Monday, 23 May 2016

TAARIFA YA KIPINDUPINDU




JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


TAMKO KUHUSU MWENENDO WA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NCHINILILILOTOLEWA NA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRWA AFYA, MAENDELEO YAJAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTOTAREHE 23 MEI,  2016.


Ndugwanahabari,

Serikali kupitia Wizara yangu inaendelea na utaratibu wa kutoa taarifa ya mwenendwmlipuko waugonjwa wa Kipindupindu nchini kila wiki kama tulivyoahidi. Takwimu za ugonjwa huu zinaonyesha kuwa hadi kufikia tarehe 22 Mei 2016, kulikuwa na jumla ya wagonjwa 21,585  ambao wametolewa taarifa ya kuwa na ugonjwa huu, na kati ya hao, ndugu zetu 338 wamepoteza maisha.

Tumefarijika kuona takwimu za wiki iliyopita kuanzia tarehe 16 hadi 22 Mei 2016 zinazoonyesha kuwa, kasi ya ugonjwa wa kipindupindu imepungua kwa asilimia 49 (karibu nusu ya wagonjwa), ambapo idadi ya wagonjwa wapya walioripotiwa ni 108, na hakuna aliyepoteza maisha, ikilinganishwa na wagonjwa wapya212 walioripotiwa wiki iliyotangulia ya Mei 9 hadi 15.

Mikoa ambayo imeripoti wagonjwa wiki hii ni Morogoro (47), Manyara(16), Lindi (14), Mara (11) Dar es Salaam (9), Pwani (6), Kagera (2), Kilimanjaro (2) na Iringa (1).

Halmashauri zilizoongoza kutoa wagonjwa wengi ni Kilosa (27),  Mvomero (15), Kilwa (14), Tarime Mjini (11), Babati Vijijini (10), Kinondoni (9), Babati Mjini (5), Morogoro Mjini (5), Kibaha Mjini (4), Bukoba Mjini (2), Chalinze (2), Same (2), Iringa Mjini (1) na Mbulu (1).

Katika wiki iliyopita, mikoa ambayo haikuwa na wagonjwa wa kipindupindu ni Kigoma, Dodoma, Mwanza, Geita, Singida, Shinyanga, Arusha, Tanga, Tabora, Rukwa, Katavi, Mbeya, Simiyu na Mtwara. Na mikoa ambayo haijawahi kuripoti mgonjwa wa kipindupindu tangu mlipuko uanze ni Ruvuma na Njombe

Ndugu wanahabari,
Kupungua kwa idadi ya wagonjwa kusirudishe nyuma juhudi za kuuzuia ugonjwa huu, bali tunatakiwa kuzidisha jitihada ili tuweze kuuondoa, tusiwe na wagonjwa kabisa. Ni vema kuchukua tahadhari zaidi, hasa katika msimu wa masika, ambapo kuna uwezekano mkubwa wa maji ya mvua kusambaza vimelea vya ugonjwa huu. Tuendelee kuzuia maambukizi, na pia kuendelea kutoa taarifa za ugonjwa kila siku, hata kama hakuna wagonjwa, na kusimamia kikamilifu hatua mbalimbali za udhibiti wa mlipuko huo.

Ndugu wanahabari,

Wizara inaendelea kutoa rai kwa wananchi wote kuzingatia kanuni za usafi binafsi na usafi wamazingira. Aidha Wizara inatoa elimu ya afya kwa njia ya kupiga simu kupitia namba 117 na kwa njia ya kutuma ujumbe wenye neno KIPINDUPINDU kwenda 15774. Huduma hizi zinatolewa bila malipo kupitia mitandao yote.

No comments:

Post a Comment