Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiangalia Matairi ya Magari aina ya BF Goodrich KO2 yanayosambazwa na
kampuni ya Superdoll baada kuwasili katika kituo cha kisasa cha huduma
za magari na Matairi cha Superdoll mjini Arusha kwa ajili ya kuzindua rasmi kituo hicho. Kusshoto Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akibonyeza kitufe na kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa
Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif alipokua akizindua rasmi kituo cha
kisasa cha huduma za magari pamoja na Matairi cha Superdoll mjini
Arusha.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Superdoll Seif Ali Seif
baada ya kuzindua rasmi kituo cha kisasa cha huduma za magari pamoja na
Matairi cha Superdoll mjini Arusha.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Mhe. Said Meck Saddik
alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya
kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Arusha, baada ya kukamilisha
zira yake ya kikazi katika Mikoa ya Mwanza na Geita. Katikati Mkuu wa
Mkoa Arusha Mhe. Daud Felix Ntibenda.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na Viongozi na Makamanda wa Kamati za Ulinzi na Usalama za
Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani
Arusha, baada ya kukamilisha zira yake ya kikazi katika Mikoa ya Mwanza
na Geita.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiangalia Vikundi vya Ngoma za aina mbalimbali alipowasili Uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya
siku tatu Mkoani Arusha, baada ya kukamilisha zira yake ya kikazi
katika Mikoa ya Mwanza na Geita.
(Picha na OMR)
No comments:
Post a Comment