Saturday, 11 June 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA JAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI PAMOJA NA JAJI KIONGOZI, PIA AAGANA NA BALOZI WA OMAN ANAYEMALIZA MUDA WAKE HAPA NCHINI. Friday, June 10, 2016 Maoni: 0 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Shaaban Ali Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Jaji Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Shaaban Ali Lila(kushoto) pamoja na Jaji kiongozi Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali, wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othmani mara baada ya tukio la uapisho wa Majaji hao Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Shaaban Ali Lila(kushoto) pamoja na Jaji kiongozi Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali, wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othmani pamoja na Majaji mbalimbali wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Oman hapa nchini Soud Al Ruqaishi ambaye anamaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA. UPINZANI WAUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ZA KUBANA MATUMIZI Friday, June 10, 2016 Maoni: 0 Mbunge wa Momba (CHADEMA), David Silinde akizungumza na waandishi wa habari kuelezea msimamo wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuhusu bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2016/17. Katikati ni Mbunge wa Vunjo, James Mbatia na Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Riziki Mngwali. Mbunge wa Vunjo (NCCR- Mageuzi), James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari kuelezea msimamo wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuhusu bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2016/17. Kushoto ni Mbunge wa Momba (CHADEMA), David Silinde na Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Riziki Mngwali.(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO) Na Jonas Kamaleki-MaelezoDodoma KAMBI rasmi ya Upinzani Bungeni imemuunga mkono Rais, Dkt. John Pombe Magufuli katika juhudi zake za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza fedha hizo katika miradi ya maendeleo na huduma za jamii kama ujenzi wa miundombinu ya barabara na reli. Pongezi hizo zimetolewa leo mjini Dodoma na Mbunge wa Momba (CHADEMA), David Silinde wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2016/17. “Tunamuunga mkono Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa kuondoa posho za vikao (Sitting Allowances) na tunamwomba aondoe posho hizo kwa wabunge nao watumie mishahara yao ili kuwe na usawa,” alisema Silinde. Silinde alisema kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani inaunga mkono juhudi za Mhe Rais Magufuli za kukusanya kodi ambayo inabidi ielekezwe kwenye miradi ya maendeleo na huduma za kijamii. “Tunaungana na Serikali kukata kodi kwenye kiinua mgongo cha wabunge lakini tunamuomba Mheshimiwa Rais apanue wigo wa kodi hiyo hadi kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya,” alisema Silinde. Kwa upande wake, mbunge wa Jimbo la Vunjo (NCCR-Mageuzi), Mhe. James Mbatia amesema kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani inamuomba Mhe. Rais Magufuli kufuta posho za vikao kwa wabunge haraka ili kuleta usawa kwa watanzania wote. WATANZANIA WAOMBWA KUSHIRIKI SIKU YA MTOTO WA AFRIKA. Friday, June 10, 2016 Maoni: 0 Lilian Lundo – MAELEZO Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewataka watanzania kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa Juni 16, kila mwaka. Kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Sihaba Nkinga imeeleza kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kuwa na siku maalum ya kuelimisha na kuwakumbusha wazazi, walezi na wadau mbalimbali kuitikia utekelezaji wa wajibu na majukumu yao katika kuwapatia watoto haki zao za msingi. “Tarehe 16 Juni ya kila mwaka, ni kilele cha maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika, katika siku hii, Tanzania inaungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Afrika kuadhimisha siku hii kwa mujibu wa Azimio lililopitishwa na nchi 51 za Umoja huo mwaka 1990,” imefafanua taarifa hiyo. Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa Azimio hilo lilipitishwa kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya watoto wa shule yaliyofanyika katika kitongoji cha Soweto, Afrika ya Kusini Juni 16, 1976, ambapo watoto wapatao 2,000 waliuawa kikatili na Makaburu wakiwa katika harakati za kutetea haki zao za msingi za kutobaguliwa kutokana na rangi yao. Katika siku hiyo watoto hupata nafasi maalum ya kujieleza, kusikilizwa, kushirikina kuonyesha vipaji vyao mbele ya wazazi, walezi na jamii kwa ujumla. Watoto wanahaki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa, kushiriki na kutobaguliwa Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni “Ubakaji na Ulawiti kwa Watoto Vinaepukika: Chukua Hatua Kumlinda Mtoto.” MAADHIMISHO YA SIKU YA WACHANGIA DAMU DUNIANI KUFANYIKA KITAIFA MKOANI DODOMA Friday, June 10, 2016 Maoni: 0 . Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya wachangia damu duniani yanayotarajia kufanyika tarehe 14 Juni mwaka huu. Maadhimisho hayo kitaifa yanatarajia kufanyika mkoani Dodoma. Kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Mapngo wa Taifa wa damu salama, Dkt. Abdu Juma. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya siku ya wachangia damu duniani yanayotarajia kufanyika tarehe 14 Juni mwaka huu. Maadhimisho hayo kitaifa yanatarajia kufanyika mkoani Dodoma. Kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Mapngo wa Taifa wa damu salama, Dkt. Abdu Juma na kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Caroline Damian.(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO) NIDA YAANZA KUTOA VITAMBULISHO VYENYE SAINI Friday, June 10, 2016 Maoni: 0 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bi. Rose Mdami akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu zoezi la utoaji wa vitambulisho vipya vyenye saini ya mwenye kitambulisho. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji Vitambulisho Bw. Alphonce Malibicha na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mifumo ya Kompyuta Bw. Mohamed Khamis. Kaimu Mkurugenzi Mifumo ya Kompyuta Bw. Mohamed Khamis akifafanua kwa waandishi wa habari kuhusu faida za vitambulisho vya taifa leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji Vitambulisho Bw. Alphonce Malibicha na kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi. Rose Mdami. Baadhi ya waandishi wa habari wakiangalia video ya faida za vitambulisho vya Taifa iliyoandaliwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili ya kuelimisha umma kwenye mkutano wa Mamlaka hiyo na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Picha na Fatma Salum (MAELEZO). Frank Mvungi-Maelezo Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeanza kutoa vitambulisho vya Taifa vyenye saini ya mwombaji kuanzia mwezi Juni mwaka huu. Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Mamlaka hiyo Bi. Rose Mdami wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. Akifafanua Mdami alisema kuwa lengo la Mamlaka hiyo ni kuhakikisha kuwa Watanzania wote wanapata vitambulisho vya Taifa ambapo katika hatua ya kwanza mamlaka hiyo inachakata taarifa za wananchi walizotoa wakati wa kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.Utoaji wa vitambulisho hivi vyenye saini ya mwombaji utasaidia kuwatambua wahusika pale wanapohitaji huduma mbalimbali za kijamii. “Upatikanaji wa vitambulisho vyaTaifa utasaidia Serikali kuondokana na tatizo la Watumishi hewa kwa kuwa mfumo wetu utaunganishwa na mifumo mingine inayosimamia utumishi wa umma” alisisitizaMdami. Utoaji huo wa vitambulisho utaanza kwa kutoa namba za utambulisho kwa wananchi ilizisaidie katika upatikanaji wa huduma mbalimbali wakati mchakato wa kuzalisha vitambulisho hivyo ukiendelea.Mdami alifafanua kuwa baada ya kuchakata taarifa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi zitarudishwa kwenye mitaa na vijiji husika kwa ajili ya uhakiki wa taarifa hizo. Lengo la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ni kuhakikisha kuwa ifikapo Desemba mwaka huu wananchi wote wawe wamepatiwa namba ya utambulisho . MAKONDA KUZINDUA MAONYESHO YA KWANZA YA SIMU ORIGINAL (SIMU EXPO). Friday, June 10, 2016 Maoni: 0 Na Daudi Manongi-MAELEZO. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda atazindua maonyesho ya kwanza ya simu original katika viwanja vya Posta jumamosi ya Tarehe 11 mwezi huu kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 12 jioni. Lengo kuu la kufanyika kwa maonyesho hayo ni kuwapa elimu wateja wa simu kujua ipi ni simu fake na ipi ni original kutoka kwa makampuni hayo ya simu,pia kwa kushirikiana na TCRA watatoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya simu na mitandao ya kijamii. Lengo la tatu ni kuhakikisha wateja wanajipatia simu original kwa bei nafuu kabla ya simu fake kuzimwa tarehe 16 mwezi huu.Nae Kaimu Katibu mtendaji wa Baraza la watumiaji wa huduma za mawasiliano(TCRA-CCC),Mary Msuya amewashauri watumiaji wa simu nchini kununua simu katika maduka ya simu na kuomba risiti ya dhamana ya muda wa matumizi ya bidhaa usiopungua miezi 12. Aidha aliwataka wafanyabishara wasio waaminifu kuacha mara moja kuingiza bidhaa feki nchini kwa njia za panya kwani serikali iko makini katika kusimamia suala hilo.Kwa upande wake mwakilishi wa makampuni ya simu Meneja mauzo wa kampuni ya Tecno Bw.Fred Kadilana ametoa wito kwa watumiaji wa simu kuja kwa wingi ili kujipatia simu zenye ubora wa hali ya juu kutoka kampuni mbalimbali. Wateja wa simu za mkononi watajipatia simu original kutoka katika maonyesho hayo kwa bei nafuu kutoka kwa makampuni ya simu ya Samsung,Tecno,Startimes,Huawei na Itel uku kukiwa na ushiriki wa makampuni ya simu ya Vodacom,Tigo na TTCL. Katika maonyesho hayo Taasisi mbalimbali za serikali zitashiriki kama mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRA-CCC) na Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF). RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AWAAPISHA MAJAJI WAWILI JUNE 10, 2016 Friday, June 10, 2016 Maoni: 0 HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA YAKAMILISHA MIRADI MITANO YA MAJI Friday, June 10, 2016 Maoni: 0 Na Lilian Lundo –Maelezo. 10/06/2016 Halmashauri ya Mji wa Kibaha imeeleza kuwa upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa mji huo kwa sasa ni asilimia 56 kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri hiyo. Akiongea kwa njia ya simu Afisa Habari wa Halmashauri hiyo Bw. Innocent Byarugaba amesema kuwa Halmashauri ina jumla ya miradi 11 ya maji ambayo mitano imekamilika na sita iliyobaki iko katika hatua za mwisho. “Maji safi na salama yanapatikana kwa asilimia 56 ikiwa ni juhudi za Halmashauri za kukabiliana na tatizo la maji na mpaka sasa miradi mitano imekamilika ambayo hutoa huduma ya maji kwa wananchi,” alisema Bw. Byarugaba. Katika kuhakikisha huduma ya upatikanaji wa maji unakuwa bora zaidi, Byarugaba amesema kuwa jitihada za kukamilisha upatikanaji wa maji unafikia asilimia 100 ambapo wanaendelea kukamilisha miradi mbalimbali inayofanywa na Halmashauri hiyo. Aliongeza kwa kutaja miradi iliyokamilika kuwa ni pamoja na Mradi wa maji Mtaa wa kwa mfipa Galagaza kata ya Msangani, Vikawe kata ya Pangani, Sagale kata ya Viziwaziwa, Zojosa kata ya Misugusugu na Mwanalugali kata ya Tumbi. Aidha alianisha miradi mingine ya maji inayotegemewa kukamilika kwa mwaka wa fedha 2016/17 kuwa ni mtaa wa Sofu kata ya Sofu, Muheza kata ya Mailimoja, Kibenge kata ya Msangani, Kibugalo kata ya Visiga, Kalabaka kata ya Misugusugu na Mikongeni kata ya Viziwaziwa. Bw. Byarugaba alitoa wito kwa kuwataka wananchi kuwafichua watu wanaokata mabomba ya maji na kujiunganishia maji kinyemela kwani kwa kufanya hivyo kunapunguza kasi ya maji na kusababisha watu wengine kukosa maji. Habari Zilizopita Search MICHUZI JR KUMBU KUMBU BLOG MBALI MBALI VYOMBO VYA HABARI COMPUTER PROBLEMS? CLOUDS FM TIMES FM PPF PENSIONS FUND SIMU TV MIMI NA TANZANIA FLORA SHOW KANDANDA CHEKA NA KITIME E

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Shaaban Ali Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali kuwa Jaji Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Shaaban Ali Lila(kushoto) pamoja na Jaji kiongozi Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali, wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othmani mara baada ya tukio la uapisho wa Majaji hao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Shaaban Ali Lila(kushoto) pamoja na Jaji kiongozi Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali, wengine katika picha ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othmani pamoja na Majaji mbalimbali wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Oman hapa nchini Soud Al Ruqaishi ambaye anamaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Picha na IKULU.

No comments:

Post a Comment