Saturday, 25 June 2016

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO YATOA ELIMU YA UBIA KATI YA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI KWA WABUNGE


1Mgeni Rasmi, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akifungua Semina  iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango kuhusu Ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta  ya Umma ilifofanyika leo Mjini Dodoma katika ukumbi wa Pius Mswekwa ikiwa na Lengo la kuwajengea uwezo wabunge kuhusu umuhimu wa kushirikisha Sekta Binafsi katika miradi ya maendeleo.
2Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu Bunge Vijana Kazi Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama(wa kwanza kushoto) akifuatilia Semina iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango ikilenga kuwajengea uwezo wabunge kuhusu umuhimu wa kushirikiana kati ya Sekta Binafsi na ile ya Umma (PPP) Katika miradi ya maendeleo. Kulia ni Spika wa Bunge Mhe. Tulia Ackson ambaye alikuwa mgeni rasmi katika semina hiyo.
3Mbunge wa Ileje Mhe. Janet Mbene akitoa maoni yake  wakati wa semina ya kuwajengea uwezo wabunge kuhusu  umuhimu wa kushirikisha Sekta Binafsi katika miradi ya maendeleo.
4Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Sophia Simba akitoa maelezo  jinsi miradi itakayotekelezwa kwa ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi inavyoweza kuchangia kukuza maendeleo.
5Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) ambaye alikuwa mgeni rasmi  wa semina ya kuwajengea uwezo Wabunge kuhusu umuhimu wa Ubia kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma (PPP) akifurahia jambo mapema leo Bungeni Mjini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bajeti Mhe. Josephat Kandege.

No comments:

Post a Comment