MKUU wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amewaomba msamaha wapinzani wao, Simba na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Hajji Manara.
Kauli hiyo, aliitoa jana ambapo alisema amefuta majina yote aliyokuwa akiwaita Simba kama vile; Wazee wa Mchangani, Wazee wa Youtong, Wahapahapa, Chura na Wamatopeni baada ya Ligi Kuu Bara kumalizika na wao kutwaa taji hilo la ubingwa.
Muro alisema alifikia hatua hiyo kwa ajili ya kulinda ajira yake inayomruhusu kuongea chochote ilimradi asitukane.
Aliongeza kuwa, hayo maneno hayo yalikuwa ni chagizo na hayakulenga kumtukana wala kumkwaza mtu yeyote zaidi ni kuleta changamoto na ushindani.
“Naomba nichukue nafasi hii kuwaomba msamaha mashabiki wote wa Simba, pia rafiki yangu Manara kwa maneno na majina ya utani niliyokuwa nawaita wakati ligi kuu ikiwa inaendelea.
“Naomba nitangaze rasmi majina hayo sitawaita tena baada ya ligi kuu kumalizika.
“Pia ningependa kuwaaga akina Manara, Bwire (Masau) na Kifaru (Thobias) kuwa mimi hivi sasa ni wakimataifa, siyo levo yao tena ninakwenda kupambana na akina TP Mazembe timu nyingine tunazoshiriki nao Kombe la Shirikisho,” alisema Muro.
No comments:
Post a Comment