Baadhi ya madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, (MNH), wakipiga makofi wakati wa mkutano wao na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Profesa Museru kwenye ukumbi wa CPL wa Hospitali hiyo jijini, Dar es Salaam Juni 22, 2016.
(PICHA ZOTE NA JOHN STEPHEN WA MNH).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akizungumza kwenye mkutano huo
NA NEEMA MWANGOMO, MNH
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru amekutana na Madaktari wa MNH ikiwa ni mkakati wa kukutana na watumishi kwa lengo la kuwasikiliza na kujibu kero zao.
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa CPL uliopo ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Museru amewapongeza madaktari hao kwa kufanya kazi kwa bidii na kuimarisha utoaji huduma kwa wagonjwa na kwamba hali hiyo imechangia MNH kuongeza mapato yake.
Amesema kuongezeka kwa mapato ya Hospitali na kufikia Sh. bilioni 4. 5 kwa mwezi kumetokana na kila mmoja kutimiza wajibu wake.
Amesema kutokana na mafanikio hayo, MNH imewaongezea madaktari wake posho mbalimbali ili kuongeza tija katika utendaji, lakini pia hospitali imeamua kutenga Shilingi Milioni 800 kwa mwaka ili kuwapa mkono wa heri wastaafu wake jambo ambalo awali halikuwapo.
Hata hivyo amesema mbali na hatua hiyo, pia MNH imefanikiwa kulipa malimbikizo mbalimbali ya stahiki za wafanyakazi wake ikiwamo pesa za likizo kwa madaktari pamoja na watumishi wengine kwa ujumla.
“ Awali changamoto kubwa ilikuwa ni ucheleweshaji wa stahiki za wafanyakazi kwa Madaktari na watumishi wengine, lakini katika hilo tumefanikiwa kwani tunaenda nalo vizuri na tumelipa malimbikizo hayo “ amesema Profesa Museru.
Akielezea mipango ya MNH Profesa Museru amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili ina mipango mbalimbali ya kuendelea kuboresha huduma zake ikiwemo kuongeza vitanda vya Chumba ya wagonjwa Mahututi-ICU-, kuongeza ICU ya watoto pamoja na kina Mama wajawazito.
Kaimu Mkurugenzi huyo Mtendaji wa MNH leo Juni 23, 2016 atakutana na Wauguzi pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii.
Baadhi ya madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, (MNH), wakipiga makofi wakati wa mkutano
Baadhi ya madaktari bingwa wakimsikiliza Profesa Museru wakati wa mkutano huo
Dk Saidia Primos wa hospitali hiyo akiuliza swali kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi wa Fedha, Gerald Kimambo (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk John Kimario kwenye mkutano huo
Dk Moa akiuliza swali baada ya kupewa nafasi kwenye mkutano huo
No comments:
Post a Comment