
Uzinduzi wa jukwaa hilo utafanyika sambamba na uzinduzi wa Akaunti ya Malaika kwa ajili ya kuwafungulia akaunti wanawake wajasiriamali wadogo wa hapa nchini.
Hafla hiyo inategemewa kuhudhuriwa na watu wapatao 1,000 kutoka makundi ya wadau mbalimbali wakiwemo wanawake wajasiriamali wa Tanzania Bara na Visiwani.
Jukwaa hilo litatoa uelewa kwa washiriki hususan kuhusu fursa zilizopo na mikakati ya kumuwezesha mwanamke kiuchumi pamoja na juhudi zinazofanywa na serikali katika harakati za kuinua wanawake kiuchumi.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
No comments:
Post a Comment