zitauzwa kwa shilingi 500 na zitapatikana kwa mawakala waliosambaa nchini kote na kwa njia ya mtandao na washitiki wa mchezo huu wa Bahati Nasibu ya Taifa wanatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea,vilevile droo nyingine za mchezo zitakuwa zikifanyika kila siku ya Jumatano na Jumamosi na kuwezesha wananchi wengi kushinda”Alisema.
Alisema mbali na mchezo huu kuwanufaisha washindi binafsi utawawezesha watanzania wengi kupata ajira Zaidi ya 1,000 za moja kwa moja na zisijo za moja kwa moja ambapomkwa sasa imeajiri watanzania 40 na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu inatarajia kuwa imeajiri wafanyakazi Zaidi ya 1,000.
No comments:
Post a Comment