Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata ufafanuzi wa mikakati ya uwekezaji kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KOYO ya Japan, Bw. Norio Shoji wakati alipokutana na ujembe wa kampuni hiyo ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Viongozi wa Kampuni ya Japan ya KOYO na kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited ambazo kwa pamoja zimekusudia kushirikiana ili kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam May 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KOYO ya Japan, Bw. Norio Shoji baada ya kukutana na Mtendaji huyo na ujumbe wake ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9, 2016. Kampuni hiyo ikishirikiana na Kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited inakusudia kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Japan ya KOYO na kampuni ya Kitanzania ya SSF Limited ambazo kwa pamoja zimekusudia kushirikiana ili kuwekeza kwenye miundombinu ya umeme wa gesi asilia na jua nchini. Waziri Mkuu alifanya mazungumzo na viongozi hao ofisini kwake jijini Dar es salaam May 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment