MUZIKI wa kizazi kipya maarufu kama ‘Bongo Flava’ ulikuwa haujulikani na pia haukuonekana kama ni sanaa halisi ya muziki; hivi ndivyo ambavyo vizazi vilivyotanguliwa vlivyoutazama takribani miongo miwili iliyopita japo ni muziki wa kuburudisha watu wa rika zote wadogo kwa wakubwa.
Muziki wa ‘Bongo Flava’ umebadilisha himaya ya muziki hapa Tanzania ambao umepata sifa katika nchi za Afrika mashariki, Afrika na Ulaya.
Ni ukweli usiofichika kuwa, sekta ya muziki wa kizazi kipya imekuwa kwa kasi na hata kuwapatia ajira vijana wengi wa kitanzania wenye vipaji ambao walikuwa hawana kazi hapa nchini kufuatia tatizo la ajira ambalo limekuwa ni changamoto kwa vijana.
Ingawaje fani ya muziki imwekuwa ikionekana kuwa na maendeleo yanayosuasua kwa kipindi cha muongo mmoja hivi, wasanii wa muziki bado wanakumbana na changamoto nyingi.
Wameeleza changamoto hizo kuwa ni mapungufu ya kuwezeshwa kitaifa na kimataifa na kuwepo kwa ujuzi mdogo miongoni mwa wanamuziki.
Kuna baadhi ya makampuni, mashirika na hata watu binafsi ambao wameona umuhimu wa kutatua matatizo kama haya yanayowakabili wasanii na wanamuziki hapa nchini, na badala yake wamegundua mikakati ya kuwawezesha ili kutimiza malengo na ndoto zao kwa ujumla.
Tigo Tanzania ni moja ya makampuni hayo, na kwa kuwa ni kampuni ya kidijitali inayobadili maisha ya
watumiaji mtandao wake, kampuni hii ilianzisha jukwaa la wanamuziki wa kizazi kipya ijilikanayo kama ‘Tigo Music Platform’
ambayo inalengo la kuwawezesha wasanii wa muziki hapa nchini na kufanya kazi zao zijulikane ndani na nje ya nchi.
watumiaji mtandao wake, kampuni hii ilianzisha jukwaa la wanamuziki wa kizazi kipya ijilikanayo kama ‘Tigo Music Platform’
ambayo inalengo la kuwawezesha wasanii wa muziki hapa nchini na kufanya kazi zao zijulikane ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment