Wakufunzi wa mafunzo ya Uongozi kutoka Chuo cha Uongozi Institute Dkt. Jochen Lohmeier (kushoto) na Nathaniel Mjema wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza mafunzo ya siku tatu kwa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wa Serikali ya Zanzibar yaliyofanyika katika Ofisi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Maisara Mjini Zanzibar.
Mkufunzi Nathaniel Mjema akiwasilisha mada ya kujitathmini kwa viongozi wanaoshiriki mafunzo ya uongozi yaliyowashirikisha Makatibu wakuu na wasaidizi wao.
Waratibu wa Mafunzo hayo wakifuatilia kwa kina uwashilishwaji wa mada mbali mbali zilizowasilishwa katika mafunzo hayo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum akitoa mchango katika mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya Maendeleo endelevu yaliyowashirikisha Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu wa Serikali ya Zanzibar.
Dkt. Jochen Lohmeier kutoka Uongozi Institute akitoa mada kuhusu kuitathmini Jamii katika mafunzo ya Makatibu wakuu na Wasaidizi wao yanayofanyika Ofisi ya CAG Maisara, Mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Ali Khalil Mirza (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Juma Ali Juma wakinakili mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakibadilishana mawazo na kujadiliana kutokana na kazi waliyopewa na wakufunzi wao.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
No comments:
Post a Comment