Waziri wa Kazi, Usafiri na Mawasiliano Mh. Makame Mbarawa akiongea na wadau mbali mbali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizopo kusini mwa Afrika (SADC) hawap[o pichani katika ufunguzi wa mkutano wa 19 wa kamati ya SADC usafiri wa anga uliofanyika jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………………………….
Na Ally Daud-Maelezo
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi zilizopo kusini mwa Afrika (SADC) imeadhimia kuimarisha usafiri wa anga ili luleta huduma bora na kuwapa amani wananchi wanaotumia usafari wa anga katika Jumuiya hiyo.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Makame Mbarawa alipokuwa akifungua Mkutano wa 19 wa Kamati ya SADC ya usafiri wa Anga uliofanyika jijini Dar es salaam.
“Mkutano huu unalenga kuadhimia kuimarisha usalama wa anga katika nchi za Jumuiya ya SADC, kwa kuwa unahitajika sana kwa wananchi ili kuongeza shughuli za kiuchumi na kijamii na kuleta maendeleo ya nchi wanachama” alisema Mbarawa
Ameongeza kuwa “ni lazima tuadhimie mambo yatayoleta maendeleo na huduma bora katika usafiri wa anga kwa jumuiya ya SADC ili kujenga uhusiano na malengo yaliyo bora kwa maendeleo ya nchi zetu.”
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Bwana Hamza Johari amesema kuwa mkutano huo unalenga kuhakikisha wanafikia na kutekeleza malengo Jumuiya ya usafiri wa anga wa kimataifa (ICAO) katika kuboresha huduma za usafiri huo.
“Ni lazima tuyafanyiekazi maadhimio ya mkutano huu ili kuboresha huduma kwa kiwango cha kimataifa pamoja na kuleta unafuu kwa watumiaji wa usafiri wa anga” alisisitiza Bw. Johari.
Naye, Mwenyekiti wa SADC Bw. Geoffrey Moshabesha amesema kuwa kamati hiyo inajipanga kuunda taasisi ya kiusalama ili kusimamia mifumo yote kwa nchi nzima ili kuweka mazingira mazuri kwa watumiaji wa usafiri wa anga.
Jumuiya ya SADC imeweka mikakati ya kutekeleza maadhimio hayo katika kuleta usalama wa anga pamoja na kutunza mazingira ili kuboresha huduma kwa watumiaji wa usafiri wa anga kwa nchi wanachama.
No comments:
Post a Comment