Wednesday, 22 June 2016

MKUTANO WA USHIRIKIANO WA VYOMBO VYA HABARI KATI YA NCHI ZA AFRIKA NA CHINA UNAOFANYIKA MJINI BEIJING NCHINI CHINA

N5Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akieleza jinsi Tanzania ilivyofanikiwa kuhama kutoka mfumo wa urushaji wa matangazo ya Televisheni kutoka Analogia kwenda Digitali katika mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za  Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.
N1Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (Kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel wakiwa katika ukumbi wa mikutano leo kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za  Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.
N2Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (Katikati), Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Star Media Tanzania Liao Lanfang wakibadilishana mawazo leo  kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.
N3Mkutano wa Ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya nchi za Afrika na China ukiendelea mjini Beijing nchini China.
N4Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la  Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Zamaradi Kawawa wakibadilishana mawazo  leo kabla ya kuanza  kwa mkutano wa tatu wa ushirikiano wa vyombo vya Habari kati ya nchi za Afrika na China unaofanyika Beijing nchini China.
Picha na Mpigapicha wetu

No comments:

Post a Comment