AccessBank
yaendelea kuwakumbusha wateja kuweka fedha kwenye akaunti zao za”RAHISI
inayowezeshwa na AccessMobile” na kisha wafanye miamala mingi ili
waokoe muda na pesa zao.Sambamba na hilo, pindi mteja afanyapo miamala
mingi, unaweza kujishindia simu mpya ya kisasa”brand new smart phone”.
Pichani
(kushoto) ni mmoja wa wateja ambao wamewahi kujishindia zawadi ya simu
mpya na ya kisasa aina ya Huawei P8 kwa kufanya miamala mingi zaidi
kupitia huduma maridhawa ya “RAHISI inayoweshwa na AccessMobile.
Mr
Amos Masunga (mmoja wa wateja ambao wamewahi kujishindia zawadi ya simu
mpya na ya kisasa), akipongezwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa AccessBank
Tanzania, Mr. Roland Coulon.
Akitoa maoni juu ya hili, Meneja Masoko wa AccessBank, Bw. Muganyizi
Bisheko, alisema kuwa, “inafurahisha sana kuona huduma hii inafanya vizuri
na imeweza kukidhi kisawa sawa mahitaji ya wateja. tutaendelea kuwaweka wateja
wetu mbele na kuwazadia kwa uzalendo wao na uaminifu wao katika kutumia huduma
zetu.”
“Ningependa kuwashauri wateja waendelee
kutumia mfumo wetu wa bure wa huduma za kibenki kwa njia ya simu, wafanye
miamala mingi na wawashauri ndugu na jamaa kujiunga na mfumo huu kwa kutembelea
tawi lolote la AccessBank huu ili nao waweze kufurahia miamala ya bure na
kufuzu kwenye mfumo huu wa zawadi.”
Mnamo
1/5/2015 AccessBank ilizindua huduma maridhawa ya “RAHISI inayowezeshwa na
AccessMobile”, huduma inayomuwezesha mteja kupata huduma zote za kibenki bure
kupitia simu ya mkononi kama ifuatavyo;
·
kupata akaunti Bure isiyo na gharama
za uendeshaji
·
kuweka na kutoa fedha Bure
kwenye tawi lolote la AccessBank
· Kuhamisha
Fedha Bure: Kwenda Akaunti ya Benki/M-pesa/Airtel Money/Tigo Pesa.
· · Kulipia
Bili Bure: Luku/Dawasco/DSTV na nyinginezo.
· Kupata
taarifa za akaunti Bure: Kujua salio, kupata taarifa fupi.
· · Kuongeza
salio Bure: Vodacom/Airtel/Tigo/Zantel.
Ili
kujiunga na huduma hii mteja anatakiwa kutembelea tawi lolote la AccessBank
lililo karibu nae na kisha atakua anapiga *
150*43# kufurahia huduma mbalimbali za Bure za kibenki mahali popote kupitia
simu ya mkononi. Kwa maelezo zaidi mteja anaweza kupiga; 0659 074000, 0784 108500
AccessBank Tanzania ni Taasisi ya Kifedha inayolenga kutoa
huduma za kibenki kwa wajasiriamali wadogo na wa kati. kupitia wanahisa wake wa
kimataifa amabao ni AccessHolding, International Finance Corporation (Word
Bank), KfW, African Development Bank na MicroVest, maono ya benki ni
kujidhatiti katika uanzishaji wa mifumo ya kifedha unayochochea maendeleo ya
jamii kwa kutoa huduma zilizobora kwa watu wote.
No comments:
Post a Comment