Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe Abdallah Jassim Al Maadadi Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe Abdallah Jassim Al Maadadi baada ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge Mstaafu na mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Spika wa Bunge Mstaafu na mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni. PICHA NA IKULU.
Tanzania inatarajia kufungua Ubalozi wake nchini Qatar kwa lengo la kuendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo huku ikitilia mkazo katika sekta za gesi asilia, utalii, usafiri wa anga na mawasiliano.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema hayo leo tarehe 16 Juni, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe. Abdallah Jassim Al Maadadi.
Pamoja na kutangaza kuufungua Ubalozi wake nchini Qatar Dkt. Magufuli amemuomba Balozi huyo kufikisha ujumbe kwa Kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Qatar kwamba zipo fursa nyingi za ushirikiano zinayoweza kufanyiwa kazi, huku akibainisha uwepo wa gesi asilia zaidi ya futi za ujazo Trilioni 57 na mpango wa kufufua shirika la ndege la taifa (ATCL).
"Najua Qatar ina uzoefu katika maeneo hayo na sisi Tanzania tungependa tushirikiane nanyi kuwekeza na kubadilishana uzoefu ili fursa hizo zilete manufaa kwa pande zote mbili" Amesema Rais Magufuli.
Kwa upande wake Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe. Abdallah Jassim Al Maadadi amemshukuru Rais Magufuli kwa nia yake ya kufungua Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar na kuimarisha zaidi ushirikiano na uhusiano na nchi hiyo, na amemuahidi kufikisha ujumbe kwa Kiongozi wa Qatar na Jumuiya ya wafanyabiashara wa nchi hiyo ili waje kuwekeza Tanzania.
Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambaye pia Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda, Ikulu Jijini Dar es salaam.
Baada ya mazungumzo hayo Mhe. Makinda amesema mazungumzo yao yameuhusu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na kwamba amemhakikishia kuwa amejipanga kuhakikisha mfuko huo uliobeba matumaini ya huduma za matibabu ya watanzania unaboreshwa zaidi na dosari zinazolalamikiwa na wanachama zinafanyiwa kazi.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
16 Juni, 2016.

No comments:
Post a Comment