SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) yazidi kutoa elimu juu ya hifahdi ya jamii kwa wananchi mbalimbali ikiwa ni mpango maalamu wa kuwafikia wanachama wengi zaidi.
Katika mkoa wa Arusha NSSF imetoa elimu kwa wafanyabiashara wadogowadogo katika soko la Kilombero. Zoezi hilo litaendelea kesho tarehe 19/05 katika eneo la soko la Kilombero.
Wananchi wakiwa katika foleni ya kujiandikisha uanchama wa NSSF wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi iliyofanyika katika Soko la Kilombero jijini Arusha.
Afisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Amani Marcel (kushoto), akimkabidhi mwanachama mpya fulana wakati wa Kampeni maalumu ya kuwafikia wanachama wengi zaidi iliyofanyika katika Soko la Kilombero Jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment