Diwani wa kata ya Meserani Mhe.Loti Naparana akimeza kingatiba ya Trakoma(Zithromax)wakati wa uzinduzi huo.
Mama wa boma bi.Himayo Merio (aliyeshika kikombe)akipokea kingatiba toka Kwa mhudumu wa afya ngazi ya jamii bi.Jamila Karanga.zoezi hili linafanyika katika jamii hiyo kwa kuwatembelea kaya kwa kaya.
Wananchi wa kijiji cha Meserani wakisikiliza hotuba toka mkuu wa wilaya (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa umezaji wa kingatiba za ugonjwa wa trakoma uliofanyika kwenye kitongoji cha Losingirani.
……………………………………………………………………………………………………
Na.Catherine Sungura-Monduli
Wilaya ya Monduli inatarajia kutoa kingatiba ya ugonjwa wa trakoma(vikope) wa watu wapatao 140,962 kwa ngazi ya jamii kaya kwa kaya hadi ifikapo mwezi julai mwaka Huu
Haya yamesemwa leo Na mkuu wa wilaya ya Monduli Fransic Miti wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji dawa katika kijijo cha Losingirani wilayani hapa
Miti alisema kila mtu yupo katika hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele”napenda kusisitiza kila mwanajamii ahakikishe kila mtu katika familia anatumia dawa hizi ili tuweze kupunguza kasi ya maambukizi ambayo ni tayari katika jamii yetu
Aidha aliahidi kulisimamia zoezi hili ipasavyo katika ngazi zote kwani vifaa vyote vya utekelezaji wa zoezi hili vimeshawafikia katika wilaya Nzima
Mkuu wa Wilaya alisema kwa mwaka uliopita wilaya yake imetekeleza zoezi la ugawaji wa dawa za kudhibiti magonjwa ya kichocho na minyoo ya tumbo kwa watoto wenye umri wa kwenda shule kwa ufanisi mkubwa ambapo kati ya watoto 29,427,watoto 28,205 walipatiwa kingatiba ambayo ni sawa na asilimia 95.8
Hata hivyo alisema kwa zoezi la mwezi wa tano mwaka huu la umezaji dawa za minyoo zilitolewa kwa watoto 31,150 sawa na asilimia 97.3 kati ya watoto 32,000.
Naye Mratibu wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa
Hayapewi kipaumbele toka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Upendo Mwingira alisema maambukizi ya ugonjwa wa vikope(trakoma) upo kwa kiwango cha juu kwenye maeneo ya wafugaji ambapo asilimia 57 ya watu waliofanyiwa utafiti mwaka 2004 hadi 2006 ilionesha wana tatizo la vikope hasa wilaya ya Monduli,Longido pamoja na Ngorongoro.
Inakadiliwa hadi kufikia mwaka 2020 dunia nzima iwe imetokomeza ugonjwa huu kwa kugawa dawa ambazo ni tiba na kinga

No comments:
Post a Comment