Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhe. Amani K. Mwenegoha amewataka waandishi wa habari nchini kufanya kazi zao kwa ueledi na kwa ufasaha kwa kuzingatia misingi na maadili ya taaluma za uandishi wa habari wakati wakifanya kazi za uandishi.
Mhe. Amani K. Mwenegoha ameyasema hayo jana akikanusha taarifa zilizoandikwa kwenye gazeti la Mwanahalisi na mwandishiAnsbert Ngurumo toleo na: 341 la Mei 30 mwaka 2016 siku ya Jumatatu ukurasa wa 10 na 11. Alisema katika gazeti hilo lenye kichwa cha Habari kinachosema “Ngono na Mwanafunzi yaleta msukosuko Ushirombo” mimi kama Mkuu wa Wilaya ya Bukombe nimetuhumiwa kutumia madaraka yangu vibaya kwa kumlinda na kumkingia kifua Afisa Tarafa wa Siloka Bw. Tumbo John Madaraka.
“Sikuwahi Kupokea barua yeyote kutoka kwa Matayo Paschal wala kuamrisha akamatwe ,pia sikuwahi kuzungumza na mwandishi yeyote kuhusu mtoto huyo,wala sijapokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Polisi Bukombe kuhusu mtoto huyo wala malalamiko yoyote kutoka kwa wazazi,mlezi au Mwalimu Mkuu wa Shule aliyosoma mwanafunzi huyo” alisema Mkuu wa Wilaya Mhe. Amani Mwenegoha akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Bukombe amekemea na kulaani kitendo cha mwandishi wa gazeti la Mwanahalisi kuandika habari bila kuzingatia maadili ya kiuandishi kwa kufika eneo la tukio na kuonana na walengwa sio kuandika habari za kupelekewa au kusikia mtaani, angezingatia kupata taarifa kwa pande zote mbili ili kupata taarifa zenye ukweli,uwazi na uhakika”.
Pia ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kuwa wazalendo na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika ujenzi wa nchi yetu kwa kufichua uovu utakaorudisha nyuma maendeleo ya jamii yetu badala ya kuweka vibonzo visivyowakilisha maslahi ya nchi yetu na kuvunja moyo juhudi zinazofanywa na Rais wetu za kuinua Uchumi.
Wakati huo huo, Mkuu wa wilaya ya Bukombe Mhe. Amani K. Mwenegoha amesisitiza wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kutoa taarifa kwa vyombo vya serikali haraka kadri inavyowezekana inapotokea wana tatizo linalohusiana na watoto wao wanapokutana na changamoto ambazo serikali inaweza kushughulikia na imekua ikifanyika hivyo pale ambapo mzazi,mlezi au jamii inapotoa malalamiko au taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ambapo yamekua yakishughulikiwa na sheria imekua ikichukua mkondo wake.
No comments:
Post a Comment