Monday, 23 May 2016

TANZIA: RAS BUPE BAKWERESA KARUDI AFARIKI DUNIA



Na Sultani Kipingo

Habari za uhakika na kusikitisha zimetufikia kuwa mwanaharakati Ras Bupe Bakweresa Karudi, maarufu pia  kama kaka Bupe Mkushi (pichani kushoto), amefariki dunia katika hosptali ya Taifa Muhimbili baada ya kupata ajali ya gari.

Ras Bupe ameacha mke na watoto. Mke na mtoto wake wa kiume wameshawasili nchini kutokea Uingereza. Msiba hupo Karakata jijini Dar-es-salaam. Marehemu Ras Bupe Bakweresa Karudi alikuja nchini Tanzania katikati mwa miaka ya 70 akifuatana na mkewe na watoto wawili Kiyenda(msichana) na Nyamiche mvulana. Ras Bupe Karudi alikuja kumuomba marehemu baba wa taifa mwalimu Nyerere hili atoe idhini kwa watu weusi wa visiwa vya Karibian vya Jamaica warudi Afrika (Tanzania) kama nyumbani kwani ndio asili yao.

Baada ya kukubaliwa maombi yake, Marehemu Bupe akaungana na wanaharakati wenziwe hapa nchini wakiwemo marehem Prof. Joshua Mkhululi aka Prof. Keneth Edward, Marehem Ras Kwetenge Zanaki Sokoni (Wa Jamaica) pamoja na  wengine ambao wapo hai Imani Mani wakaungana na wenyeji wao Said Jazbo Vuai, Isza Suleiman na Ebrahim Makunja au Kamanda Ras Makunja kiongozi ambapo wakasajili chama cha ushirika chenye jina la UHURU, UMOJA NA MAENDELEO chenye makao kule Mbezi Beach jijini Dar es salaam wakiwa wanajishughulisha na mipango ya kilimo na kumiliki maroli ya usafirishaji. 

Marehem Kaka Ras Bupe atakumbukwa sana kwa harakati zake zake za kuupigania uafrika na kuwahamasisha raia wenye asili ya kiafrika kurudi Tanzania.

Mungu mlaze pema peponi marehemu 
Bupe Bwakweresa Karudi 
Amen

No comments:

Post a Comment