Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kamba kuashiria uzinduzi wa gari la matangazo ya Kampeni ya kupambana na Rushwa ya LONGA NASI kwa kupiga namba 113 na kutuma kutuma sms kwenda namba 113 ili kutoa taarifa ya kutoa au kupokea Rushwa kwa TAKUKURU.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye uzinduzi wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za watu wanaotoa rushwa au kupokea rushwa kwaajili ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113 unayoweza kupiga na kutuma sms za kawaida Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Tehama TAKUKURU, Neema Mwalyelye akitoa maelekezo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipotembelea kwenye banda la kitengo cha Tehama wakati wa uzinduzi wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za watu wanaotoa rushwa au kupokea rushwa iliyofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Mkurugenzi wa elimu kwa umma TAKUKURU, Stela mpanju akizungumza kabla ya kuzindua wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za vitendo vya Rushwa au maoni ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113 kupiga au kutuma sms ya kawaida bila gharama yeyote. Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valontino Mlowola akizungumza kabla ya kuzindua wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za vitendo vya Rushwa au maoni ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113 kupiga au kutuma sms ya kawaida bila gharama yeyote. Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA KAMPENI YA LONGA NASI LEO
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akihutubia kwenye uzinduzi wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema
au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za vitendo vya Rushwa au maoni ya
kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana
pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113. Uzinduzi
huo umefanyika leo Mei 24,2016 katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke
jijini Dar es salaam.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki kabla ya kuzindua
mpango wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU
kwa kutoa Taarifa za vitendo vya Rushwa au maoni ya kuboresha mapambano
dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa
matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113. Uzinduzi huo umefanyika leo
Mei 24,2016 katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiangalia mpango wa utekelezaji wa TAKUKURU kwenye uzinduzi wa kampeni
ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa
za vitendo vya Rushwa au maoni ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa
ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya
simu ya Dharura ya 113. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 24,2016 katika
viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam. Kushoto Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Angela Kairuki, kushoto Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valontino Mlowola.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akivuta kamba kuondoa kitambaa kuzindua mpango wa kampeni ya LONGA NASI
inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za vitendo vya
Rushwa au maoni ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi
huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura
ya 113. Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 24,2016 katika viwanja vya
Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam. Kushoto Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela
Kairuki, kushoto Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valontino Mlowola.
Makamu wa
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi
ya Kuzuwia na kupambana na Rushwa Nchini TAKUKURU Valontino Mlowola
baada ya kuzindua mpango wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au
ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za vitendo vya Rushwa au maoni ya
kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana
pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113. Uzinduzi
huo umefanyika leo Mei 24,2016 katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke
jijini Dar es salaam. (Picha na OMR).
SERIKALI KUZITAMBUA NA KUZIRASIMISHA BANDARI BUBU ZILIZOKIDHI VIGEZO.
Na.Aron Msigwa - MAELEZO
24/5/2016.DODOMA.
Serikali
imesema kuwa inaendelea na utaratibu wa kuzitambua na kuzirasimisha
bandari Bubu zote zilizokidhi vigezo ambazo zinatumiwa na
wafanyabiashara kupitisha bidhaa mbalimbali ili ziweze kuchangia katika
Pato la Taifa kulingana na wingi wa bidhaa zinazopitishwa katika
bandari hizo.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani ametoa
kauli hiyo bungeni mjini Dodoma leo wakati akijibu maswali ya Wabunge
waliotaka kujua mkakati wa Serikali katika kudhibiti bidhaa
zinazoingizwa nchini na wafanyabiashara wasio waaminifu kupitia bandari
bubu hali inayoikosesha serikali mapato.
Mhe.
Ngonyani amekiri kuwepo kwa ongezeko la wafanyabiashara wasio waaminifu
wanaotumia bandari hizo katika maeneo mbalimbali nchini hasa ukanda wa
Pwani wa Bahari ya Hindi, Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria na maeneo ya
mipakani ambayo yanaingia moja kwa moja kwenye makazi ya watu akieleza
kuwa wengi wa wafanyabiashara wanakwepa kodi na kutafuta urahisi wa
kupitisha mizigo yao.
Amesema
maeneo hayo yamekuwa chanzo kikubwa cha upitishaji wa bidhaa
zisizokidhi viwango, Silaha na Biashara haramu na kubainisha kuwa baadhi
ya wafanyabiashara wa ndani wasio waaminifu wamekuwa wakishirikiana na
raia wa kigeni kuagiza na kuingiza bidhaa hizo kupitia bandari hizo kwa
lengo la kukwepa kodi.
Amesisitiza
kuwa Serikali ya Awamu ya tano inalishughulikia kwa nguvu zote suala
hilo kupitia watendaji wake wakiwemo wakuu wa mikoa wa maeneo husika
ambao hushirikiana na mamlaka zinazohusika vikiwemo vyombo vya ulinzi na
usalama kudhibiti njia na maeneo yote yanayotumiwa na wafanyabiashara
hao.
" Kama
Serikali tunaendelea kufanya vikao kwa kushirikiana na wakuu wa mikoa
na mamlaka zinazohusika kuangalia namna ya kurasimisha bandari bubu
zilizobaki ili tuweze kukusanya mapato ya Serikali yaliyokuwa yakipotea
kutokana na wingi wa mizigo inayopitishwa" Amesema Mhandisi Ngonyani.
Amefafanua
kuwa mwaka katika kipindi cha mwaka 2015 na mwezi Januari, 2016, doria
zilizofanyika katika maeneo yanayotumiwa na wafanyabishara hao
zilifanikisha kukamatwa kwa wafanyabiashara 98 ambao wote walichukuliwa
hatua za kisheria ikiwem mali zao kutaifishwa pamoja na kuwafikisha
mahakamani.
Kuhusu
bandari bubu zilizotambuliwa na kuzirasimishwa na Serikali katika
Pwani ya Bahari ya Hindi ni Mbweni ya jijini Dar es salaam, Mlingotini
mkoani Pwani, Kisiju na Nyamisati mkoa wa Pwani na Bandari bubu ya
Kilambo mkoani Mtwara.Aidha, amesema Serikali inaendelea na utaratibu wa
kurasimisha bandari binafsi umefanyika katika ziwa Victoria mkoani
Mwanza na maeneo mengine ambayo serikali inaendelea kuyafanyia kazi.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Masauni
amesema kuwa Serikali inaendelea kuvijengengea uwezo vikosi vyake vya
ulinzi na usalama kwa kuviongezea vifaa vya kisasa ili viweze kuimarisha
doria nchi nzima ili kukabiliana na vitendo vyote vya uvunjaji wa
sheria.
Amesema
Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na wananchi kukusanya taarifa
za kiharifu ili kuwabaini na kuwakamata wafanyabishara wote
wanaojihusisha na uagizaji na uingizaji wa bidhaa kupitia bandari bubu
ambaoumekua ukiisababishia serikali ikose mapato.
"
Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinaendelea kukusanya taarifa za
kiharifu kutoka kwa wananchi ili kukabiliana na wimbi hili, pia
tunaendelea kuviongezea nguvu vikosi vyetu vya ulinzi na usalama ili
viweze kutimiza majukumu yao ipasavyo" Amesisitiza Mhe.Masauni.
No comments:
Post a Comment