Tuesday, 7 June 2016

SAMATTA AHIDI KUJENGA KITUO MAALUM NCHINI CHA KUIBUA NA KUKUZA VIPAJI VYA WANASOKA WACHANGA



Familia ya mchezaji bora Afrika, Mbwana Samatta wakiwa katika picha ya pamoja katika eneo alilikabidhiwa mchezaji huyo kwa ajili ya kujenga kituo cha michezo katika kijiji cha Mwanzega, MKuranga juzi. wa Kwanza kulia ni kaka yake Mbwana, omari, wa tatu ni baba yake mzani na mama yake mlezi.


NAHODHA wa  Timu  ya Soka ya Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Ali Samatta ameahidi  kujenga kituo maalum nchini cha kuibua na kukuza vipaji vya wanasoka wachanga ili wafikie viwango vya kimataifa.

Sambamba na  hilo, ameweka azma  ya kukifanya kituo  chake kuwa na wigo mpana wa kuwawezesha vijana wa  kutoka nje ya  Tanzania kuja  kujifunza  soka katika kituo  hicho na kuwapeleka vijana wawili kila mwaka kwenda kujifunza zaidi mchezo huonchini Ubelgiji.

Hayo  yamebainishwa  na baba wa mwanasoka  huyo wa kimataifa, Ali Samtta alipozungumza kwa niaba ya  mwanae, katika halfa ya kukabidhiwa  ekari tano  za eneo la ujenzi wa kituo hicho kulikofanywa na Mtandao wa Wasanii na Wanamichezo  nchini, (SHIWATA.).

Hafla ya makabidhiano  hayo yaliyofanyika juzi katika kijiji  cha wasanii kilichopo Mwenzanga, wilayani Mkuranga.

Akizungumza  kwa niaba ya mwanae, baba wa  nyota  huyo alisema, azma ya Samatta (Mbwana) ni kujenga kituo kikibwa  cha kimataifa ambacho, moja ya madhumuni ni kuendelea kuwaibua na kuwakuza akina 'Samatta'  wengine wajao.

Alisema,  Salamu alizoziacha Mbwana kwa wasanii kwanza ni kuishukuru SHIWATA kwa hatua ya kutambua mchango wake kitaifa, hivyo, katika kulipa fadhila ni kujenga uwanja utakaokuwa na hadhi ya kimataifa kwa taifa.

"Niliongea na Mbwana  amenituma niwakilishe salamu zake kwa kwanza kwa  kuishukuru SHIWATA na kisha kueleza nia yake ya kutaka kuendelea kuibua  vipaji  vya  soka la vijana kupitia kituo kitakachojengwa hapa katika kijiji cha wasanii Mwenzange" alisema Ali Samatta na kuongeza. 

"Engekuwapo  hapa  leo, lakini alilazimika kusafiri mara tu baada ya kumalizika kwa mechi ya Stars dhidi ya Misri, kurejea  Ubelgiji kwa wito wa  haraka, lakini anatarajia kurejea  tena nchini kwa mapumziko, na mimi amenituma nimwakilishe kwa kauli zake hizi"

Katika  hatua nyingine, mwakilishi wa mgeni rasmi, Nape Mnauye, Bi Leah Kihindi aliipongeza SHIWATA kwa hatua yake ya kuwawekea misingi wanachama wake ili wawe na makazi ya kudumu kupitia kijiji hicho.

Sambamba na hilo, alilipongeza shirikisho  hilo kwa kutambua mchango wa Mbwana Samatta katika  soka ambako katika sherehe hizo wanachama 35 walikabidhiwa nyumba na misingi ya kujenga nyumba.


Mwenyekiti wa SHIWATA< Cassim Taalib akiwatoa taarifa fupi ya kijiji hicho alisema lengo ni kuwasaidia wasanii, wanamichezo na waandishi wa habari kujenga nyumba za kuishi ili kujiandaa kwa ajili ya kuishi maisha ya taabu baada ya kustaafu kazi zao.

SHIWATA inayomiliki ekari 300 za makazi katika kijiji hicho jumla ya wanachama 185 wamnejenga nyumba kwa njia ya kuchangishana.

No comments:

Post a Comment